MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday 2 August 2016

SAMAHANI KWA KUTOKUWA HEWANI

Hii ni baada ya kuwa kwenye marekebisho na utafiti wa masuala kadhaa ya kijamii, tunarejea sasa kwenye majukumu.

Monday 4 January 2016

SERIKALI YAVUNJA UHUSIANO



Bahrain imetangaza kwamba imevunja uhusiao wa kibalozi na Iran, saa chache baada ya Saudi Arabia kuchukua hatua sawa.

Saudi Arabia iliwapa wanabalozi wa Iran siku mbili kuondoka nchini Saudi Arabia kufuatia mvutano uliotokana na kuuawa kwa mhubiri maarufu wa Kishia.

Bahrain hutawaliwa na Mfalme Msuni lakini raia wengi ni wa dhehebu la Shia.
Ufalme huo pia umewapa wanabalozi wa Iran saa 48 wawe wameondoka nchini humo.

Sudan nayo imemfukuza balozi wa Iran kutoka Khartoum huku muungano wa Jumuiya ya Milki za Kiarabu UAE nayo ikipunguza idadi ya maafisa wa ubalozi. Waislamu wengi nchini Sudan ni Wasuni.
Mhubiri huyo Sheikh Nimr al-Nimr aliuawa pamoja na watu wengine 46 baada ya kupatikana na makosa yanayohusiana na ugaidi.

Washia walishutumu hatua hiyo na maandamano yalishuhudia maeneo yenye Washia wengi.
Mjini Tehran, waandamanaji waliteketeza majengo ya ubalozi wa Saudi Arabia.

Saudi Arabia na Iran ndiyo mataifa makuu ya Kisuni na Kishia mtawalia Mashariki ya Kati, na yamekuwa yakiunga mkono pande pinzani katika mizozo inayoendelea Syria na Yemen.
Kuna wasiwasi huenda machafuko yakatokea kanda hiyo.

Jumatatu, misikiti miwili ya Wasuni ilishambuliwa na imam mmoja akauawa.
Saudi Arabia ilitangaza kwamba imekatiza uhusiano wake na Iran baada ya maandamano yaliyotokea ubalozi wake mjini Iran. Ilisema pia kwamba imemwagiza balozi wake arejee nyumbani.

Wizara ya mambo ya nje ya Iran imesema Saudi Arabia inaendeleza sera ya kuzidisha chuki na makambiliano katika kanda hiyo.

Msemaji wa wizara hiyo Hossein Jaber Ansari alisema Jumatatu kwamba Saudi Arabia inajaribu kusuluhisha matatizo yake ya kinyumbani kwa “kuyatoa nje kwa mataifa mengine”.
 

Na Mwanaharakati.

MAHAKAMA KUTOA HUKUMU BOMOABOMOA

Mbunge wa Kinondoni, Maulidi Mtulia akihojiwa na waandishi baada ya kutoka katika mahakama Kuu ya ardhi
Umati wa wananchi wa Mabondeni ikiwemo bonde la Msimbazi, Magomeni Mkwajuni, Hananasifu, Magomeni Sunna, Kigogo  na maeneo mengine wa Jimbo la Kinondoni wamefurika kwa wingi mapema kuanzia asubuhi ya leo katika Mahakama Kuu ya Ardhi iliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam kusikiliza kesi ya msingi ya kupinga kubomolewa nyumba zao iliyofunguliwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Mh. Maulidi Mtulia (CUF).
 
Mtulia amefungua kesi hiyo kupinga kubomolewa kwa wakazi hao bila kuwa na njia mbadala ikiwemo kupatiwa makazi mengine kwa wananchi wake yenye usalama zaidi.

Hata hivyoi Modewjiblog iliyokuwa katika eneo la tukio tokea asubuhi, ilishuhudia umati mkubwa wa wananchi wakifurika katika viunga vya Mahakama hiyo kiasi cha kufanya shughulo zingine za mahakama hiyo kusimama.

Baada ya masaa matatu, Jaji wa Mahakama hiyo Kuu ya Ardhi, Mh. Panterine Kente aliweza kusimamia kesi hiyo huku baadhi ya wananchi wakiwakilishwa na wajumbe zaidi ya saba, pamoja na wanasheria wa Mbunge huyo, ambapo maamuzi yalidumu kwa muda wa saa zaidi ya saa moja,  na baadae Mawakili wa upande wa Mbunge wa Kinondoni, akiwemo Abubakari Salim aliweza kuutangazia wananchi hao pamoja na wanahabari kuwa, baada ya kupitia vielelezo vyote, kesi hiyo itatolewa hukumu kesho  siku ya Jumanne, Januari 5.2016.

“Kwa shahuri lililopo sasa linatarajiwa kutolewa jibu kesho  Januari 5, Saa tano asubuhi ndio tutapata jibu kamili, kwa sasa  tunarudi na tutakutana hapa hapa Mahakamani.” alieleza  Wakili huyo.

Na Mwanaharakati.

UKUSANYAJI KODI WA IKABILI HALMASHAURI YA MANISPAA



Afisa uhusiano manispaa ya Ilala Bi. Tabu Shaibu, amesema kuwa katika mwaka  wa fedha 2010/11, walipanga kukusanya bilioni 2.8 lakini wakakusanya bilioni 2.1, mwaka 2012/13 walipanga kukusanya bilioni 4, lakini walikusanya bilioni 1.8, na hivyo kusababisha hasara serikalini, ambapo katika mwaka wa fedha 2015/16 manispaa inatarajiwa kukusanya bilioni 11.5.

Amesema kuwa viwango vya kodi ya majengo vimetajwa kweenye kifungu namba tatu, kifungu  kidogo cha kwanza cha sheria ya ardhi nyumba na makaazi, ambapo imefafanuliwa kuwa nyumba ya biashara na viwanda inatozwa 0.2% ya thamani ya jengo zima , nyumba  ya makazi inatozwa 0.15% kwa mwaka, huku akitaja sababu mbalimbali za kushindwa kutimiza malengo ya ukusanyaji kodi.

Meneja wa kodi ya majengo  halmashauri ya manispaa ya Ilala Bw. Kajuna, imejipanga kuanza utaratibu wa kuchukua taarifa upya kwa usahihi, kurahisha huduma za malipo kupitia mitandao ya kijamii, na kuanza kutuma ujumbe kwa kila mlipa kodi kupitia simu ya mkononi, ili kukumbushia deni na jinsi ya kulipa.

Novemba 2015, serikali ilitangaza kuanza kutumika kwa mfumo wa kielektroniki yaani ulipaji kwa njia ya mtandao  Tehama, kukusanya kodi za majengo na huduma mbalimbali, huku ikianzisha dawati la usaidizi kwenye halmashauri zenye shida ya mtandao, ili kuondoa ulipaji kodi kwa muhasibu, baada ya kubaini upotevu wa fedha zinazolipwa.
 

Na Mwanaharakati.

UBADHILIFU SERIKALINI SABABU YATAJWA


.Ni ukosefu wa mwongozo
Serikali kupitia wizara ya fedha, inaandaa mwongozo mpya chini ya sheria ya fedha namba 38, ili kuondoa ubadhilifu unaojitokeza nchini.
Mkaguzi mkuu wa ndani wa serikali Bw. Mohamed Mtonga, amesema kuwa sheria ya fedha inaelekeza kuandaliwa kwa mwongozo huo,ambao utahakikisha majukumu ya idara yanatekelezeka kwa kuwezesha wakaguzi wa ndani wanatimiza majukumu yao kwa kina, na kuhakikisha masuala ya utawala bora yanatekelezwa ipasavyo.

Hatahivyo bwana Mtonga amesema kuwa, idara ya ukaguzi wa ndani ina taarifa nyingi na nzito kuliko za CAG, ila zinahishia kwenye utawala kutokana na mfumo uliopo, kwa kusisitiza kuwa kuna uwezekano halmashauri  kupata hati safi baada ya utafiti wa ndani lakini ikawa tofauti baada ya kufanyiwa ukaguzi na  mkaguzi mkuu wa serikali CAG.


Idara ya mkaguzi mkuu wa ndani wa serikali, inafanyakazi katika wizara ya fedha ikiwa na vitengo vya uhakika wa ubora, usimamizi viashiria hatarishi, ukaguzi wa bajeti na mishaara, ukaguzi wa kiufundi na kitengo cha ukaguzi wa serikali za mitaa, ambavyo kwa pamoja vinanafasi ya kufanya ukaguzi maalumu wa kiuchunguzi, kulingana na mahitaji ya kitengo husika. 

Na Mwanaharakati.