Watoto sita
wamefariki dunia na mwingine
kujeruhiwa vibaya katika
kijiji cha RUGARAMA kata ya IHANDA
wilaya ya karagwe mkoani kagera bada ya
kuripukiwa na kitu kinachosadikiwa kuwa
ni bomu.
Kamanda wa
polisi wa mkoa wa kagera PHILIPO
KALANGI amethibitisha kutokea
tukio hilo lililotokea asubuhi ya jumanne,ambapo kati ya watoto waliopoteza maisha wapo
waliokuwa wanafunzi wa shule ya msingi
Mwenyekiti wa
kamati ya ulinzi na usalama ambaye ni mkuu wa wilaya ya karagwe darry rwegasila
ambaye yupo katika eneo la tukio amesema kuwa wataalamu wa jeshi la wananchi wa
Tanzania
wamethibitisha kuwa hao waliopoteza maisha walikuwa wakichezea bomu ambalo
limewalipukia.
Rwegasira amewataadharisha wananchi kuwa
makini wanapookota vyuma chakavu na kwamba wanapohisi kitu chochote
wasichokielewa ni muhimu wakatoa taarifa katika vyombo vya dora.
Uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo bado unaendele.
No comments:
Post a Comment