Wakizungumza na waandishi wa kituo hiki, wafanyabiashara hao
wamesema kuwa hawakubaliani na utaratibu unaofanyika kwasasa kwani unawanyioma
ushirikiano, huku wakihamini kuwa vifaa hivyo vimeletwa kwajili ya kufanya
tathmini ya kina cha maji katika soko hilo, ili liweze kubomolewa.
Hata hivyo dereva na mafundi waliokuwa na gari hiyo aina ya
FUSO yenye nambari za usajiri T 975 AUJ kutoka kampuni ya GEOPINUS ENGINEERING
LTD kutoka Dar es salaam, wamesema kuwa
kampuni yao imetambulika na wameletwa na tajiri yao kwa shughuli ambayo
hawakupenda kuisema.
Hali hiyo imejitokeza siku moja baada ya mbunge wa jimbo la
Bukoba mjini Balozi HAMIS KAGASHEKI, kusema kuwa ili soko livunjwe ni lazima
kufanyika upembuzi yakinifu ikiwa ni pamoja na kujua ni kiasi gani cha maji
kiko chini ya ardhi ya soko, jambo ambalo mpaka sasa halijafanyika.
No comments:
Post a Comment