Jana tarehe 15 januari, Wafanyabiashara wa soko kuu la
Bukoba waliazimia kukesha karibu na soko hilo, ili wahakikishe kama kutafanyika
uvunjaji wa soko hilo, kama taarifa zilivyotolewa awali na baadhi ya viongozi
wa manispaa.
Nilipozungumza na katibu mkuu wa wafanyabiashara hao
Bwana DAVID DAMIAN, akasema kuwa wafanyabiashara wanasubiri kauli ya mahakama
kwa kila jambo litakalojitokeza, kwani waliambiwa kuwa soko alipaswi kuvunjwa
hadi kesi iliyopo mahakamani itakapomalizika.
Amesema kuwa kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa tare 18
mwezi wa 3 mwaka huu.
Baadhi ya wafanyabiashara waliozungumza nami, walionesha
kuwa na wasi wasi kuwa soko hilo lingevunjwa
usiku wa kuamkia leo wakati wa usiku,
muda ambao hawatakuwapo sokoni hapo, hivyo inawezekana wakajikuta wakipoteza
mali zao, lakini hatahivyo mpaka sasa hakuna kilichofanyika.
Wamesema kuwa wanashindwa kuongeza bidhaa, kwasababu
wanahofia kupata hasara ikitokea soko hilo
likavunjwa.
Katika mikutano mbalimbali ya hadhara, wananchi
walitangaziwa kuwa soko hilo litavunjwa tarehe ya leo 15 januari 2013, suala
ambalo mbunge wa jimbo la Bukoba mjini na naibu waziri wa maliasili na utalii
BALOZI HAMIS KAGASHEKI, aliwahakikishia wananchi hao kuwa ili soko hilo livunjwe lazima
taratibu za kisheria zifuatwe.
No comments:
Post a Comment