MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Saturday 31 May 2014

NEWS ALERT!!!KIFO CHA MSANII MWINGINE BONGO MOVIE

Ni mwongozaji George Otieno Tyson ambaye taarifa inasema amekufa baada ya gari waliokuwa wakisafiria kupata ajali mkoani Morogoro.

Alikuwa akielekea kuandaa kipindi cha THE MBONI SHOW kwani yeye ndiye alikuwa mwongozaji wake akiwa wafanyakazi wengine.

Director George Tyson aliwahi kuwa mume wa msaniii Monalisa na walizaa pamoja mtoto mmoja.

Tunaendelea kufuatilia taratibu zinazoendelea kwani ukumbukwe ni kifo cha msanii wa tatu hivi karibuni baada ya Adam Kuambiana, na Rechal Haule.
Na Mwanaharakati.

BREEAKING NEWS!!!BASI LAPATA AJALI SINGIDA

Taarifa iliyotumwa na mwakilishi wetu kutoka Ssingida, inasema kuwa ni la kampuni ya KIMOTCO lililokuwa likitoka Dodoma kuelekea mikoa ya kanda ya ziwa.

Imesema kuwa limeacha njia na kujikita kwenye ukingo wa barabara katika la kati ya Manyoni na kijiji cha Ikungi muda mfupi uliopita.

Picha na taarifa za majeruhi zitakujia kwani inasemekana hakuna aliyepoteza maisha katika ajali hiyo ambayo imesababisha tairi ya mmbele ya basi hilo kuchomoka.

Na Mwanaharakati.


Thursday 29 May 2014

WANAFUNZI IRINGA KATIKA HALI MBAYA YA UHABA WA MADAWATI HUKU WAKO KWENYE SHAMBA LA TAIFA. WANAFUNZI IRINGA KATIKA HALI MBAYA YA UHABA WA MADAWATI HUKU WAKO KWENYE SHAMBA LA TAIFA.

Na Mwanaharakati.

Kutokana na hali hiyo kuzikabili shule mbalimbali na kushusha kiwango cha elimu, moja ya shule za msingi ijulikanayo kama LUGODA LUTALI wameamua kuanzisha mpango wa kutengeneza madawati ya udongo almaarufu Adobe, ilhali wakishindwa kufaidi shamba la miti la taifa SAOHILL mkoani humo.
Wakati huo huo kila kijiji na shule wanapewa Qubick meter za shamba kwajili ya kukata na kutengeneza dawati, lakini jamii inashindwa kutekeleza hilo.

Miongoni mwa sababu zinazosababisha wasitekeleze ni pamoja na masharti ya ukataji miti na gharama za kutenegeza dawati, hivyo waandishi wamepewa changamoto ya kulifanyia kazi na kujua ni kwanini wananchi hawatengenezi madawati.

WANACHUO SAUTI WAGOMA NA KUANDAMANA

Na Mwanaharakati.
Wanachuo wa chuo cha SAUTI tawi la mtwara leo wameandamana mpaka kwa  mkuu wa mkoa wa Mtwara kutaka ufumbuzi juu ya mikopo yao kama wanachuo kutoka kwenye bodi ya mikopo.

Madai yao kwa sasa ni kutolipwa miezi 4 ndipo wakaamua kuandamana maandamano ambayo hayakuwa rasmi hivyo jeshi la polisi mkoa wa mtwara likaingilia kati na kuzima maandamano hayo yaliyoanza mchana majira ya saa 8 mpaka saa 10.

WANAHABARI KUKUTANA DODOMA HII LEO

Na Mwanaharakati.
Ni maandalizi ya mkutano wa siku mbili mjini Dodoma.



Tuesday 27 May 2014

NEWS ALERT!!! WASICHANA WALIOTEKWA WABAINIKA WALIPO NIGERIA

Marshal Alex Badeh


Nigeria's defense chief is claiming that the country’s military has located nearly 300 schoolgirls abducted by Islamic extremists but cannot go in with force to free them.

Air Marshal Alex Badeh told demonstrators supporting the country's much criticized military on Monday that Nigerian troops can save the girls, according to The Associated Press. But he added, "we can't go and kill our girls in the name of trying to get them back."

He spoke to thousands of demonstrators who marched to Defense Ministry headquarters in Abuja, the capital. Many were brought in on buses, indicating it was an organized event.

Asked by reporters where they had found the girls, Badeh refused to elaborate.
A senior U.S. defense official who spoke to Fox News also said that the reports cannot be independently confirmed.

"We want our girls back. I can tell you we can do it. Our military can do it. But where they are held, can we go with force?" Badeh asked the crowd.
People roared back, "No!"
"If we go with force what will happen?" he asked.
"They will die," the demonstrators said.
Badeh said no one should criticize the military.

"Nobody should come and say the Nigerian military does not know what it is doing. We know what we are doing," he insisted.
Nigeria's military and government have faced national and international outrage over their failure to rescue the girls seized by Boko Haram militants from a remote northeastern school six weeks ago.

President Goodluck Jonathan was forced this month to accept international help. American planes have been searching for the girls and Britain, France, Israel and other countries have sent experts in surveillance and hostage negotiation.
Jonathan's reluctance to accept offered help for weeks is seen as unwillingness to have outsiders looking in on what is considered a very corrupt force.

Soldiers have told The Associated Press that they are not properly paid, are dumped in dangerous bush with no supplies and that the Boko Haram extremists holding the girls are better equipped than they are.

Some soldiers have said officers enriching themselves off the defense budget have no interest in halting the five-year-old uprising that has killed thousands.
Soldiers near mutiny earlier this month fired on the car of a commanding officer come to pay his respects to the bodies of 12 soldiers who their colleagues said were unnecessarily killed by the insurgents in a night-time ambush.

The military also is accused of killing thousands of detainees held illegally in their barracks, some by shooting, some by torture and many starved to death or asphyxiated in overcrowded cells.

More than 300 teenagers were abducted from their school in the town Chibok on April 15. Police say 53 escaped on their own and 276 remain captive.

A Boko Haram video has shown some of the girls reciting Koranic verses in Arabic and two of them explaining why they had converted from Christianity to Islam in captivity. Unverified reports have indicated two may have died of snake bites, that some have been forced to marry their abductors and that some may have been carried across borders into Chad and Cameroon.

Boko Haram -- the nickname means "Western education is sinful" -- believes Western influences have corrupted Nigerian society and want to install an Islamic state under strict Shariah law, though the population 170 million people is divided almost equally between Christians and Muslims.

Na Mwanaharakati.

BREAKING NEWS!!! MSANII RECHAL HAULE WA BONGO MOVIE AFARIKI DUNIA

 Msanii wa Bongo Movie, Rachel Haule 'Recho' (pichani), amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es slaaam. Habari zilizotua Global na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere, zimesema kuwa Recho alikwenda Muhimbili jana kujifungua ambapo mara baada ya kujifungua mtoto alifariki na yeye hali yake kuwa mbaya, ilibidi ahamishiwe ICU ambako hali ilizidi kuwa mbaya na baadae kufariki dunia.

 

Kifo cha Recho kimekuja ndani ya wiki moja baada ya kufariki kwa msanii mwingine wa Bongo Movi Adam Kuambiana Jumamosi iliyopita, kifo hiki kimeleta mstuko mkubwa kwenye tasnia ya ya filamu za kibongo. Habari na picha zaidi zitawajia baadae.
Na Mwanaharakati.

MSAKO MKUBWA DAR ES SALAAM

 Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanya msako wa nyumba kwa nyumba, mtaa na maeneo yaliyoathirika kwa hofu ya vijana ambao ni vibaka maarufu kama Mbwa mwitu au Panya Road.  Msako huu uliofanyika ndani ya masaa 24 hadi alfajiri ya tarehe 26/5/2014 kwa lengo la kuwaondolea hofu na uhalifu dhidi ya makundi ya vijana wadogo wasio na ajira ambao uliibuka hivi karibuni.

        Maeneo yaliyoathirika ni Kigogo, Magomeni, Tabata, maeneo yote yanayozunguka mto Msimbazi, maeneo ya Mbagala nk.  Msako huu unaendelea kufanywa na askari wa vikosi maalum ambao wamepewa kazi ya kuhakikisha kuwa vikundi hivyo haviibuki tena na vinatokomezwaa kabisa kwa  kuwakamata wale wote wanaojihusisha na vitendo vya kuvamia kwa mkundi wananchi ambao hawana hatia
Kamishna kova ambaye amezungumza na wanahabari muda mfupi uliopita
 Kati ya watuhumiwa 149 waliokamatwa mmoja amegundulika kuwa ni kiongozi aitwaye ATHUMANI SAIDI miaka 20, Mkazi wa Kigogo na amekiri anaongoza kundi la watu zaidi ya 15 ambao baadhi yao ni kati ya waliokamatwa. 

          Imegundulika pia kwamba vijana hawa wanatumia dawa za kulevya aina ya bangi na wengine hujichoma sindano na kuwafanya iwe rahisi kujihusisha na matukio ya uhalifu.  Vijana hao hupenda kushiriki katika ngoma kama Mnanda, Mchiriku, Kigodoro, Kanga moja nk. ambazo kwa kawaida huchezwa hadi usiku wa manane. 

         Wakitoka katika ngoma hizo hujikusanya pamoja na kufanya matukio ya uporaji kwa mtu wanayekutana naye, kufanya uvunjaji katika majumba na wakati mwingine wana mtindo wa kugema mafuta ya diesel au petrol katika matanki ya malori yanayosafirisha mafuta. 

         Operesheni kali inafanyika katika maficho ya wahalifu hao ikiwa ni pamoja na daraja la River side, Kigogo darajani, Manzese, maeneo ya Tandale pamoja na maeneo mengine ya maficho mkoa wa Kipolisi Temeke.

  Tunawasiliana na Maafisa utamaduni wa Wilaya zote za Mkoa wa D’Salaam kusimamisha utoaji wa vibali wa ngoma za usiku ambazo hazina tija.  Pia Jeshi la Polisi linafuatilia na kuwavizia vijana wanaopora  watu wanaotoka katika sherehe za usiku kama vile Harusi na wanaotoka katika mikesha ya Ibada na sehemu zozote zenye mikusanyiko.

      Aidha Jeshi la Polisi wanapambana na vijana wanaowavizia watu katika vituo vya mabasi pindi wanapotoka alfajiri kwenda katika shughuli zao za kila siku.
Zipo taarifa kwamba baadhi ya wazazi wasio waaminifu wamewasafirisha watoto wao wahalifu katika makundi haya kwenda mikoani ili kukwepa wasinaswe na msako huu mkali.  Hata hivyo Jeshi la Polisi lina mtandao wa kutosha kati yake na mikoa mingine na nchi jirani hivyo litawatafuta popote walipo na kuwakamata.

          Oparesheni hii ni endelevu na ya kudumu hadi kero hii ya vibaka itakavyokwisha kabisa. Baadhi ya majina waliokamatwa ni kama ifuatavyo:-
1.    DANIEL PETER @ MALUNDE, miaka 25, mkazi wa Yombo Kigunga
2.    MWISHEHE ADAM, miaka 35, mkazi wa Mtoni mashine ya maji
3.    MOHAMED SAID, miaka 32, mkazi wa Mtoni
4.    JAKAMA ALPHONCE, miaka 23, mkazi wa Mtoni Kilakala
5.    HAMADI MDUDU, miaka 25, mkazi wa Mbagala
6.    SALUM MUSA, miaka 25, mkazi wa Kiwalani
7.    ANTHONY DANIEL, miaka 20, mkazi wa Mashine ya maji
8.    FIDELIN ANTHONY, miaka 18, mkazi wa Kigogo
9.    HAMZA MAZUMA, miaka 19, mkazi wa Kigogo
10.           MGANGA ABEID, miaka 20, mkazi wa Kigogo
11.           SAID ABEID, miaka 19, mkazi wa Kigogo
12.           SALUM NYENJE, miaka 36, mkazi wa Chamazi
13.           DOMINICK PETER miaka 22, Mkazi wa Kigogo
14.           KULWA ABEID, miaka 20, mkazi wa Mabibo
15.           MUSA IBTRAHIM, Miaka 20, mkazi wa Magomeni
16.           HUSSEIN SHABAN, miaka 22, Mkazi wa Magomeni
S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
Na Mwanaharakati.

MAGAZETI LEO 27 MAY 2014

 
 
 
 
 
 
Na Mwanaharakati.

Monday 26 May 2014

NEWS ALERT!!! ASKOFU DESDERIUS RWOMA AONGOZA MAZISHI YA MONSINYORI BAMANYISA

Baba Askofu jimbo Katoliki la Bukoba Deziderius Rwoma.
Monsinyori Justinian Bamanyisa, amezikwa katika makaburi ya ya seminari ya Rubya, ambapo Askofu Rwoma amesema kuwa alikuwa na mfano wa pekee wa kuwasaidia watu wote ususani wahitaji , walemavu, na wazee ambapo amewahimiza wananchi kuiga mfano wake.

