MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Wednesday 31 October 2012

RAIS WA ZANZIBAR AMEFANYA UTEUZI MWINGINE KATIKA MWEZI WA KUMI

NA MAELEZO ZANZIBAR 31/10/2012 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amemteua Amina Juma Zidikheir kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utumishi wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Zanzibar. 
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar Dkt Abdulhamid Yahya Mzee imesema kuwa uteuzi huo ameufanya kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 8(1) (a) cha sheria ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Zanzibar namba 11 ya mwaka 2003. 
Amina Juma Zidikheri aliwahi kuwa Mhasibu mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kabala ya kustaafu kwake. Uteuzi huo umeanza tarehe 27 Oktoba,2012 

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR 31/10/2012

MECHI KATI YA TOTO AFRIKA NA KAGERA IMEAHIRISHWA SABABU YA MVUA NA WATU WATATU WAMENUSURIKA KIFO BAADA YA JIWE KUBWA KUPOROMOKA KUTOKA MLIMANI MKOANI MWANZA.

Watu watatu akiwemo mtoto mdogo wamekimbizwa hospitali ya mkoa Sekou Toure mara baada ya kuumizwa vibaya kwa kuangukiwa na ukuta wa nyumba yao kupitia jiwe lililoporomoka kutoka mlimani jijini Mwanza.

Waliokumbwa na ajali hiyo ni Bw. Msalam Husein(30) ambaye ni  dereva  na mkewe Bi. Nadia Grecian(25) ambaye ni mama wa nyumbani  pamoja na kichanga wao Asfati Mslam (aliyechini ya umri wa mwaka).


Tukio hilo limetokea leo hii majira ya saa 6:00 mchana katika nyumba wanayoishi kilima cha Sabato mtaa wa Ngara eneo la Mlimani B Kirumba jijini Mwanza ambapo pamoja na kwamba ni majira ya mchana watu hao  mke na mume walikuwa wamejipumzisha kitandani, (yawezekana kutokana na hali ya hewa kwa mvua inayoendelea kunyesha leo tangu asubuhi hadi muda huu tunakupa taarifa) ndipo wakakutana na ajali hiyo.


Kwa mujibu wa  Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai wilaya ya Ilemela  (OC-CID) Afande Magesa amesema kuwa hali ya Msalam Husein ni mbaya kwani amekimbizwa hospitali akiwa ajitambui huku mkewe akiwa akilia kwa maumivu makali kufuatia ajali hiyo.


Taarifa ya tukio hilo ilichelewa kufika polisi kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha lakini hata hivyo polisi walifika eneo la tukio na kutoa msaada kwa kuwakimbiza hospitalini wajeruhiwa hao.
HABARI KWA HISANI GSENGO

Tuesday 30 October 2012

BOMU LA KILIPUKA KARAGWE NA KUUA

Watoto  sita wamefariki dunia na mwingine  kujeruhiwa  vibaya katika kijiji  cha RUGARAMA kata ya IHANDA wilaya ya karagwe  mkoani kagera bada ya kuripukiwa na kitu kinachosadikiwa kuwa  ni bomu.

Kamanda  wa polisi wa mkoa wa kagera   PHILIPO KALANGI  amethibitisha  kutokea  tukio hilo lililotokea asubuhi ya jumanne,ambapo  kati ya watoto waliopoteza maisha wapo waliokuwa wanafunzi wa shule ya msingi
 
Mwenyekiti  wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye ni mkuu wa wilaya ya karagwe darry rwegasila ambaye yupo katika eneo la tukio amesema kuwa wataalamu wa jeshi la wananchi wa Tanzania wamethibitisha kuwa hao waliopoteza maisha walikuwa wakichezea bomu ambalo limewalipukia.

Rwegasira amewataadharisha wananchi kuwa makini wanapookota vyuma chakavu na kwamba wanapohisi kitu chochote wasichokielewa ni muhimu wakatoa taarifa katika vyombo vya dora.
Uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo bado unaendele.

MKUTANO WA TISA WA BUNGE KUANZA VIKAO LEO MJINI DODOMA, WAKATI HUO CHAGUZI MBALIMBALI ZIKIKAMILIKA, AMBAPO NAPE NNAUYE ALONGA JUU YA UCHAGUZI.

Tarehe 28/10/2012 kumefanyika uchaguzi mdogo katika kata 29 kwenye mikoa mbalimbali nchini. Kata hizi zilikuwa wazi kwa sababu mbalimbali, hivyo kwa mujibu wa sheria ililazimika kufanya uchaguzi mdogo kujaza nafasi wazi.

Ukiacha matukio kadhaa ya vurugu, maeneo mengi uchaguzi umeenda kwa utulivu. Chama Cha Mapinduzi kinawapongeza wote waliofanya uchaguzi kwa amani na utulivu, huo ndio utamaduni wa watanzania, kushindana bila kupigana.

Muhutasari wa matokeo ya jumla unaonyesha kuwa TLP wameshinda kata moja(1), CUF wameshinda kata moja(1), CHADEMA wameshinda kata 5 na CCM imeshinda kata ishirini na mbili(22).

Kwa matokeo haya ambayo kwakweli yanatafisiri pana sana hasa ikizingatiwa kuwa mgawanyo wa kata ulikuwa nchi nzima basi matokeo haya yanatoa ujumbe wa jinsi CCM inavyokubalika nchini kwasasa.


Na pia ni uthibitisho wa kile kilichoitwa M4C(movement for change) kwa Chadema kuwa ni kiini macho kisichokuwa na matunda chanya bali ni M4D ( movement for dealth). Na hii inatokana na aina ya siasa za hovyo zinazoambatana na operesheni hii. Bila shaka sauti ya Watanzania kwa aina hii ya siasa imesikika bila kumumunya maneno.

Aidha kwa upande mwingine siasa za uongo,uzushi na ulaghai zilizotumiwa na vyama vya upinzani hasa Dr. Slaa kwenye kampeni hizo imekidhalilisha chama hicho na kudhalilisha utu uzima wa Katibu Mkuu huyo wa Chadema.

Mfano mzuri ni pale ambapo Dr. Slaa bila ya soni alipoamua kumzushia Rais na Mwenyekiti wa CCM kuwa kasafiri mpaka China eti kwenda kumuokoa mwanae ambaye kwa madai ya Dk. Slaa alikamatwa na madawa ya kulevya nchini humo.

Bila aibu Dr. Slaa alizusha uongo huo Tabora kwa wapiga kura huku akijua kuwa ni uongo, lakini hata hivyo uongo huo hauna sehemu kwenye kampeni hizo za udiwani. Wananchi walitegemea kusikia namna ya kutatua kero zao badala yake wakashuhudia mtu mzima akizusha ujinga wa ajabu.

Uongo huu na mwingine mwingi unathibitisha kuwa Dr. Slaa anazeeka vibaya kwani kila anavyoongeza siku hamu na tamaa yake ya kusema uongo ili kujiongezea umaarufu na kujenga chuki kati ya watanzania inaongezeka sana. Hakika TAPELI HUYU WA KISIASA, LICHA YA KUZEEKA VIBAYA SASA ANACHANGANYIKIWA.

Naamini mzigo aliotwishwa na wenzake unamlemea sana, hivyo namshauri awaachie vijana wajaribu kukiokoa chama hicho kinachoporomoka kwa kasi, vinginevyo wana Chadema waanze kuandaa matanga kwa chama chao.

Ukitazama mgawanyo wa ushindi huu utagundua kuwa, pamoja na Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Slaa kwenda na kupiga kambi kanda ya ziwa ameambulia kata sifuri(0). Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwa kutumia gari ya serikali alijikita kusini nako katoka kapa.

Nguvu iliyotumika kutoka kwa vyama vya upinzani hasa Chadema hailingani na ushindi walioupata. Wakati CCM ikiwa busy na chaguzi za ndani ya Chama wao wamezungusha viongozi wa kitaifa nchi nzima na matokeo ndio hayo.

Tunawashukuru sana Watanzania kokote nchini walioendelea kutuamini na kutupa dhamana ya kuendelea kuwaongoza na kutekeleza ilani yetu. Tunawaahidi utumishi uliotukuka.

UMEPERUZI JUMANNE LEO?






MWANA HARAKATI

Saturday 27 October 2012

BALOZI KAGASHEKI AMETEMBELA NA KUTOA MSAADA WA CHAKULA NA MABATI VYENYE THAMANI YA SH MILIONI 5.3 KWA WALIOTHIRIKA NA MVUA ILYOAMBATANA NA UPEPO KATIKA MANISPAA YA BUKOBA

 Kata zilizoathirika na mvua hiyo, ni pamoja na HAMUGEMBE, RWAMISHENYE, NYANGA, BUHEMBE, NSHAMBYA, KASHAI NA KAHORORO, ambapo Mbunge huyo alitembelea na kukutana na waathirika hao huku akiwapa pole pamoja na kuwapatia chakula na sehemu nyingine mchango wa fedha.

 Chini ni picha ya kanisa katoliki kigango cha Kyakailabwa ambalo limeezuliwa na upepo ambapo katika kanisa hilo mbunge amechangia bando moja ya mabati.


Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayotoa huduma za mawasiliano yenye gharama nafuu zaidi na mtandao wenye wigo mpana leo imezindua mwendelezo wa huduma za Airtel kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuwawezesha wateja wake nchi nzima kulipia Kodi kupitia huduma ya Airtel Money. Hii imekuja wakati huduma za pesa kutumia simu zimekuwa zikibadilisha huduma za kibiashara na kuongeza ufanisi.

Kwa kupitia huduma ya Airtel money na ushirika na Mamlaka ya Mapato Tanzania Airtel wateja wa makampuni hayo wataweza kulipia kodi ya mapato na majengo kupitia Airtel Money.

Akiongea wakati wa uzinduzi uliofanyika makao makuu ya kampuni ya Airtel, Mkurugenzi wa Biashara za Mashirika bi Irene Madeje Mlola alisema” Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kuleta ufanisi na mapinduzi katika sekta ya mawasiliano nchini. Leo tuna furaha kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuwezesha wateja wake kulipa kodi kwa kupitia huduma ya Airtel Money.  Airtel money ni huduma iliyotengezwa kukithi mahitaji ya wateja wetu na hii ni hatua nyingine muhimu kwa Airtel kutumia miundo mbinu tuliyonayo na TRA katika kuhakikisha wanaboresha huduma zao. Sasa walipaji wa kodi wadogo na wakubwa wanalipia kodi zao kwa urahisi wakiwa katika biashara zao na nyumbani”

“Mpaka sasa takribani nusu ya wateja wa Airtel wamejiunga na kutumia huduma ya Airtel money, huduma iliyo rahisi, iliyojitosheleza, salama na nyenye kutoa nafasi kufanya miamala mbalimbali ikiwemo malipo ya bidhaa mbalimbali. Kwa kupitia huduma ya Airtel money inayotoa huduma nyingi zaidi ya kutuma pesa tumeona maisha ya watanzania wengi yakibadilika kila siku na biashara zao kuwa na ufanisi zaidi aliongeza Madeje.”

Kwa upande wake Kamishina Msaidizi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania bw Rished Bade alisema” Tunayofuraha kuzindua huduma yenye kutumia mfumo wa teknolojia ya malipo ya uhakika na salama kwa wateja wetu nchi nzima.

Uzinduzi wa leo ni udihirisho wa juhudi za Mamlaka katika kuongeza uboreshaji katika huduma za malipo ya kodi na ukusanyaji wa mapato.Tunategemea kwa kupitia huduma ya Airtel Money kutawezesha ulipaji wa kodi kwa wakati na kuwahamasisha watanzania wengi zaidi kulipia kodi zao za mapato na majengo. TUnategemea kuona ongezeko kubwa la wafanya biashara wadogo na wakati ambao leo hii wanalipia malipo ya kodi kwa kupitia maofisi na vituo mbalimbali vya kodi nchi nzima. 

Akiongelea kuhusu njia ya kulipia kodi hizo kwa njia ya simu Meneja Uendeshaji Airtel Money Asupya Naligingwa alieleza”Kulipia kodi ya majengo au mapato mteja wa Airtel atatakiwa kupiga namba  *150*60#*  kisha

   1. Atachagua Lugha
   2. Atachagu malipo ya bili 
   3. Lipa Bili
   4. Atachagu “JIna la fumbo” *MAJENGO” 
   5. Ingiza kiasi cha fedha unachotaka kulipia
   6. Ingiza neno la siri
   7. Ingiza namba ya akaunti ya Mamlaka ya Mapato (TRA) kisha bonyeza OK
   na utapokea meseji(SMS)itakayothibitisha malipo yako ”

Huduma ya Airtel Money service inayopatikana kwa kupiga  *150*60# inawawezesha
wateja kulipia huduma mbalimbali zikiwepo kama vile za kulipia bili za maji na umeme,bidhaa na huduma mbalimbali kama vile  bima,kununua muda wa maongezi, miamala ya huduma za kibenkiikiwemo kuweka na kupokea kutoa na vile vile kulipia huduma nyingine nyingi.

Airtel Money ni huduma inayopatikana masaa 24, siku 7 za wiki kutoka katika simu na ni salama ya uhakika na rahisi kutumia. Kinachohitajika ni kitambulisho na usajili wa simu yako ili kuweza kupata huduma hii katika maduka na mawakala wote waliopo nchi nzima. 

Friday 26 October 2012

IDD EL HAJI- WAUMIN MKOANI KAGERA WASWALI KATIKA MSIKITI WA JAMIAH BUKOBA WAKIONGOZWA NA SHEKH WA WILAYA ARUN KICHWABUTA.

Pamoja na mambo mengine, Shekh Kichwabuta amewataka wazazi na walezi kuwaleoa watoto, katika mazingira ya kidini ili kuendana na maadili ya Mungu ili kunusuru taifa na dunia nzima, ili kupunguza majanga na matendo ya kibinadamu. BOFYA KATI KATI YA VIDEO KUSIKILIZA*



MWANA HARAKATI

WAUAJI WA MAREHEMU KAMANDA BARLOW MBARONI.

-->Akitaja majina hayo mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania IGP Said Mwema, MKURUGENZI wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba,  amesema kuwa simu iliyoporwa ya mwanamama ambaye alikuwa akisindikizwa nyumbani na marehemu ndiyo imesaidia kukamilisha upelelezi huo hatimaye wahusika kukamatwa.

                              -->
Majina ya wahusika hao kuwa ni Muganyizi Michael Peter (36) ambaye inatajwa kuwa ndiye aliyemuua Barlow, Chacha Waitare Mwita (50), Magige Mwita Marwa (48),  Buganzi Edward Kusuta pamoja na Bhoke Marwa Mwita (42) ambao wote wamekatwa katika jiji la Dar es Saalm.

Alisema Kikosi kazi cha upelelezi kilichokuwa chini yake  Manumba kilijigawa kwenye makundi matatu moja ni lile la Ukamataji, Mahojiano na lingine la interejensia huku wakitumia njia ya sanyansi kwa kufuatia mitandao ya simu.

Kukamatwa kwa watuhumiwa hao wa dar na wale wa Mwanza kunafanya jumla yao kuwa 10 na bado jeshi linasaka wengine.  Lakini hakuna sababu iliyotokana na mauaji hayo ambayo imeelezwa mpaka sasa na jeshi hilo
-->
Liberatus Barlow aliuawa Oktoba 13 mwaka huu, saa 8 usiku kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana katika eneo la Minazi mitatu huko Kitangiri wakati alipopita kumsindikiza Mwalimu Dorothy Moses nyumbani kwake kutoka katika kikao cha harusi kilichofanyika Mtaa wa Rufiji. moja  
MWANA HARAKATI