MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Wednesday 30 April 2014

KUSHUKA KWA KIWANGO CHA ELIMU KAGERA HIKI HAPA



Wanafunzi wa Kidato cha Tano na sita, katika Shule ya Sekondari ya Lukole, iliyopo wilayani Ngara mkoani Kagera wanalazimika kutembea umbali wa kilomita saba kufuata huduma ya maji, kutokana na kuharibika kwa mashine ya kusukuma maji.

Akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi hao, wakati wa mahafali ya nne ya kidato cha sita, Ishengoma Edibily amesema kuwa kutokana na kuharibika kwa mashine hiyo, inayosimamiwa na idara ya maji, wanalazimika kukatisha baadhi ya masomo.

Ishengoma amesema kuwa, hali hiyo inawaathiri Kitaalaum kutokana na kutumia muda wingi wa kujifunza kutafuta maji.

Amesema kuwa mbali na shule hiyo kukabiliwa na ukosefu wa huduma ya maji, pia inakabiliwa na ukosefu nishati ya umeme na upungufu wa vitabu kwa ajili ya kufundishia na kujifunzia masomo.

Akizungumza katika mahafali hayo, Mkuu wa wilaya ya Ngara Bwana Costantine Kanyasu amesema kuwa, wananchi wa eneo la K9 wataondokana na tatizo la ukosefu wa maji baada ya kufungwa mashine na nishati ya umeme.

Bwana Kanyasu amesema kuwa, halmashauri ya wilaya ya Ngara tayari imepokea zaidi ya Shilingi milioni 80 kutoka Ofisi ya Rais, na kuwa mashine itakayofungwa katika chanzo cha maji cha K9 itasaidia kuwapatia maji wakazi wa eneo hilo.
Na Mwanaharakati.

UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE KUZIMA MAADHIMISHO YA UHURU WA HABARI

Waziri Mkangara
Katika maelezo ya Mh waziri kuhusu uzinduzi wa mbio za mwenge, amesema kuwa hasa vijana watumie mwenge huo kudumisha amani upendo na mshikamano, na kuongeza kuwa mbio hizo za mwenge wa uhuru zitafikia kilele chake tarehe 14 oct 2014 mkoani Tabora.
Kulia ni mkuu wa mkoa wa Kagera Mh Fabian Massawe, akifafanua jambo kwa wanahabari.
 Kaulimbiu ya mbio za mwenge 2014, ni "jitokeze kupiga kura ya maoni tupate katiba mpya"
 Katika mbio hizo za mwenge utazunguka na kufikia halmashauri/manispaa 165 za jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo mwaka jana ulizindua miradi yenye thamani ya zaidi ya bilioni 184 na milioni 578 na laki 6.
Hawa ni baadhi ya waandishi habari wakifuatilia kwa karibu


Siku ya uhuru wa habari, uhadhimishwa May2 kila mwaka, ambapo kwa waandishi habari huweza kuzungumzia uhuru wa kazi zao za kihabari, pamoja na kuzungumzia masuala yanayowakabili wanahabari na kazi zao katika maeneo ya kazi.

Kutokana na siku hiyo muhimu, waandishi habari wameona watumie nafasi hiyo kujua mikakati ya wizara yao kuhusu utekelezaji wa shughuli za kihabari, wizara inazungumziaje siku hiyo na kauli mbiu ya mwaka huu pamoja na kuzungumzia nafasi ya vyombo vya habari na wanahabari katika suala la upatikanaji wa katiba mpya, ila kwa Kagera wamegonga mwamba kuzungumza na waziri, ilhali na naibu wake Juma Suleiman Nkamia naye akiwa Kagera katika mikakati hiyohiyo ya mwenge.
Na Mwanaharakati.

Tuesday 29 April 2014

NEWS ALERT!!!ABIRIA WANUSURIKA KIFO BAADA YA BASI LA HOOD KUTEKETEA KWA MOTO



Basi la Kampuni ya Hood, lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Arusha limeteketea kwa moto jana jioni eneo la Wami mkoani Pwani.
Taarifa zinasema kuwa hakuna majeruhi wala aliyepoteza maisha katika ajali hiyo.
 

Na Mwanaharakati.