Monsinyori Bamanyisa, amefariki juzi akiwa na umri wa miaka 88, ambapo ametumikia upadri kwa miaka 59 na kushika nyadhifa mbalimbali, pamoja na kuwa Dereva wa Cardinal Laurian Rugambwa. Mungu ailaze roho yake mahala panapostahili.

Na Mwanaharakati.

NEWS ALERT!!!KANDA YA ZIWA KUKABILIANA NA UCHAFUZI VYANZO VYA MAJI


Ofisa  wa maji Bonde la Ziwa Victoria Jumanne Mpemba akizugumza na wandishi wa habari.
Ni mtambo unaoitwa Tera Tem, wenye kifaa maalum cha kuchunguza miamba iliyo na maji katika tabaka mbalimbali ardhini kwa kutumia mawimbi yanayotkana na umemeusumaku (Electromagnetic Conductivity Method)


Wito huo umetolewa na Afisa wa Maji Bonde la Ziwa Victoria Jumanne Mpemba wakati akiwasilisha mada ya usimamizi wa rasilimali za maji kwa pamoja katika warsha ya siku moja kwa waandishi wa habari jijini Mwanza.

Alisema ili utunzaji wa vyanzo vya maji na rasilimali za maji katika bonde la Ziwa Victoria, mambo muhimu yanayotakiwa kuzingatiwa ni pamoja na kuwapo kwa usimamizi wa pamoja, ushirikishwaji wa sekta ikiwa ni pamoja na usitishaji wa shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji.


Alisema ushirikiano wenye tija unahitajika na kutaja sekta za Madini, misitu, Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Viwanda na Utalii kama maeneo yanayopaswa kushirikiana katika usimamizi endelevu wa rasilimali za maji.


"Ili kulinda Bonde la Ziwa Victoria, ni lazima kuwepo na sera ya pamoja kwa nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi zinazowiana katika utunzaji  wa rasilimali za maji katika maeneo ya nchi hizi, pia utoaji wa elimu kuhusu umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji kwa wadau na wananchi ili kuwezesha jamii inayozunguka vyanzo vya maji kutambua faida na umuhimu wake" alisema.


Mpemba ameshauri kuwako kwa mpango utakaositisha shughuli zote za kibinadamu zinazofanywa karibu na vyanzo vya maji kama Mahoteli na Viwanda kuzuia uchafuzi wa mazingira na uharibifu wa vyanzo vya maji, na katika sekta ya uvuvi kuzingatia kanuni za uvuvi endelevu ili kujihakikishia ukuaji wa kiuchumi unaotokana na zao la samki ziwa Victoria.


Pia Afisa huyo amewataka wananchi na makampuni yanayotaka kutumia maji ya Ziwa Victoria au kuchimba visima kuomba vibali vya kufanya utafiri wa maji ardhini kutoka Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria kwani ndivyo inavyosema katika kunusuru ziwa hilo na vyanzo vyake kwa matumizi yasiyofaa.


“Maji ni rasilimali ya kiuchumi,ni vyema ikafahamika kuwa wananchi hawana budi kuchangia gharama kidogo ili rasilimali hii iendelee kuwepo na sheria ya rasilimali za maji ya mwaka 2009 kifungu cha 96 na 112  inamtaka kila mtumiaji maji apate kibali cha kutumia maji kwa kuomba katika ofisi ya maji,Bodi ya Bonde husika.
“Lakini  wapo wananchi wachache wenye uelewa kuhusu sheria hii wamejitokeza na kuomba vibali na kulipia ada ya matumizi ya maji ,hivyo ni vyema kila mtumiaji wa maji akaitekeleza sheria hii ili kuepuka adhabu ya kuivunja.
“Sheria  ya rasilimali za maji namba 11 ya mwaka 2009 kifungu cha 102 kifungu  kidogo cha 2 inatamka yeyote atakaye kaidi kuitekeleza adhabu yake ni faini isiyopungua shilingi laki tano  au isizidi shilingi milioni moja na kama ataendelea kutolipa atatozwa faini ya shilingi milioni moja au kwenda jela miaka si chini ya mitatu”alisema

Aliongeza kuwa ili kufikia malengo ya pamoja shughuli zote za usimamizi wa matumizi ya maji ya rasilimali hiyo zinapaswa kujiendesha zenyewe, hivyo kulipa ada ya matumizi ya maji kwa wakati ni kuchangia katika uboreshaji huduma ya maji itakayo saidia kusimamia matumizi bora ya rasilimali hii.
 Na Mwanaharakati.