Jaji mkuu mstaafu Mac Bomani, amesema kuwa mbadala pekee
katika uchaguzi wa Zanzibar ni kuondoa dosari zilizobainika, siyo kuishinikiza
tume kutangaza matokeo yaleyale.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kuonesha msimamo
wake katika mambo kadha hapa nchini, jaj Bomani amesisitiza kuwa haiwezekani
tume ya uchaguzi Zanzibar ikatangaza matokeo iliyoyafuta kwa sababu za
kubainika makosa mbalimbali, kabla ya kuondoa dosari zilizobainika na kurudia
uchaguzi, ili kuendelea kuaminika kwa wananchi.
Hatahivyo amesema kuwa mchakato wa katiba usiishie njiani
kwani katiba inahitajika, hivyo baada ya uchaguzi wa Zanzibar ni muhimu
lifuatiliwe kwani mengi yameshafanyiwa kazi kupitia waliohusika na mchakato huo
hasa tume ya Warioba, kwani fedha nyingi imetumika na katiba mpya inahitajika.
Wakati huo jaj Bomani, amesema kuwa migogoro ya wakulima na
wafugaji imekithiri nchini, jambo ambalo linasababishwa na kukosekana kwa
mbadala kama ardhi ya kutosha hasa ya kufanyia malisho, na kuondoa taratibu za
zamani zinazotumika kwa mfugaji mmoja kufuga ng’ombe elfu moja, ilhali hawezi
kuwapa huduma ya kutosha, hivyo serikali iangalie katika sekta hiyo.
Ameitaja Tanzania kama nchi ya pili barani afrika kwa kuwa
na ng’ombe milioni 42 ambao wanaweza kuinua uchumi wa nchi kwa kuingiza pesa za
kigeni zingewekewa utaratibu kibiashara, kama ilivyo nchi ya Botswana yenye wakaazi milioni mbili, mifugo michache
ya ufugaji wa kisasa na kuuza tani laki 6 za nyama nchi za ulaya, tofauti na Tanzania
inayoendekeza ufugaji wa kuhamahama na idadi kubwa ya mifugo na kuwa watumwa wa
mifugo hiyo.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment