MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday 31 March 2014

HIFER INTERNATIONAL NA MRADI WA KUENDELEZA SEKTA YA MAZIWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo ambae pia ni Naibu waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mh Kaika Telele akifungua Pazia kuashiria Mradi huo wa Kuendeleza sekta ya maziwa umezinduliwa rasmi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl Nyerere uliopo jijini Dar Es Salaam.

Naibu waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ambae pia alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mh Kaika Telele akiongea na wageni waalikwa na wadau wa sekta ya Maziwa Afrika Mashariki uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwl Nyerere Mwishoni mwa Wiki.

Mkurugenzi Mkuu wa Heifer International Tanzania, Dk Henry Njakoi akiongea na wageni waalikwa na wadau wa sekta ya maziwa nchini na wa kimataifa waliofika katika uzinduzi wa Mradi wa Uendelezaji Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki uliodhaminiwa na Mfuko wa Bill na Melinda, Mradi huo mkumbwa ulizinduliwa ijumaa iliyopita katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl Nyerere uliopo Jijini Dar Es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa East Africa Dairy Development (EADD), Mh Rakesh Kapoor akichangia mada kwenye uzinduzi wa Mradi wa Kuendeleza sekta ya Maziwa kwa Nchi za Afrika Mashariki mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl Nyerere, jijini Dar Es Salaam. Mradi huo mkubwa kutoka Heifer International Tanzania umedhaminiwa na Mfuko wa Bill na Melinda Foundation.
 Na Mwanaharakati.

KAMATI ZA BUNGE ZIMEANZA KUJADILI VIPENGELE VYA RASIMU

Akiahilisha bunge hilo maalumu ili wajumbe waamie kweye kamati, mwenye wake SAMUEL SITTA, amesema kuwa watanzania wasubiri kupata katiba mpya hivyo wajumbe wasifanye mzaha katika suala hilo muhimu. Bunge limealishwa hadi ijumaa watakaporejea kupata taarifa za kilichopitishwa kwenye kamati hizo.


Kutoka kushoto ni Kingunge Ngombale mwilu,, waziri mkuu Pinda, James Mbatia mwenyekiti wa NCCR, na mwenyekiti wa CHADEMA na UKAWA Freeman Mbowe.

Na Mwanaharakati.

TAADHARI PICHA INAOGOFYA!!! NI KUONESHA WATU 12 WALIOKUFA KWENYE AJALI MOSHI IJUMAA USIKU

Ilitokea eneo la EDARU wakati wakitoka kuudhuria mazishi ya mtoto aliyesombwa na maji ya mafuriko
Na Mwanaharakati.