MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday 21 May 2017

MKURUGENZI WA SHULE ZA KAIZIREGE ATAPELIWA BUKOBA



By Lameck Richard

Ikiwa vitendo vya utapeli kwa njia ya mtandao vinaendelea katika maeneo mbalimbali,hali hiyo imemgusa pia mkurugenzi wa shule za Kaizirege zilizopo katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera Eusto Kaizirege.

Akiongea kwa niaba ya mkurugenzi huyo, meneja wa shule za Kaizirege William Katiti amesema kuwa tangu Mei 17 mwaka huu namba ya mtandao wa tigo{0717  972 752}ilianza kusumbua na kulazimu  kukata mtandao kabisa katika simu yake huku watu wengine wakiendelea kupokea message kupitia namba hiyo.

Aidha amesema kuwa kuna matapeli waliswapu  namba hiyo{walisajili namba kama yake} ambapo wanatumia jina la mkurugenzi wa wa shule hizo kuwatapeli wazazi wa wanafunzi wake ikiwa ni pamoja na kuwatapeli watu wa karibu nae kwa kuwatumia message zikidai anaomba wamkope fedha ikiwa ni pamoja na mambo mengine ambayo ni tofauti na mipango yake.

Ameongeza kuwa kufuatia kitendo hicho yeye ameacha kutumia laini hiyo huku akiwaomba wazazi na watu wake wa karibu kutokubali kufanya kitu chochote watakachoelekezwa kupitia namba hiyo,na kusema kuwa tayari amechukua hatua ambapo ametoa taarifa kituo cha polisi na mamlaka husika ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa kwa wanaofanya vitendo hivyo.

Sanjali na hayo Bw. Katiti amewaondolea wasiwasi wazazi na walezi ambao wamepokea taarifa za kwamba wanafunzi wa kidato cha sita walikamatwa na majibu katika mtihani wao na kusababisha shule hiyo kufutiwa usajili,amesema kuwa taarifa hizo si za kweli na wazipuuze kwani hata afisa elimu mkoa Kagera amesikiksa katika vyombo vya habari mbalimbali akikanusha taarifa hizo na kudhibitisha kuwa mtihani umemalizika salama kwa mkoa wa Kagera.

Pia amesema kuwa wao kama shule hawawezi kukata tama kwa maneno ya baadhi ya watu ambao hawapendi wasonge mbele katika msingi wa kutoa elimu,badala yake watanaendelea na kazi kwa kuhakikisha wanafunzi wao wanazidi kupata elimu iliyo bora.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA………………………………………………………............


Na Mwanaharakati.

No comments: