MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Friday 31 August 2012

WAZIRI MWANRI AFUNGA MKUTANO WA HALMASHAURI 130 KUTOKA MATAIFA YA KENYA, UGANDA, RWANDA, BURUNDI NA TANZANIA

 Pamoja na mambo mengine, waziri wa TAMISEMI amesisitiza matumizi mbadala ya mazingira ili kupunguza uchafuzi wa mazingira na utunzaji wake. Lakini zaidi washirki wameambiwa wakitembea kwenye mikutano kama hiyo wajifunze suala la utawala bora na mazingira, kwani kumekuwepo tabia ya watu kupata fursa za kutembea wakashindwa kujifunza wanabaki kununua nguo na vitu vya kifahari tu.
 Picha juu ni mbunge wa Bukoba vijijini Kason Rwehikiza akimkaribisha Mwanri ili kutoa hotuba ya ufungaji.
 Juu ni mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali mstaafu FABIEN MASSAWE pamoja na mwenyekiti wa umoja wa halmashauri hizo 130 za ukanda wa ziwa Victoria, wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na mshiriki kutoka SNV Mwanza. Na chini ni wananchi akiwemo menejea wa KIROYERA TOURS Wilium Rutta wakifuatilia mada hiyo.
 Chini ni mkuu wa wilaya ya Bukoba ZIPORA LION PANGANI katikati na meya manispaa ya Bukoba Dokta ANATOL AMAN kushoto, pamoja na mshiriki mwingine kutoka Uganda.
 Chini mkurugenzi wa UTT Dokta KIBOLA akihojiwa na waandishi habari kutoka vituo vya redio Kasibante na Vision.
 Dokta KIBOLA akiwa na Matrida Leopord Meneja Redio Vision.

Thursday 30 August 2012

AJALI AJALI AJALI - KIDUCHU

Ni baada yadereva kujikuta anashindwa kukata kona, na hatimaye kuacha  na kugonga mti na dereva ambaye hata hivyo hakutajajina na hakutaka kupigwa picha amejeruhiwa.



MADEREVA WA HACE WALIOKUWA WAMEGOMA SASA WAMEREJEA KAZINI BAADA YA MKUU WA WILAYA KUWASIHI WAREJEA HUKU HOJA YAO ITATULIWA BAADAYE

 Mkuu huyo wa Wilaya Bi Zipora Pangani aliambata na Meya wa Manispaa na kuwatahadharisha kuzua makubwa zaidi kwani wanapogoma hawawagomei viongozi wa manispaa bali usumbufu unaamia kwa abiria wanaotumia usafiri wao.
 Awali madereva hao waligoma kutokana na uhitaji wao wa kuondolewa kwa tozo la shilingi elfu mbili ambapo wanalazimika kulipa kila wanapoingia kwenye stendi ya Bukoba badala yake wangelipia mara moja tu kwa siku kwani kiasi hicho cha elfu mbili kila wanapoingiza gari ni kikubwa mno.


MKUTANO WA 11 WA HLMASHAURI 130 ZA EAC LVRLAC

Mkuu wa mkoa wa KAGERA, kanali mstaafu FABIAN MASSAWE, leo ameufungua rasmi Mkutano wa 11 wa Umoja wa  Halmashauri 130 kutoka UGANDA,    KENYA na TANZANIA,-   LVRLAC.
Katika hotuba yake ya ufunguzi kwa niaba ya rais JAKAYA KIKWETE, kanali MASSAWE amewakaribisha Wajumbe kutoka KENYA na UGANDA, pamoja na Halmashauri zinazozunguka Ziwa Victoria,Huku akiipongeza LVRLAC kwa mafanikio na kutoa ushauri kwa umoja huo.
Takriban Washiriki  450  wakiwemo  Wakurugenzi wa Halmashauri, Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri 28 za Tanzania wanahudhuria  mkutano huo, ambao unafanyika  katika viwanja vya GYMKHANA, katika  manispaa ya BUKOBA.
 Picha juu ni katika kuimba nyimbo za mataifa shiriki.

Washiriki wa Mkutano huo, jana, walishiriki katika shughuli za hifadhi mazingira na upandaji miti katika  maeneo mbalimbali ya Manispaa ya BUKOBA.
Hatua hiyo  ni kuunga mkono jitihada za Mkuu wa mkoa wa KAGERA, kanali mstaafu FABIAN MASAWE.

Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, bwana AGGREY MWANRI,  ambaye pia amehudhuria mkutano huo, anatarajia kuufunga  mkutano huo.
Kasibante fm Redio kama kawaida yetu tukarusha matangazo ya moja kwa moja kutoka viwanjani hapo.

Wednesday 29 August 2012

MAFUNZO YA MAADILI KWA WAANDISHI HABARI KAGERA YAFUNGWA RASMI

 Hata hivyo waandishi wenyewe, wamefrahia mafunzo hayo kwani yamewajengea uwezo katika kutambua uhuru wa habari, jinsi ya kushirikiana kati ya mmiliki, mwandishi mwenyewe na wananchi ambao ndiyo waajiri wakuu kwani ndiyo wanaoandikiwa na kutangaziwa habari.
 Wkati huo huo waandishi wamekubali kuliunga mkono azimio la Dar es salaam, ambalo limeahinisha masuala mbalimbali kuhusu utendaji wa kazi kwa wahariri na waandishi wa kawaida.
 Mafunzo hayo ya siku tatu yalifunguliwa rasmi tarehe 27 na kuhitimishwa 29 Agost 2012 katika ukumbi wa ELCT Bukoba Hotel, chini ni picha ya pamoja kati ya washiriki na wawezeshaji wao, Deodatus Mfugale na Chris Rweyemamu kutoka MCT.

MAANDALIZI YA MKUTANO WA 11 WA HALMASHAURI 130 NCHI ZA UGANDA, KENYA NA TANZANIA-LVRLAC

Mwenyekiti wa Umoja huo hapa nchini, Dk ANATOLI  AMANI amesema kuwa Mkutano huo wa LVRLAC,  utaenda sambamba na viongozi hao kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya manispaa ya Bukoba.

Hatua hiyo  ni kuunga mkono jitihada za Mkuu wa mkoa wa KAGERA, kanali mstaafu FABIAN MASAWE.
Wakurugenzi wa Halmashauri, Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri 28 za Tanzania ambao wanahudhuria  mkutano huo,  jana, walishiriki katika semina ya kuwajengea uwezo namna ya kubuni miradi ya maendeleo katika Halmashauri zao ili kuongeza mapato.

Katika semina hiyo,  baadhi ya Halmashauri zimependekeza miradi kadhaa ya maendeleo ambayo zitaitafutia wafadhili. 

Halmashauri  za mkoa wa KAGERA  kwa pamoja zimependekeza ujenzi wa maegesho mapya ya magari, ujenzi wa viwanja bora vya michezo,  pamoja na kuimarisha msitu wa BURIGI,  kuwa moja ya kivutio cha utalii mkoani KAGERA.

Akifunga semina hiyo ya siku moja, Mkuu wa wilaya ya BUKOBA, bi ZIPORRAH PANGANI  amewataka viongozi hao kujenga desturi ya kuwashirikisha wananchi katika kupanga na wakati wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
 Hapa juu ni ukumbi wa utakaotumika kufanya mkutano huo ambao hadi sasa uko kwenye maandalizi
 Kama ilivyo ada kunapokuwa upokeaji wa geni lazima usafi uzingatiwe, hii ni shimo la taka ambalo linakaa na uchafu muda mrefu lakini sasa naona itifaki imezingatiwa.