MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday 27 November 2012

KIFO CHA SHARO MILLIONEAR KIKO HIVI

Kuhusu kifo cha msanii na mwigizaji Sharo Milionea, nKamanda wa Polisi Tanga akisema usiku majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo la Maguzonizonga wilayani Muheza hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza”

Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei.

Kwenye gari alikua pekeyake.

Monday 26 November 2012

BREAKING NEWS;- HABARI ZISIZO RASMI ZINASEMA SHARO MILIONEAR AMEFARIKI KWA AJALI

Kuna habari zinasema msanii Mchekeshaji huyo Sharo Millionea kafariki dunia kwa ajali ya gari huko Muheza, mkoani Tanga.  (Habari hazijathibitishwa)
Fuatilia zaidi ili upate habari rasmi zitakazothibitishwa na vyombo husika.

Sunday 25 November 2012

SIKU MOJA BAADA YA MBUNGE WA BUKOBA MJINI KUSEMA KUWA SOKO LA BUKOBA HALITAVUNJWA MPAKA WATAALAMU WAPIME HALI YA ARDHI YA SOKO, LIMEFIKA GARI LILILOSHEHENI MASHINE ZA KUCHIMBA ARDHI ILI KUPIMA KINA CHA MAJI NA KUFUKUZWA NA WAFANYABIASHARA WA SOKO HILO

Wakizungumza na waandishi wa kituo hiki, wafanyabiashara hao wamesema kuwa hawakubaliani na utaratibu unaofanyika kwasasa kwani unawanyioma ushirikiano, huku wakihamini kuwa vifaa hivyo vimeletwa kwajili ya kufanya tathmini ya kina cha maji katika soko hilo, ili liweze kubomolewa.
Hata hivyo dereva na mafundi waliokuwa na gari hiyo aina ya FUSO yenye nambari za usajiri T 975 AUJ kutoka kampuni ya GEOPINUS ENGINEERING LTD  kutoka Dar es salaam, wamesema kuwa kampuni yao imetambulika na wameletwa na tajiri yao kwa shughuli ambayo hawakupenda kuisema.
Hali hiyo imejitokeza siku moja baada ya mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Balozi HAMIS KAGASHEKI, kusema kuwa ili soko livunjwe ni lazima kufanyika upembuzi yakinifu ikiwa ni pamoja na kujua ni kiasi gani cha maji kiko chini ya ardhi ya soko, jambo ambalo mpaka sasa halijafanyika.

Sunday 18 November 2012

MTANGAZAJI WA BBC FRED MTOI AMEFARIKI DUNIA



BBC inasikitika kutangaza kifo cha mtangazaji mwenzetu Fred Mtoi ambaye alifariki Ijumaa usiku mjini London.
Fred alianza kazi ya utangazaji katika Radio Tanzania kabla ya kuja Ulaya kwa mafunzo.
Amekuwa akifanya kazi huku akiendelea na masomo ya shahada ya pili ya masters kwenye digital media katika chuo kikuu kimoja cha London.
Alishiriki katika vipindi muhimu na vilivyopata sifa hasa vya sanaa, utamaduni na jamii kutokana na kuwafahamu wakaazi wengi wa London hasa wenye asili ya Afrika Mashariki.
Alishiriki piya katika matangazo ya kawaida ya habari ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC.
Wenzake katika Idhaa ya Kiswahili ya BBC wanamkumbuka Fred kuwa mtu mwema, mpole, mchangamfu na anayepatana na wote, na ambaye alikuwa mtangazaji tulivu na akishikilia kazi lazima ahakikishe kuwa ameimaliza vema iwezekanavyo.
Matayarisho yanafanywa kusafirisha mwili wake hadi Tanzania.

Thursday 15 November 2012

DRC inataka UN kuadhibu Rwanda

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imetoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuichukulia hatua Rwanda, kwa madai ya kusaidia waasi nchini Congo badala ya kumfuatilia mtu mmoja kama vile kanali Sultani Makenga.
Waziri wa habari wa serikali ya Congo amesema hayo siku moja baada ya Umoja wa Mataifa na Marekani kutangaza vikwazo dhidi ya kiongozi wa waasi wa M23, Jenerali Makenga, vikiwemo vya usafiri na kukamata mali yake.

UZINDUZI WA MRADI WA WAENDESHA PIKIPIKI WILAYANI MISENYI MKOANI KAGERA.

 
 
Kamanda wa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani mkoani Kagera  Wiliam Nkonda ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa mradi wa waendesha pikipiki wilayani Misenyi mkoani Kagera.

Kamanda NKONDA amesema kuwa,madereva hao wakizingati hayo wananweza kupunguza ajali kwa kiasi kikubwa.

Aidha ameongeza kwa kuwataka madereva hao kuachana na  tabia ya kuhusisha pikipiki zao  katika matukio ya uharifu kwani baadhi ya  waarifu hutumia pikipiki hizo katika shughulki zao za uporaji.

Kamanda NKONDA amewaomba watumiaji wa usafiri wa pikipiki kuzingatia suala la uvaaji wa element kwa usalama wao kwani nao wamekuwa kikwazo kwa kupuuzia suala hilo.

Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoani hapa bwana WISTON KABANTEGA amewaombwa waendesha pikpiki kuzingatia mafunzo wanayokuwa wanapewa pamoja na sheria za usalama barabarni kwani takwimu zinaonesha ajali za pikipiki zinaongezeka mwaka hadi mwaka nchini.

Pia bwana KABANTEGA amewaombwa bodaboda hao kuacha tabia ya kutumia njia za mikato mikato kwa kupata vyeti vya kugushi ili wapate leseni kitu ambcho si sahihi na ni kosa la jinai hivyo hawana budi kuvitumia vyuo vya udereva ili kupata vyeti sahihi na hatimaye kupata leseni.

Mradi huo unaundwa na vikundi sita vyenye waendesha pikipiki 170 na madereva zaidi ya ishirini na nne kati yao wametukiwa vyeti vya mafunzo na leseni.