MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Wednesday, 26 March 2014

UJENZI DARAJA KIGAMBONI WAINGIA SURA MPYA


Ni baada ya kufikia hatua za kuridhisha katika ujenzi wake
Meneja wa Mradi wa ujenzi wa daraja la Kigambonio Bw. Lin Tao kutoka kampuni ya China Railway Construction Engineering Group and  Major Bridge Co. Ltd (CRCEG-MBEC JV) akionesha jinsi ambavyo daraja la kigamboni litakavyoonekana baada ya kukamilika. Kulia kwake ni Mratibu wa Mradi kutoka Wizara ya Miundombini Bw. Hussein Mativila. Daraja hilo kutoka Kurasini mpaka Kigamboni takribani kilometa moja litakuwa na njia sita kwa ajili ya magari.  Daraja hili linajengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa daraja la kigamboni kutoka kwa Bw Lin Tao (katikati) kulia kwake (mwenye tai nyekundu) ni Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Kongane ya Sekta za Uzalishaji. Wa kwanza kulia (mwenye suti nyeusi) ni Meneja wa Mradi kutoka NSSF, Bw Karimu Mataka
Mafundi wa Kampuni ya ujenzi wa daraja la Kigamboni wakisuka nondo katika moja ya nguzo zitakazoshika daraja hilo


Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Kongane ya Sekta za Uzalishaji, Bw. Maduka Kessy akisisitiza jambo wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa daraja la Kigamboni. Mbele yake ni Menaja wa Mradi kutoka Kampuni ya ujenzi wa daraja hilo (CRCEG-MBEC JV)
Na Mwanaharakati.

No comments: