Ni watano wa Halimashauri ya wilaya ya Geita katika
idara ya misitu wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Geita baada ya kuwa na kutuhuma 30 likiwemo la kusababishia hasara kwa mwajiri
wao kiasi cha shilingi milioni 22, 9866,400,
Akisoma mashitaka hayo mbele ya hakimu wa mahakama ya wilaya
Desidery Kamgisha ,mwendesha mashitaka wa serikali Enosi Erasto alisema kuwa
mnamo mwezi wa sita mwaka 2009 na mwezi wa 12 mwaka 2011 huko katika msitu wa
akiba wa Geita, kwa muda tofauti washitakiwa hao wakijua ni
kosa la jinai na kwa makusudi walitenda makosa hayo na kusabasha
hasara kubwa kwa mwajiri wao.
Mwendesha mashitaka huyo ameongeza kuwa baada ya kutenda makosa hayo hawakuweza kutoa taarifa
yoyote ya ukweli kwa mwajiri wao.
Aidha amewata watuhumiwa hao kuwa ni Emanueli Mabala,Kasika
Gamba,Elizakayo Yobu shuma, Alexanda Makali Masawe, Paulo Maganya, wote wakiwa
ni watumishi wa wilaya ya Geita.
Mara baada ya kusomewa mashitaka hayo kwa mara ya kwanza kwa
hakimu Kamgisha washitakiwa hawakujibu chochote kutokana na ushaidi
kutomilika na wamerudishwa rumande baada ya kukosa vigezo vya dhamana na
kesi yao itasikilizwa tena taree 07 mwezi wa nanae.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment