MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday 31 July 2014

UNAIDS, ASLM and Partners Launch Initiative to Improve HIV Diagnostics






MELBOURNE, Australia, July 30, 2014/ -- The Joint United Nations Programme on HIV/AIDS (UNAIDS) and the African Society for Laboratory Medicine (ASLM) (http://www.aslm.org) have joined with global partners to launch the Diagnostics Access Initiative which calls for improving laboratory capacity to ensure that all people living with HIV can be linked to effective, high-quality HIV treatment services.

Partners in the initiative include UNAIDS, the World Health Organization (WHO), the Clinton Health Access Initiative (CHAI), UNICEF, the US President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR) and ASLM.

“Around 19 million of the 35 million people living with HIV don’t know they have the virus. If they don’t find out, they will die,” said Michel SidibĂ©, UNAIDS Executive Director. “This is why we have to make it simpler for people to test for HIV to be able to start lifesaving treatment when they need it.”

The Diagnostics Access Initiative specifically focuses on ensuring that at least 90% of all people living with HIV know their HIV status. It also aims to ensure that all people accessing HIV treatment have ready access to tests that monitor the levels of the virus in their bodies.

For treatment to be optimally effective, it is essential that all people accessing HIV treatment monitor their viral load frequently. Currently very few high-burden countries routinely offer viral load testing to people receiving HIV treatment. New viral load testing technologies which are made available when people first come in for care, offer promise for expanding access to viral load testing. However they will need to be affordable, appropriately deployed and used effectively.

“To achieve control of the HIV/AIDS epidemic, it’s essential that all people have access to high-quality HIV laboratory services, both for accurate HIV diagnosis and treatment monitoring. Building a country’s capacity for virologic testing is critical for early identification of virologic failure, drug resistance and overall improved impact of the country’s HIV care and treatment programs,” said Ambassador Deborah Birx, U.S. Global AIDS Coordinator. “The Diagnostic Access Initiative represents an important step in ensuring the close collaboration among all donors and stakeholders to expand access and enable strategic scale-up of HIV laboratory services.”

To ensure early diagnosis of HIV, laboratory procedures need to be simplified and multiple testing tools and strategies made available. These also need to be integrated into community-centred health campaigns that focus on multiple diseases.

“It is essential that people know whether they have HIV infection, and that people who take treatment know whether their medicines are controlling the virus,” said Dr Hiroki Nakatani, Assistant Director-General, WHO. “As diagnostic technology changes rapidly, and our Member States need guidance on how to use it, WHO will play a key role in this initiative.”

HIV treatment is effective in reducing HIV-related illness and AIDS-related deaths. It also helps to prevent new HIV infections, by sharply suppressing viral load and decreasing the risk of HIV transmission.

“The Diagnostic Access Initiative focuses urgent attention on the importance of developing new, affordable viral load and infant diagnosis technologies and effectively using the laboratory capacity we currently have,” said Dr. Tsehaynesh Messele, Chief Executive Officer of ASLM. “Effectively using existing and emerging viral load and infant diagnosis technologies will demand substantially stronger laboratory capacity as well as strategic planning to ensure that all technologies are optimally used.”

Partners in the initiative will advocate for greater funding for laboratory services and for the development of new diagnostic tools. They will also strengthen efforts to ensure that diagnostic services are of the highest quality and forge well-coordinated partnerships to close diagnostic access gaps.

Distributed by APO (African Press Organization) on behalf of the African Society for Laboratory Medicine (ASLM).
Na Mwanaharakati.

NEWS ALERT!!! WATUMISHI WATANO WA HALMASHAURI WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Ni watano wa Halimashauri ya wilaya ya Geita katika idara  ya misitu wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Geita baada ya kuwa na kutuhuma 30 likiwemo la kusababishia hasara kwa mwajiri wao kiasi cha shilingi milioni 22, 9866,400,


Akisoma mashitaka hayo mbele ya hakimu wa mahakama ya wilaya Desidery Kamgisha ,mwendesha mashitaka wa serikali Enosi Erasto alisema kuwa mnamo mwezi wa sita mwaka 2009 na mwezi wa 12 mwaka 2011 huko katika msitu wa akiba wa Geita,  kwa muda tofauti washitakiwa hao wakijua ni kosa la jinai na kwa makusudi   walitenda makosa hayo na kusabasha hasara kubwa kwa mwajiri wao.

Mwendesha mashitaka huyo ameongeza kuwa baada ya kutenda makosa hayo hawakuweza kutoa taarifa yoyote ya ukweli kwa mwajiri wao.

Aidha amewata watuhumiwa hao kuwa ni  Emanueli Mabala,Kasika Gamba,Elizakayo Yobu shuma, Alexanda Makali Masawe, Paulo Maganya, wote wakiwa ni watumishi  wa wilaya ya Geita.

Mara baada ya kusomewa mashitaka hayo kwa mara ya kwanza kwa hakimu Kamgisha  washitakiwa hawakujibu chochote kutokana na ushaidi kutomilika na wamerudishwa rumande baada ya kukosa vigezo vya dhamana na kesi yao itasikilizwa tena taree 07 mwezi wa nanae.

Na Mwanaharakati.

MASIKINI NDOA YA MSANII MAARUFU LUCY KOMBA! MANENO YA KUPIMA UKIMWI YAANZA KUJITOKEZA

 
 Taarifa zinasema akiwa kwenye vikao vya maandalizi ya harusi na Mzungu, staa wa filamu Bongo, Lucy Francis Komba (pichani na mchumba wake), amejikuta katika wakati mgumu baada ya habari kudai kwamba, mchumba wake huyo amemwambia ili ndoa ifungwe lazima aoneshe cheti cha kipimo cha Ukimwi kwanza.
Chanzo chetu, kilisema kwa sasa Lucy anahaha kutafuta cheti feki cha kipimo hicho kwa kwenda hospitali mbalimbali ili anunue kwa gharama yoyote lakini imeshindikana.

“Ukweli Lucy anahaha kutafuta cheti cha Ukimwi, mchumba anasubiri akione vinginevyo hawatafunga ndoa,” kilisema chanzo.
 Ilidaiwa kuwa, mpaka sasa Lucy ameshafika kwenye hospitali tatu kubwa mbili, TMJ na Marie Stopes ili kufanya maarifa lakini imeshindikana.

Baada ya kupata habari hizo paparazi wetu alimtafuta Lucy ambapo alikuwa na haya ya kusema:

“Si kweli! Hao wanaosema hivyo ni wanafiki, sijui wanataka nini maana kila siku wanazusha mambo ya ajabu. Kwanza mimi huwa sitibiwagi kwenye hospitali hizo ulizozisema, natibiwa Regency.

“Kuhusu  kupima Ukimwi, mimi na mchumba wangu tulishapima hukohuko kwao Ulaya (Denmark) ndiyo maana tukaanza taratibu za ndoa.

“Namshangaa sana huyo aliyesema hayo hata kama ni mtu wangu wa karibu, mimi huwa simwelezi mtu mambo yangu binafsi kwa sababu duniani hakuna rafiki wa kweli, rafiki anakuchekea machoni lakini wote ni wabaya,” alisema Lucy.

taarifa za hospitali zinasema, hakuna utaratibu wa kumtaja jina mgonjwa kama alikwenda kutibiwa.

Na Mwanaharakati.

Tuesday 29 July 2014

EID MUBARAK

KANDAYAZIWA BLOG, INAKUTAKIA SIKUKUU NJEMA YA EID, AMBAPO WAISLAMU KOTE DUNIANI USHEREHEKEA BAADA YA MFUNGO WA MWEZI MTUKUFU RAMADHANI.
Na Mwanaharakati.

MAGAZETI YA LEO 29 JULY 2014

 
 
 
 
 
 
 
 
 
Na Mwanaharakati.

RAIS ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI


Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mheshimiwa Dkt. Parseko V. Ole Kone kuomboleza kifo cha aliyepata kuwa Naibu Waziri, Mbunge na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Mheshimiwa Alhaji Mahami Rajab Kundya.
Mzee Kundya aliaga dunia jana, Jumapili, Julai 27, 2014 mjini Zanzibar.
Katika salamu zake, Rais Kikwete amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kuwa taifa limempoteza Mzee Kundya katika kipindi ambacho ushauri wake ulikuwa unahitajika sana na kuwa Watanzania wataendelea kumkumbuka kwa mchango wake katika nafasi zote alizozishikilia za Serikali, za Chama cha Mapinduzi na za kidini.
“Naungana nawe na wana-Singida wote katika kuomboleza kifo cha Mzee Kundya.Tumepoteza kiongozi ambaye mchango wake utaendelea kukumbukwa na sisi sote. Kupitia kwako, natuma pia salamu zangu za rambirambi kwa familia ya marehemu. Niko nao katika kuomboleza msiba huu mkubwa na naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke peponi roho ya Marehemu Mzee Kundya,” amesema Rais Kikwete.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
28 Julai,2014

Na Mwanaharakati.

NEWS ALERT!!! MBUNGE CHAMI AJIBU TUHUMA ZA MAUAJI


 Mimi Dr Cyril August Chami, Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM) napenda kueleza masikitiko yangu kwa taarifa za uzushi na za kutunga kuwa eti mke wangu asiye na jina amemuua mfanyakazi wetu Mwislamu kwa sababu "marehemu" alikataa kwenda kanisani.


Mimi sina mfanyakazi wa jina hilo la Mariamu. Wala sina mfanyakazi mwenye umri wa miaka 16. Hatuna tatizo lolote la mfanyakazi yeyote kupigwa, achilia mbali kuuawa. Lakini taarifa hizo ambazo ni za uongo mtupu zimewashtua wengi kwa sababu zimejengwa katika misingi ya chuki za kidini. Mwandishi alilenga kuifanya jamii iamini kwamba mke wangu ambaye ni Mkristo anawalazimisha wafanyakazi wetu wasio Wakristu waikane dini yao na kuwa Wakristo. Alilenga kuibua chuki dhidi ya Waislamu na familia yangu. 

