MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday 21 January 2013

BREAKING NEEEEWS!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Taarifa zinasema kuwa ukuta katika stand kuu ya mabasi yaendayo mikoani Ubungo Terminal umeanguka ghafra na kusababisha uharibu mkubwa wa mali yakiwemo magari ya watu tofauti.

Hizo ni taarifa za awali, hivyo yawezekana mahafa yakaongezeka lakini hatahivyo tutakuletea km tutapata habari zaidi ngoja tufuatilie, ila hakuna taarifa ya waliopoteza maisha katika ajali hiyo.

CCM JANA WALIHUTUBIA WANAMWANZA

Katika hotuba ya viongozi hao wanachama kadhaa wa CCM waliopata nafasi mbalimbali pamoja na wananchama wapya waliojiunga kutoka vyama vingine vya siasa walihapishwa.

Ni baada ya kuwasili juzi kwa viongozi wa kitaifa, akiwepo makamu wa ccm Tiafa na katibu mwenezi wa chama hicho Nape Nnauye.

MWANA HARAKATI

Wednesday 16 January 2013

SOKO LA BUKOBA KATIKA SIKU YA PILI BILA KUVUNJWA KAMA ILIVYOSEMWA AWALI

Jana tarehe 15 januari, Wafanyabiashara wa soko kuu la Bukoba waliazimia kukesha karibu na soko hilo, ili wahakikishe kama kutafanyika uvunjaji wa soko hilo, kama taarifa zilivyotolewa awali na baadhi ya viongozi wa manispaa.
 Nilipozungumza na katibu mkuu wa wafanyabiashara hao Bwana DAVID DAMIAN, akasema kuwa wafanyabiashara wanasubiri kauli ya mahakama kwa kila jambo litakalojitokeza, kwani waliambiwa kuwa soko alipaswi kuvunjwa hadi kesi iliyopo mahakamani itakapomalizika.

Amesema kuwa kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa tare 18 mwezi wa 3 mwaka huu.
 Baadhi ya wafanyabiashara waliozungumza nami, walionesha kuwa na wasi wasi  kuwa soko hilo lingevunjwa usiku wa kuamkia leo wakati  wa usiku, muda ambao hawatakuwapo sokoni hapo, hivyo inawezekana wakajikuta wakipoteza mali zao, lakini hatahivyo mpaka sasa hakuna kilichofanyika.

Wamesema kuwa wanashindwa kuongeza bidhaa, kwasababu wanahofia kupata hasara ikitokea soko hilo likavunjwa.




Katika mikutano mbalimbali ya hadhara, wananchi walitangaziwa kuwa soko hilo litavunjwa tarehe ya leo 15 januari 2013, suala ambalo mbunge wa jimbo la Bukoba mjini na naibu waziri wa maliasili na utalii BALOZI HAMIS KAGASHEKI, aliwahakikishia wananchi hao kuwa ili soko hilo livunjwe lazima taratibu za kisheria zifuatwe.

WATU WATATU WAUAWA KAGERA KWA KUTUHUMIWA KUWA NI MAJAMBAZI

Akiongea na waandishi wa habari mkoani Kagera, kamanda wa polisi mkoani humo kamanda Philipo Kalangi amesema kuwa majambazi walio huawa ni mioingoni mwa majambazi sugu ambao wamekuwa wakijiusisha na vitendo vya uhalifu ndani na nje ya mkoa kagera.
 Jeshi la polisi mkoa kagera limefanikiwa kuwaua majambazi watatu huku wengine wawili wakifanikiwa kukimbia hatua iliyofikia kufuatia opreisheni inayo endelea kufanywa na jeshi la polisi mkoani humu ikilenga kuwatia mbaroni watu wanao jiusisha na vitendo vya ujambazi mkoani humo.
Katika opreisheni hiyo kumekamatwa injini tanoza boti zenye thamani ya shilingi milioni ishirini bunduki tatu na risasi 25.

Pia jeshi hilo limekamata misokoto ya bangi na lita 120 za pombe aina ya gongo katika operesheni inayoendelea mkoani humo.


MWANA HARAKATI

Wednesday 9 January 2013

REAKING NEWS!!!!!!!!!!! AJALI YA BASI LA BUNDA KANDA YA ZIWA

Taarifa za awali zinasema kuwa watu ambao hawajafahamika idadi yao wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa, katika ajali ya Basi ya kampuni ya BUNDA, ambalo inasemekana limepinduka wilayani MAGU mkoani Mwanza,

Kamanada wa polisi mkoani humo ERNEST MANGU, ambaye hata hivyo wakati anaongea na kandayaziwaleo, alikuwa bado anafuatailia taarifa, amesema kuwa basi hilo ambalo hakulitaja namba limepata jali wilayani Magu lilipokuwa likitokea Musoma kuelekea Mutukula mkoani Kagera.

Taarifa zaidi tutaendelea kukuletea.

MWANAMKE AUAWA KWA KUGONGWA NA GARI KWENYE KIWANDA CHA SUKARI

Mwanamke huyo JANE EMMANUEL, aliyekuwa na umri wa miaka 26, amefariki dunia jana baada ya gari la kubebea miwa kiwandani hapo kurudi nyuma ghafla na kumkanyaga, ambapo amepasuka kichwa na tumbo ambalo hatahivyo alikuwa na ujauzito wa mtoto wa kike baada ya tumbo kupasuka na mtoto kutoka nje.
 Mwanamke huyo amezikwa jana hiyo hiyo kijijini kwao Maruku Bukoba, kwasababu ya mwili wake kuharibika vibaya na kichanga kimezikwa katika kaburi la peke yake.
 Mwanadada huyo ambaye awali alikuwa akiishi mjini Bukoba, alikuwa anafanya kazi katika kiwanda cha sukari mkoani Kagera katika wilaya ya Misenyi ambapo kwa taarifa zilizopo, alikuwa akifanya mahesabu ya mzigo unaopakiwa kwenye magari hayo, ambapo hadi kifo kinamkuta alikuwa akichkuwa rekodi ya kiasi kilichopakiwa.
 Picha chini ni kichanga alichokuwa nacho tumboni JANE EMMANUEL, A.K.A FIRST kwa jina tulilokuwa tukimuita.
Mungu ailaze mahala panapostahili JAH RASTER FARIE.

Tuesday 8 January 2013

MSANII OMAR OMAR AMEFARIKI DUNIA


Kwa mwaka huu pekee amabo una wiki ya pili sasa, wasanii wawili wameshaaga dunia.

Omari Omar  ambaye ni msaanii wa miondoko ya Mnanda/Mchiriku,  amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Habari zinasema kuwa, Omar Omar aliyetamba na nyimbo mbalimbali kama 'Kupata ni Majahariwa' alifariki nyumbani kwao Temeke, saa chache baada ya kurejeshwa toka hospitali ya temeke alipokuwa amelazwa kwa siku kadhaa.

Taarifa hizo zinasema kuwa mara baada ya kurejea nyumbani, msanii huyo alizidiwa na hatimaye kufariki na kwamba msiba wake upo nyumbani kwao Temeke Mikoroshini kwa ajili ya mipango ya mazishi.
Msiba wa msanii huo umekuja siku chache baada ya tasnia ya sanaa na burudani kumpoteza Juma Kilowoko 'Sajuki' msanii nyota wa filamu aliyefariki pia kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya muda mrefu.

Amefanya kazi hiyo sambamba na wasanii wengine na waliopenda kumuiga kama Dogo Mfaume, Ferouz, Easy Man na wengine.

MAGAZETI LEO

BARAZA la Vijana la Chadema (Bavicha), limesema limemvua uanachama Makamu Mwenyekiti wa baraza hilo, Juliana Shonza baada ya kubainika alikuwa akifanya vikao vya siri kukisaliti chama hicho akishirikiana na viongozi wa CCM.
Mwenyekiti wa Bavicha, John Heche alisema Shonza alikuwa akiwashawishi wenzake kuitisha mikutano na waaandishi wa habari kumkashifu Katibu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa.
“Aende CCM hapa tumemg’oa kwa sababu alikuwa kirusi hatari kwa chama, alikuwa Chadema huku akifanya kazi na CCM, tuna ushahidi wa picha, mikanda ya video na ujumbe wa simu za mikononi,” alisema Heche.
Licha ya kumfuta uanachama Shonza, baraza hilo pia limewavua uanachama Habib Machange aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Kibaha Mjini na Mtela Mwampamba aliyegombea ubunge Jimbo la Mbozi Mashariki.

                         



POLISI jijini Arusha imekamata shehena ya nyara za serikali zenye thamani ya mamilioni ya shilingi wakati huo zikiwa zimefungwa kwenye makasha.
Inasemekana yalikuwamo mafuvu ya samba, mamba, tembo na wanyama wengine wa porini pamoja na ngozi za chui mamba tembo na meno mawili ya tembo.
 NI KWA HISANI YA GAZETI LA HABARI LEO 




TUME ya Mabadiliko ya Katiba, jana ilianza kukusanya maoni ya vyama vya siasa katika mchakato wa Katiba Mpya, huku baadhi ya vyama hivyo vikitoa mapendekezo mbalimbali kuhusu suala la urais.
Vyama vilivyozungumzia urais katika mkutano huo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam ni CCM, CUF na Chadema.
Taarifa za vyama hivyo zilipatikana baada ya wawakilishi wao kuwasilisha maoni kwenye tume hiyo katika mkutano wa ndani ambao waandishi wa habari hawakuruhusiwa kuingia.

Wakati CCM ikitaka Katiba ijayo iruhusu mgombea binafsi, Chadema imependekeza Mtanzania yeyote mwenye umri wa kuanzia miaka 18 aruhusiwe kupiga kura na kugombea nafasi yeyote ya uongozi nchini. CUF imependekeza Muungano wa Mkataba.

Mwanasheria wa Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alisema chama hicho cha upinzani, kimependekeza Katiba Mpya imtambue mtu mwenye umri wa kuanzia miaka 18 kuwa ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa kushika nafasi yoyote ya uongozi nchini.

                           








TAARIFA ZINASEMA BUNDUKI ZIMESALIMISHWA
POLISI nchini wametangaza kupokea bunduki 439 na risasi 37 kutoka kwa watu waliozisalimisha kutokana na wito uliotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi mwezi mmoja uliopita kuwataka wenye silaha kinyume cha sheria wazisalimishe.
Miongoni mwa silaha zilizosalimishwa na watu hao ni pamoja na shortgun (29), gobore (352), SMG (11), Riffle (20), bastora (22), Airgun (1), Rocket launcher (2) na SAR (2).

Msemaji wa polisi , Advera Senso alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana kwamba kupatikana kwa silaha hizo ni ushirikiano mzuri kati ya polisi na wananchi.
Senso alisema polisi wamejipanga kwa kufanya operesheni maalumu itakayoendeshwa nchi nzima kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola pamoja na raia wema ili kuwabaini na kuwakamata wale wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria.

Alisema operesheni hiyo itafanyika kutokana na kumalizika kwa muda maalumu alioutoa Waziri Nchimbi kwa watu wenye silaha kuzisalimisha bila masharti yoyote.

Hata hivyo taarifa ya Senso haikutaja ni lini operesheni ya kusaka bunduki itaanza nchini.
Alitoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za mtu ama kikundi cha watu wanaosadikiwa kujihusisha na umiliki wa silaha isivyo halali au matukio ya uhalifu wa aina yoyote ile ili kuhakikisha uhalifu wa kutumia silaha unapungua.”

Senso alibainisha kwamba mtu yeyote atakayetoa taarifa za mafanikio zitakazowezesha kukamatwa kwa watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria watazawadiwa Sh100,000 kulingana na mafanikio ya taarifa aliyoitoa.

Monday 7 January 2013

BREAKING NEWS!!!!!!!!!!! POLISI WAUAWA TENA KAGERA

MWANA HARAKATITaarifa za awali zinasema kuwa makamanda wawili wa jeshi la polisi mkoani Kagera wameuawa na wananchi katika shughuli zao za utendaji kazi.

Taarifa za awali kutoka kwa kamanada wa polisi mkoani Kagera Kamishina msaidizi PHILIP KALANGI, vifo hivyo vimetokea baada ya polisi watatu wa kituo cha Benako wilayani Ngara, kujifanya wanunuzi wa meno ya tembo katika kijiji cha Lugu ili wawabaini wananchi wanaojihusisha na biashara hiyo, lakini baada ya kufanikiwa kuwapata wauzaji na kuwakamata, inasemekana zilipigwa simu kwa wananchi wengine na kukusanyika na wakaanza kupigana na polisi hao kwa kuwakata mapanga, huku wakiwawekea kizuizi barabarani na hatimaye wawili kuawa na mmoja kukimbia.

Tukio hilo linatokea siku chache baada ya polisi wengine wawili kuawa huko huko Ngara, jambo ambalo linaonesha kuwa hali si nzuri kwa kipindi kifupi mkoani humo.

Siku chache katika mkutano wa mkuu wa mkoa wa Kagera kanali mstaafu FABIAN MASSAWE, mkuu huyo wa mkoa aliulizwa na waandishi habari kuhusu mkoa kuwa katika hali ya vurugu ambapo alisema kuwa kwasasa mkoa huko shwari, lakini tukio la leo linaonesha kuwa majibu ya mkuu huyo si sahihi.

Saturday 5 January 2013

MKUTANO WA VIONGOZI SUDAN WAFANYIKA

Ni viongozi wa kutoka Sudan na Sudan kusini ambao wamekutana Ijumaa(04.Jan.2013)

Lengo ni kuondoa hali ya wasi wasi ambayo imetanda tangu kusini kujitenga mwaka 2011 na kuanza usafirishaji mafuta ili kukwamua uchumi wa nchi hizo unaodidimia.

Hakuna taarifa zaidi zilizojitokeza wakati rais wa Sudan Omar al-Bashir na Salva Kiir wa Sudan ya kusini walipokutana pamoja na waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn, ambaye anajaribu kufanya upatanishi kati ya nchi hizo jirani ambazo zilikaribia kupigana vita mwezi wa Aprili.

Viongozi wote hao wawili watakutana kwa mara ya kwanza peke yao katika mkutano utakaofanyika hii leo Jumamosi (05.01.2013), limeeleza shirika la habari la Sudan SUNA.

Taarifa hii ni kwa hisani DW.

MWANAHABARI AZIKWA MWANZA

Ni mwandishi wa habari wa gazeti la CHANGAMOTO, HELLEN KABAMBO, ambaye alifariki kwa kuugua kwa muda mfupi na hatimaye wikii hii akapoteza maisha.




Amezikwa jana ijumaa kwa ushirikiano wa wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habri mkoani Mwanza, Mungu aiweke roho yake mahali anapostahili, JAH RASTAFARIE.

Friday 4 January 2013

SAJUKI AMEZIKWA RASMI KISUTU

Baadhi ya wasanii wameubeba Mwili wa Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam mchana huu tayari kwa Mazishi yaliyoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.
 Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye Kaburi la Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika mchana huu kwenye Makaburi ya Kisutu,Jijini Dar es Salaam.
 Chini ni baadhi ya waandishi wakichukuwa picha kwenye mazishi ya marehemu SAJUKI hii leo.
MWANA HARAKATI

BIASHARA YA MAGENDO KUSABABISHA UPUNGUFU WA PATO LA MKOA WA KAGERA

Mkuu wa mkoa wa Kagera kanali mstaafu FABIAN INYASI MASSAWE, amesema kuwa hadi sasa changamoto kubwa ya kushuka kwa mapato ya mkoa ni pamoja na biashara ya magendo hasa ya kahawa, sababu nyingine ni kuchelewa kupitishwa kwa sheria ya mapato kwa halmashauri. Hata hivyo kanali Massawe amesema kuwa tatizo lingine kupungua kwa ushru wa kahawa pamoja na uhaba wa wataalamu wa kilimo na maofisa ughani.
 Kanali Massawe amesema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari, alipokuwa akitoa taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa serikali ya awamu ya nne.
 Katika mkutano huo mkuu huyo wa mkoa, amewataka vijana kuacha kutoa lawama kwa serikali, badala yake wajibidiishe kufanya kazi kwa kutumia nguvu zao wenyewe na serikali itaendelea kuwaunga mkono katika hilo.

MWANA HARAKATI

WAUMINI WAOMBA MSAADA WA MBUNGE KUKAMILISHA UJENZI WA KANISA HUKU SHULE YA MSINGI IKIEZULIWA KWA UPEPO

Ni Kanisa la Kigango cha KAHYOLO kata ya Mikoni Bukoba vijijini, ambapo kunafanyika ujenzi huo, ambao una miaka kadhaa na bado unaendelea, hivyo mbunge wa jimbo hilo JASSON RWEIKIZA alipotembelea eneo hilo kujionea shughuli zao za ujenzi, mwenyekiti wa kamati ya ujenzi alimtembeza akimsihi kuwasaidia.
 Mbunge huyo alichangia bando ya mabati yenye thamani ya shilingi laki 3.5.
 Chini ni shule ya msingi iliyoko kwenye Kata ya KAIBANJA Bukoba vijijini ambayo iliezuliwa na upepo mwezi Oktober, hata hivyo ukarabati unaendelea ambapo pia mbunge huyo alichangia kiasi cha shilingi laki tatu na nusu, ili kuchangia nguvu za wananchi.

Bukoba vijijini kumekuwa na tabia ya wazazi na walezi kuchapwa viboko na mugambo wakiongozwa na watendaji pamoja na viongozi wengine wa vijiji, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limekuwa likiwaweka wananchi katika wakati mgumu, hivyo wananchi wakiona mchango huo wanajihisi kuwa wameona mlango wa mbinguni.

Thursday 3 January 2013

MNAPOKUTANA KAMA FAMILIA INAPENDEZA

Ni katika sikukuu za Xmass na mwaka mpya baada ya kukutana familia ya Mzee Trazias Ngaiza.
 Kwasasa kila mtu ameshatawanyikia kwenye sehemu yake ya kazi na majukumu ya yanaendlea baada ya kumtembelea mama mzazi BERTHA NGAIZA nayeonekana amejifunga kitambaa kichwni.
MWANA HARAKATI

MAZIKO YA SAJUKI NI KESHO IJUMAA 04/01/2013

Taarifa zinasema kuwa msanii huyo JUMA KILOWOKO atazikwa kwenye makaburi ya KISUTU jijini Dar es salaam, tofauti na taarifa za awali kuwa atasafirishwa kwenda kijijini kwao huko SONGEA.
Ni baada ya kuugua kwa muda mrefu huku akipelekwa India kwa matibabu bila mafanikio, wasanii pamoja na wadau wa tasnia hiyo tunasikitika sana kwasababu ni kama amefungua milango ya 2013, kutokana na historia ya tasnia hii mwaka jana kuondoka wasanii kwa kiasi kikubwa hila hatuna jinsi.

Mungu aiweke roho yake popote anapoona anastahili, JAH RASTAFARIE.