MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Friday 18 December 2015

WASTAAFU KULIPWA NDANI YA WIKI MOJA; WAZIRI ASHTUKIZA PSPF



Wizara ya fedha na uchumi imetoa siku 7 kwa mkurugenzi wa mfuko wa pensheni kwa wastaafu  PSPF, iwe imelipa mafao ya wastaafu wanayodai shirika hilo.
Naibu waziri wa fedha Dk. Ashantu Kijachi  amesema kuwa serikali imeshalilipa shirika hilo jumla shilingi bilioni 154, kati ya bilioni 177 walizokuwa wakidai serikali, akisisitiza kuwa kama fedha hizo zimelipwa hakuna sababu ya wastaafu kuendelea kutaabika na mafao yao, kuwa haiwezekani kwasababu wanaotakiwa kupewa kipaumbele na hilo ni jasho lao.
Amesema kuwa serikali imejiridhisha baada ya kupokea malalamiko kuwa hundi zao zimeandikwa tangu mwezi januari, ilhali haijulikani zinakopotelea.

Mkurugenzi mkuu wa PSPF Bwana Adam Mahingu, amesema kuwa wananchama wake
wengi ni watumishi wa serikali, na serikali imekuwa ikitakiwa kuleta michango, ingawa serikali ilikuwa haijalipa fedha za miezi saba lakini wiki hii shirika hilo limeandaa hundi za wastaafu 444, waliostaafu kwa kipindi cha kuanzia mwezi wa nne hadi wa kumi, pamoja na wanaodai mirathi 142.
Kumekuwa na mkanganyiko wa fedha za wastaafu, ambazo zinaonesha kuwa zimeshatoka serikalini, ambapo naibu waziri amesema kuwa katika miezi ya 11 na 12 mwaka huu, serikali imelipa bilioni 70 za kufunga mwaka, hivyo haikutegemea kuona malalamiko ya wastaafu na hili halikubaliki katika serikali ya awamu ya 5.
 

Na Mwanaharakati.

Thursday 17 December 2015

KAULI NZITO YA MACK BOMANI KUHUSU SIAZA ZA ZANZIBAR



Jaji mkuu mstaafu Mac Bomani, amesema kuwa mbadala pekee katika uchaguzi wa Zanzibar ni kuondoa dosari zilizobainika, siyo kuishinikiza tume kutangaza matokeo yaleyale.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kuonesha msimamo wake katika mambo kadha hapa nchini, jaj Bomani amesisitiza kuwa haiwezekani tume ya uchaguzi Zanzibar ikatangaza matokeo iliyoyafuta kwa sababu za kubainika makosa mbalimbali, kabla ya kuondoa dosari zilizobainika na kurudia uchaguzi, ili kuendelea kuaminika kwa wananchi.

Hatahivyo amesema kuwa mchakato wa katiba usiishie njiani kwani katiba inahitajika, hivyo baada ya uchaguzi wa Zanzibar ni muhimu lifuatiliwe kwani mengi yameshafanyiwa kazi kupitia waliohusika na mchakato huo hasa tume ya Warioba, kwani fedha nyingi imetumika na katiba mpya inahitajika.

Wakati huo jaj Bomani, amesema kuwa migogoro ya wakulima na wafugaji imekithiri nchini, jambo ambalo linasababishwa na kukosekana kwa mbadala kama ardhi ya kutosha hasa ya kufanyia malisho, na kuondoa taratibu za zamani zinazotumika kwa mfugaji mmoja kufuga ng’ombe elfu moja, ilhali hawezi kuwapa huduma ya kutosha, hivyo serikali iangalie katika sekta hiyo.

Ameitaja Tanzania kama nchi ya pili barani afrika kwa kuwa na ng’ombe milioni 42 ambao wanaweza kuinua uchumi wa nchi kwa kuingiza pesa za kigeni zingewekewa utaratibu kibiashara, kama ilivyo nchi ya Botswana  yenye wakaazi milioni mbili, mifugo michache ya ufugaji wa kisasa na kuuza tani laki 6 za nyama nchi za ulaya, tofauti na Tanzania inayoendekeza ufugaji wa kuhamahama na idadi kubwa ya mifugo na kuwa watumwa wa mifugo hiyo. 

Na Mwanaharakati.

MAHAFALI YA CHUO KIKUU HURIA TANZANIA PINDA ASISITIZA-MSIKILIZE HAPA



Waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda, amesisitiza umuhimu wa elimu ya masafa ya chuo kikuu huria, kuwa ni muhimu kujiendeleza ukiwa mahala pa kazi.
Mh. Pinda amesema hayo wakati wa mahafali ya 29 ya chuo kikuu huria cha Tanzania, yaliyofanyika kwa mara ya tisa katika viwanja vya makao makuu ya chuo hicho Bungo Kibaha mkoani Pwani, kwa wahitimu 4,265 kutunukiwa shahada ya udhamivu, stashaada na ngazi ya cheti.

Amesema kuwa elimu ya masafa ilibezwa na kusababisha kiwango cha elimu nchini kutokupanda, akimwomba mkuu wa chuo hicho Dr Asha Rose Migiro, kudumisha mahusiano katika nchi za nje ili kupeana uzoefu jinsi ya ukuzaji wa elimu bora.

Udahiri wa wanafunzi wapya umeongezeka kutoka elfu 10 wa awali hadi laki moja  kwa muhula ambapo uongozi wa chuo hicho kwa sasa unafanya utaratibu wa kuendelea kutumia Tehama kufundishia ili kupunguza gharama za uendeshaji na kuweka majengo katika mikoa ambayo bado, na kufanya ukarabati katika baadhi ya maeneo.

Tangu chuo hicho kuanza hapa Tanzania, kimekwisha kuhitimisha wanafunzi 26,241, ambapo kimeweka vituo nchi za Rwanda, Namibia, Malawi na Kenya, na katika mahafali ya 29 mwaka huu, Bi Anne Kilango Malecela, mkuu wa mkoa Kagera John Mongela na aliyekuwa mkuu wa wilaya Kinondoni Jerry Slaa ni miongoni mwa wahitimu waliotunukiwa shaada.
 
Na Mwanaharakati.

Friday 11 December 2015

SOMA VYAMA VILIVYOFUTWA NA SERIKALI BAADA YA KUKIUKA TARATIBU

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi Bw Izack John Nantanga, amesema kuwa vyama 1268 vimefutwa, huku vingine 1406 vikipewa taarifa ya kufutwa wakati wowote.

Miongoni mwa vyama hivyo vilivyofutwa ni pamoja na vya taasisi za kidini, wazee Tanzania, umoja wa wapiga picha na vilabu vya habari (press clubs) vimepewa siku 21 pamoja na vingine kufutwa muda wowote.

Amesema makosa ni ukiukwaji wa sheria kwa kutowasilisha hesabu baada ya kukaguliwa, kujisajili serikalin badala ya NGOs, pamoja na kutolipa ada elekezi.
Na Mwanaharakati.

Thursday 10 December 2015

SAUTI YA RAIS MAGUFULI AKITANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI



Rais wa awamu ya tano nchini Tanzania Dr John Joseph Magufuli, ametangaza bara la mawaziri lenye wizara 18, kwa kusisitiza kuwa ameamua kupunguza matumizi ya serikali kwa kuteua baraza hilo dogo.


Na Mwanaharakati.

RAIS ATANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI

Jumla ya wizara in 18 zenye mawaziri 19 na naibu 18, mbili aziacha wazi zikiwa na naibu pekee huku bil2 zilizotakiwa kutumika kuwapa semina akizizuia.

Raid Magufuli amesema kuwa sasa wasifurahie kuteuliwa badala take wajiandae kufanya sherehe baada kufukuzwa wakishindwa kazi.

Magufuli: Tutakuwa na mawaziri 19, kuna baadhi ya wizara zitakuwa na mawaziri na hazitakuwa na manaibu waziri. Lengo ni kuwa na baraza dogo kupunguza gharama. Zilitengwa bilioni 2, mawaziri watakapoteuliwa waende semina elezi, baraza nitakaloliteua halitakuwa na semina elekezi na fedha tutaelekeza sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure.

Ofisi ya Rais, Tamesemi utumishi na utawala bora, Simbachawene na Kairuki, Naibu waziri Jaffo

Mazingira: Makamba, naibu Makamba
Ajira, walemavu: Jenista Mhagama, Naibu nimemtua mbunge, Pos Abdallah ambae ni mhadhiri Dodoma

Ulemavu: Mavunde

Kilimo, mifugo na uvuvi: Mwigulu Lameck Nchemba, Nashe naibu

Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano: Waziri bado sijamtafuta, naendelea kumfikiria, Naibu waziri Ngonyani.
Fedha na mipango: Waziri bado, naibu Kijachi
Nishati na madini: Waziri ni Muhongo, Naibu

Katiba na sheria: Waziri Mwakyembe

Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki: Augustino Mahiga nmemteua mbunge na waziri,  Naibu Dr Suzan

Ulinzi na kujenga taifa: Waaziri Dr. Hussein Mwinyi

Ardhi na maendeleo ya makazi: Waziri ni Wiliam Lukuvi, Naibu Angelina Mabula

Utalii: Waziri bado

Viwanda na biashara: Waziri Charles Mwijage

Sayansi na ufundi: Naibu ni Stella Manyanya

Afya na Ustawi wa jamii: Ummy Mwalimu, Naibu ni Kingwangala

Habari: Nape Nnauye



Wizara ya maji na umwagiliaji: Makame Mbarawa,  Naibu ni KamweneNa Mwanaharakati.

Tuesday 8 December 2015

KATIBU MKUU CCM ATOA KAULI KAZI ZA MAGUFULI KWA WAPINZANI



Cahama nchini Tanzania cha mapinduzi CCM, kimesema kuwa kinaunga mkono juudi za rais wa sasa Dr. John Pombe Magufuli, kwa kusisitiza kuwa anatekeleza Ilani ya chama hicho, huku kikiwataka watendaji wengine kutekeleza maagizo yake ili kufanya mabadiliko ya kweli.
Na Mwanaharakati.