Kwa hakika, mikakati hii ya kuichafua familia yangu inasababishwa na harakati za ubunge Moshi Vijijini 2015. Wapinzani wangu wanajua wazi kuwa hawana hoja ya msingi ya kuwafanya wapiga kura wasinirudishe kwenye nafasi ya ubunge. Kwenye jukwaa na hata kwenye medani ya maendeleo wanakwama. Kwa mfano, kabla ya barabara za lami kuanza kujengwa walisema mimi sina ushawishi wa kuifanya Serikali kuzijenga. Sasa zimejengwa na zinaendelea kujengwa wanajenga hoja kuwa sihusiki wala Serikali ya CCM haihusiki, bali ni Benki ya Dunia inajenga!!! Wananchi wanawauliza kwani kabla ya Dr Chami kuwa mbunge Benki ya Dunia haikuwepo? Wanakosa hoja! Hivyo hivyo kwa mashule, maji, vyuo vya ufundi nk.

Kwa hiyo kwa upeo wao wanaona silaha pekee waliyo nayo ni kuzua kashfa dhidi yangu. Miezi michache iliyopita walizua nimeuza shamba la KNCU kwa shilingi bilioni 4 wakati mimi sina wadhifa wowote KNCU. Eti nimeuza nyumba mbili za Coffee Curing Moshi wakati mimi sina wadhifa wowote Coffee Curing. Walipoona tuhuma hizo za kutunga hazijakubalika masikioni mwa wapiga kura wa Moshi Vijijini,  sasa wamezua hili la mke wangu kuua ili Waislamu wa Moshi Vijijini wanione mtu nisiyefaa.

Sasa mimi napenda kuwauliza maswali haya:
Huyo mke wangu muuaji anaitwa nani? Inaingia akilini kweli kwamba mke huyo muuaji hafahamiki jina kwa hao "majirani" wetu wa kufikirika? Binti Mariamu kauawa mji upi? Kwa nini majirani hao wenye uchungu hawajatoa taarifa kwa RPC wa mkoa au kanda husika? Maiti kahifadhiwa hospitali ipi? Au "mke" wangu amekaa naye ndani baada ya kumuua na majirani wamekaa kimya tu?

Kwa desturi za dini ya Kiislamu binti huyo angeshazikwa sasa maana kwa mujibu wa habari hiyo ya kizushi, "aliuawa" usiku wa kuamkia jana. Je, kazikwa makaburi yapi na yako mji gani? Nani kahudhuria hayo mazishi? Kwa nini vyombo vya habari visituonyeshe hayo mazishi? Kwa nini RPC mhusika asimkamate huyo mke wa mbunge fedhuli namna hiyo na muuaji asiyevumilika?

Kwa nini polisi hawajaniita mimi Dr Chami kunihoji kuhusu huyo "mke" wangu? Si wanajua niko jimboni Moshi Vijijini na RPC Boaz wa Kilimanjaro anafahamu niko jimboni, tena jana nimeutembelea msikiti mmoja kwa minajili ya kuutafutia umeme na maji? Sote tunafahamu kuwa kuna mkuu mmoja wa mkoa alimuua mtu kwa kumpiga risasi na alikamatwa akapelekwa mahabusu. Huyo mke wa Dr Chami ni maarufu kuliko Mkuu wa Mkoa?  Kwa nini asikamatwe tuione sura yake magazetini?

Majibu ya maswali haya HAYAPO kwa sababu kila kitu kimetungwa kwa kujenga chuki tu. Hakuna Mariamu, hakuna kipigo, hakuna kifo. Ila kuna UBUNGE WA MOSHI VIJIJINI. Ndio unaopiganiwa, hamna kingine.  Napenda kuwaasa wanasiasa wenzangu kuwa Watanzania wa leo si wa jana. Si jambo rahisi kuwaghilibu kwa staili hii. Waende kwa wananchi wachape kazi. Wasipofanya hayo wakadhani uongo wa mitandao utawapa ubunge watashangazwa mwaka kesho 2015.

Mimi naendelea kuwaahidi wapiga kura wangu utumishi wa dhati. Nawapa pole ndugu zangu wa Kiislamu kwa usumbufu walioupata. Waislamu wa Moshi Vijijini wananifahamu kama kiongozi nisiyewabagua kwa sababu ya dini yao. Wanafahamu kuwa nawapenda na nafahamu kuwa wananipenda sana. Ndiyo maana wengi wamejiuliza iweje tena mke wangu amwage damu ya Mwislamu kwa sababu iliyotajwa. Naendelea kuwaahidi Waislamu wote upendo na ushirikiano siku zangu zote za kuwatumikia.
Wasalaam
Dr Chami.

Na Mwanaharakati.