WAANDISHI WATAKAORUHUSIWA KURIPOTI HABARI ZA BUNGE LA BAJETI

Mkurugenzi wa habari maelezo




HIVYO BASI TUNAOMBA ORODHA YA WAANDISHI WAKO NA WAPIGA PICHA WAKO WATAKAOSHIRIKI KURIPOTI TUKIO ZIMA KUANZIA MWANZO HADI MWISHO WA BUNGE HILO. TAFADHALI LETE MAJINA YA WAANDISHI WAKO MAANA BAADA YA KUPELEKWA HAKUTAKUWA NA NAFASI YA KUONGEZA.

VITU VINAVYOTAKIWA;-
    1. AWE NA PRESS CARD 2014
    2. MAJINA YAJE KATIKA BARUA RASMI.
    3. MAJINA YALETWE KABLA YA SAA 6.00 MCHANA 30.5.2014

UTAWALA- MAELEZO
Na Mwanaharakati.

MALI ZA MZEE GURUMO ZAGOMBANIWA


 Kwa mujibu wa chanzo ambacho ni ndugu wa karibu wa familia hiyo, siku moja baada ya msiba, mtoto huyo alitangaza kuwa gari hilo ni lake na akaanza kutafuta madalali wa kuliuza gari hilo lakini akakwamishwa na kukosekana kwa kadi ya gari.

“Yaani hawa watoto wa marehemu sijui wana nini jamani, hata arobaini ya baba yao bado wameanza kushikana mashati, hii ni hatari sana. Huyo mmoja ndiyo anajitapa kabisa kuwa gari ni la kwake na ameshaanza kutafuta mteja,” kilisema chanzo chetu kwa masharti ya kutotajwa gazetini.
 Mtoto wa marehemu, Mariam Gurumo ambaye alipoulizwa kuhusu ishu hiyo, alisema: “Aliyekupa hizo taarifa ni muongo, hakuna ishu kama hiyo. Kwanza bado tunaomboleza kifo cha baba yetu. Sasa tuuze gari na nyumba ili iweje? Siyo kweli.

“Ni kweli kuna kesi ya nyumba ipo mahakamani lakini siyo nyumba hiyo unayoisema. Unajua sisi watoto wa Gurumo tunataka kudhulumiwa nyumba iliyoachwa na marehemu mama yetu iliyopo Ilala. 

“Unajua huyu mjane wa marehemu, hakubahatika kupata mtoto, sisi mama yetu ni marehemu na tulizaliwa wanne, mimi (Mariam), Mwalimu, Mwazani na Omary.

“Abdallah yeye ana mama mwingine lakini ni ndugu yetu wa damu. Kabla mama hajafa, Gurumo alimjengea nyumba Ilala.
“Sasa mama yetu alipokufa, mdogo wake (jina tunalihifadhi) akawa anataka kuiuza, hivi jana tu (Ijumaa) tumetoka mahakamani. Tumefungua kesi pale yenye jalada namba RB/IL/112/2013 kuzuia nyumba kuuzwa. Tunashukuru mahakama imeingilia kati vinginevyo tungedhulumiwa.

Naomba watu wasichanganye, nyumba yenye matatizo ni ya Ilala. Kuhusu gari, kwa sasa bado hatujaamua chochote mpaka arobaini ipite,” alisema Mariam.
Mariam Gurumo



“Ni kweli nyumba inauzwa. Hilo lilikuwa ni agizo la mume wangu kabla hajafariki, aliniambia ni bora aiuze kabla hajafa kwani anawajua wanaye watanisumbua sana pindi akifa.
“Tulianza kutafuta wateja miezi minne kabla Gurumo hajafa, bahati mbaya ametangulia kabla hatujakamilisha hiyo kazi. Yeye alikuwa na lengo zuri la kutaka atugawie kila mmoja chake ili akifa yasitokee haya yanayotaka kutokea.

“Unajua hii nyumba tumejenga na mume wangu, mimi nilikuwa mfanyabiashara na tulisaidiana kabla hata hawa watoto hawajazaliwa lakini nashangaa wanataka kunigeuka eti mimi sihusiki.”
“Naomba serikali iingilie kati kwenye hili suala, nyumba wala gari viziuzwe kwanza. Jamani hata eda sijamaliza mambo yameanza kuwa hivi.

Hao watoto wenyewe tangu tumzike baba yao hawajakanyaga hata hapa nyumbani kunijulia hali, sijui wanafikiria nini kuhusu mimi, naomba mnisaidie nimalize eda salama na mali zikiuzwa, basi na mimi nipewe staahili yangu,” alisema mjane huyo kwa huzuni.

Na Mwanaharakati.