MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday 29 September 2011

Ni askari wa usalama barabarani alipomwita kondakta wa bas la ZUBER likitokea ARUSHA kwenda mwanza.

Ni katika barabara ya Babati mkoani arusha ambapo basi la kampuni ya ZUBER likiwa linatokea Arusha kulekea mwanza lilionekana kuwa na mapungufu katika safari hiyo jambo lililopelekea kusimamishwa mara kwa mara askari wa usalama barabarani.

Baada ya kusimamishwa askari hawa wamekuwa wakimwita pembeni kondakta wa gari hiyo na katika kile kinachooneka katika video hii ni pale askari wakipokea kitu kunachosadikika kuwa ni hela.

Abiria waliokuwa katika gari hiyo ususani wale waliozoea kusafiria magari ya kampuni hiyo wamesema magari yanayoonekana kuwa na mapungufu usimamishwa kila wanapokutana na askari kwa sababu askari hao upeana taarifa ni jinsi gani watakavyozungumza nao kuhusu chochote.
Ni mchanganyiko wa magari ya binafsi na ya biashara lakini yote yakisubiri abiria katika stendi ya Bihalamuro.

Katika stendi ya mabasi wilayani bihalamuro mkoani kagera kumekuwa kukithiri kwa matumizi ya magari binafsi kubeba abiria jambo ambalo ni kosa katika taratibu za usalama barabarani.

Madereva na makondakta wanaotumia stendi hiyo wamesema kuwa kila siku magari yao ukaguliwa askari wa usalama barabarani na jambo hilo analiona lakini kutokana na kuwa inasemekana wenye magari hayo wanafahamiana na mengine ni baadhi ya askari hao jambo hilo linaendelea kuwepo.

Pia wamesema inavunja moyo wale ambao wanafuata sheria za biashara hiyo na tofauti na hiyo magari hayo kiuka taratibu kwa kujaza abiria kupita kiasi lakini askari uangali na kuona kinachoendelea.

Stendi ya Bihalamuro ipo katika wilaya hiyo na inahusisha magari yaendayo sehemu mbalimbali nchini.
Kwa taratibu za nchi ni kosa gari binafsi kufanya biashara ya kusafirisha abiria lakini baadhi ya maeneo magari haya utumika kwa kificho lakini katika wilaya ya bihalamuro jambo hili ni waziwazi, hapa ni stendi ya magari wilayani hapo na hii ni mojawapo ya magari yaliyosubiri abiria karibu na kituo kidogo cha polisi.

Thursday 22 September 2011

Mgeni rasmi katika mechi ya KAGERA SUKARI na JKT OLJORO ambapo kagera wametandikwa 2-1

Kagera sugar katika mechi hiyo ilitandikwa mambao mawili yote yakiingizwa kimiani na AMIR OMAR  katika DK 4 na bao la pili DK-25.

Bao la kufuta machozi kwa KAGERA SUGAR lilipatikana kwa njia ya penati baada ya beki yake kumfanyia madhambi mchezaji wa kagera sugar katika DK 54 iliyofungwa na TEMISTOCRES FELIX (MNYAMA).

Mechi hiyo imepigwa tarehe 22/09/2011.

Monday 19 September 2011

Trafic anaposimamisha gari ya abiria na kondakta akaitwa faragha, abiria wanajifikiliaje?(HAPA NI MOJAWAPO YA VITUO VYA ASKARI WA USALAMA BARABARANI MKOANI DODOMA)
Baada ya kubainika amepora viatu raia wamehamua kujichukulia sheria mikononi sasa kujana huyu atapona jamani?
Sukari ikiwa katika bei ya shilingi 2500 kwa kilo katika maduka bado upatikanaji wake umeleta shida na hapa katika kituo cha uuzaji sukari cha KAGERA SUGAR njini bukoba na hawa ni wafanyabiashara.

Katika kipindi cha karibuni imetangazwa operesheni ya kukamata wanaovusga sukari hiyo kwenda nchi za nje kutokana na kuadimika kwa bidhaa hiyo hapa nchini jambao ambalo linaonekana kuleta mafanikio kwa kiasi kikubwa.

Wiki hii mkoani kagera askari walifanikiwa kukamata kiasi flani cha sukari na kukirudisha mikononi mwa serikali lakini kinachosikitisha ni kuwa sukari hiyo inauzwa kwa bei ya shilingi laki moja tofauti kabisa na aagizo la waziri mkuu kwamba ikikamatwa iuzwe kwa bei ambayo wenye maduka watauza kwa kilo shilingi 1700.
Hawa ni baadhi ya waandishi habari mkoani kagera wakitokea uwanja wa ndege wa Bukoba huku wakingali wakionesha maskitiko yao baada ya kukosa nafasi ya kuzungumza na mkuu mpya wa mkoa kuhusu mikakati atakayoanza nayo.

Imeshakuwa deturi kuwa anapowasili kiongozi kuanza kazi rasmi inakuwa ni vizuri kuapata kutoa mikakati yake anapowasili eneo la kazi lakini imekuwa tofauti kwa mkuu huyo mpya wa mkoa wa kagera kutozungumzia mikakati aliyokuja nayo ukizingatia amekuwa akifanya mambo makubwa wilayani karagwe wakti kimkoa bado yameendelea kuleta tabu watu walitaka kujua yuko tayari kuyakomalia?

Jmabo moja kubwa ni pale alipopunguza kiasi kikubwa cha kuwapatia mimba wanafunzi lakini pia aliwahi kusema mwenyewe kwamba atatafuta ufumbuzi katika suala la sukari.
Mkuu mpya wa mkoa wa Kagera FABIAN MASAWE akipokelewa na mwenyeji wake aliyemaliza muda wake MOHAMMED BABU
Nicolaus Mac Mwanaharakati wa kweli asiyefungamana na upande wowote,jamani na anza namna hii kwa habari mototo.