Msanii wa Bongo Movie, Rachel Haule 'Recho' (pichani), amefariki dunia
usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es
slaaam. Habari zilizotua Global na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie,
Steve Nyerere, zimesema kuwa Recho alikwenda Muhimbili jana kujifungua ambapo
mara baada ya kujifungua mtoto alifariki na yeye hali yake kuwa mbaya, ilibidi
ahamishiwe ICU ambako hali ilizidi kuwa mbaya na baadae kufariki dunia.
Kifo cha Recho kimekuja ndani ya wiki moja baada ya kufariki kwa msanii
mwingine wa Bongo Movi Adam Kuambiana Jumamosi iliyopita, kifo hiki kimeleta
mstuko mkubwa kwenye tasnia ya ya filamu za kibongo. Habari na picha zaidi
zitawajia baadae.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment