MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Saturday 31 March 2012

 
 Katika tuzo hizo aliyeibuka mshindi wa jumla ni Mhariri wa gazeti la Mwananchi, NEVILLE MEENA.
Tuzo hizo uandaliwa na EJAT na kushirikisha waandishi habari wa vyombo mbalimbali nchini na imeanza kutolewa miaka mitatu iliyopita.
Mkoani Kagera mwandishi aliyepokea tuzo hiyo ni Audax Mtiganzi ambapo wandishi waliofanikiwa kuingia kwenye kinyag'anyiro ni Joasi Kaijage wa Gazeti la CITIZEN, Lilian Lugakingira kutoka Mwananchi, Audax Mtiganzi wa Mtanzania pamoja na Angela Sebabstian kutoka Gazeti la Uhuru.

Sunday 25 March 2012

                                KOMBE LA UEFA KUTIMBA TANZANIA RASMI;


KESHO (JUMATATU) ASUBUHI SAA 2.00, MHE WAZIRI MKUU ATAKABIDHIWA KOMBE LA UEFA KWA NIABA YA MHE. RAIS JAKAYA KIKWETE AMBALO LINAZUNGUZUSHWA KTK NCHI KADHAA DUNIANI. BARANI AFRIKA ZIMECHAGULIWA NCHI ZA TANZANIA NA KENYA TU.

Saturday 24 March 2012

 Ni baada ya wanafunzi wa ualimu mwaka wa kwanza na wa pili walipo chuoni hapo kufanyishwa kazi ngumu za kugonga kokoto karai 3 au zaidi kila jioni, pamoja na kujipikia wakti wanalipa kiasi cha shilingi milioni moja na 30 elfu.   PICHA HII CHINI NI JIWE LINALOGONGWA NA WANAFUNZI ILI KUPATA KOKOTO.
 Chini ni baadhi ya majengo ya chuo hicho ambayo hayajakamilika na ujenzi wake unaendelea lakini kazi za kubeba vifusi baada ya kushushwa na gari inafanywa na wanafunzi hao ambao wanalalamika.
 Mkuu wa chuo picha ya chini MICHAEL RWEKITI, alipozungumza nami amekili uwepo wa hali hiyo ambayo hata hivyo baadhi nimeishuhudia mwenyewe na amesema hakujua kama ni makosa pengine alijua ni shughuli ya kawaida hivyo atarekebisha.
 Mkuu wa wilaya ya BUKOBA Bwana SAMWEL KAMOTE, baada ya mimi kumfanyia mahijiano ameagiza uchunguzi ufanyike chuoni hapo ili kunusuru wanafunzi hao zaidi ya 160 ambao hata hivyo wanashinda njaa wanapokuwa BTP-Block Teaching Placties, wakati wamelipia mwaka wa kwanza elfu 75 na wa pili laki moja.
 Chini ni mkaguzi mkuu wa Shule manispaa ya Bukoba ameomba nimpe muda kwani hata hivyo amepewa maelekezo ya kukagua vyuo vilivyo chini ya VETA.
Ni Mwalimu MEDAD BISHAGAZI Afisa mkaguzi mkuu wa shule Manispaa ya Bukoba.

Sunday 18 March 2012


KUTEULIWA KUWA MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA

Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Meja Jenerali Samwel Albert Ndomba  kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa kuanzia tarehe 14 March 2012.

Meja Jenerali Samwel Albert Ndomba alizaliwa tarehe 22 Apr 1954 wilaya ya Mbinga, mkoa wa Ruvuma. Meja Jenerali Ndomba aliandikishwa Jeshi mwaka 1976 na kutunukiwa kamisheni 1977.

Katika Utumishi wake amewahi kushika madarakayafuatayo, Afisa Mnadhimu Makao Makuu ya Jeshi, Mkuu wa Wilaya Ngara, Mkuu wa Mkoa Arusha na Mkuu wa Utumishi wa Jeshi.

Meja Jenerali Ndomba anashika nafasi iliyoachwa wazi na Meja Jenerali Samweli Kitundu ambae amestaafu kwa mujibu wa sheria.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 92023, Simu: 0764-742161
Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk

Thursday 15 March 2012


MKOA WA KAGERA KUANDAA MKUTANO WA KISWAHILI NA USHAHIRI KITAIFA;

Mkoa wa Kagera umeteuliwa kuwa mwandaaji wa mkutano mkuu wa Usanifu wa Kiswahili na ushahiri Tanzania utakao-anza mwishoni mwa mwezi huu.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya mkuu wa mkoa kagera, imesema kuwa mkutano huo unatarajiwa kuudhuriwa na wajumbe zaidi ya 80 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.

Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali FABIAN INYASI MASSAWE, ametumia fursa hiyo kuwaalika  wananchi, wadau, taasisi na makampuni mbalimbali kuhudhuria harambee itakayofanyika kesho asubuhi katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa.

Hata hivyo, kanali MASSAWE amesema wakti wa mkutano huo litafanyika kongamano litakalojadili changamoto litakalojadili changamoto zinazoikali lugha ya Kiswahili hapa nchini.

Mkuu wa mkoa amesema kuwa Kongamano hilo litaongozwa na mabingwa wa lugha ya Kiswahili kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam.

Wednesday 14 March 2012





Chama tawala cha zamani nchini Zambia cha Movement for Multiparty Democracy –MMD kimefutiwa usajili wake baada ya kushindwa kulipa ada.

Msajili mkuu wa vyama vya siasa nchini ZAMBIA Bwana Clement Andeleki, amesema kuwa vyama vya siasa vinatakiwa kulipia ada ya mwaka, lakini MMD haijalipia tangu mwaka 1993 na mpaka sasa inadaiwa zaidi ya kwacha milioni 390, sawa na dola zaidi ya milioni 74.

Akizungumza mbele ya waandhishi habari mjini Lusaka, bwana Andeleki mesema anafuta usajili wa chama hicho kwa kufuata sheria ya vyama siasa ya nchi hiyo.

Amemwambia Spika wa bunge la nchi hiyo Bwana Patrick Matibini kuwa uamuzi huo umebatilisha viti 53 vya wabunge wa chama hicho kuanzia leo, kwa kumtaka kutekeleza sheria hiyo kutowaruhusu kukanyaga bungeni tangu kutolewa kwa uamuzi huo.
Chama kitarudishiwa viti vyake vya bunge baada ya kupewa taarifa rasmi kupitia kwa Spika wa bunge.

Msajili huyo amesema kuwa uamuzi huo umefikiwa na ofisi yake baada ya kupokea malalamiko mbalimbali kuhusu kuonekana kuna ubaguzi kwa vyama vingine kulipa huku MMD ikiendelea kudaiwa kwa zaidi ya miaka 20.

MMD ilipoteza kiti cha urais katika uchaguzi wa mwaka jana baada ya mgombe wa upinzani kupitia  Patriotic Front Bwana MICHAEL SATTA kuchukuwa madaraka kutoka kwa rais wa zamani wan chi hiyo RUPIA BANDA.

Tangu rais SATTA kuchukuwa madaraka ya nchi hiyo amegundua tuhuma mbalimbali za rushwa kwa viongozi MMD.

Tuesday 13 March 2012


                                 NAFASI ZA KAZI;

EDI  LTD, YATANGAZA NAFASI ZA  KAZI  KWA WENYE  SIFA;
Mwombaji awe na elimu ya kidato cha sita au zaidi, uwezo wa kusoma na kuandika  kwa ufasaha lugha ya kiingereza na Kiswahili.

Nafasi maalum zimetengwa kwa mwenye taaluma ya uuguzi au taaluma ya maabara.

Maombi yatumwe kupitia applications@edi-africa.com,  au maelezo zaidi tembelea mbao za matangazo kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa na halmashauri za wilaya na manispaa mkoani kagera, au tembelea www.zoomtanzania.com au www.edi-africa.com.

Mwisho wa kutuma maombi ni 16 march 2012.

Monday 12 March 2012

Baada ya hotuba ya rais kwa wazee iliyozungumzia mgomo wa madaktari pekee, mwakilishi wa wazee wa Dar es salaam IDD SIMBA amepewa nafasi lakini kubwa zaidi amesema kuwa kazi ya usuluhishi wa migogoro iko mikononi mwa wazee hivyo ni budi kutafakari sababu na kushauri kuhusu utatuzi wa masuala ya migomo.
Ni katika mkutano wake na wazee wa Dar es salaam, katika ukumbi wa Diamond Jubilee,
Rais amesema amesikitika kuwaona wanaharakati wakishinikiza Madaktari kuendelea kugoma badala ya kuwahamasisha kurejea ili kunusuru maisha ya watu.

Pia amefafanua Sekta zisizotakiwa kugoma ikiwemo Idara ya maji, Tanesco na Kitengo cha wauguzi, kwa kusema kuwa hiyo ni kwa mujibu wa sheria za Tanzania.

Saturday 10 March 2012

Hapa juu hili ni jengo la chama cha ushirika ambalo liko jirani na shule ya msingi Katoke "B" ambayo iliezuliwa na upepo vyumba viwili vya madarasa ziliponyesha mvua tarehe 22 Feb 2012.Chini wanafunzi 90 wa darasa la kwanza wakisoma katika kijengo hicho kidogo na taarifa zinzsema kuna hewa nzito kwani hakina madirisha na kuna giza. 
Chini ni sehemu ya jengo la shule lililobomoka ambalo hata hivyo limechakaa baada ya kukaa muda mrefu bila ukarabati tangu ilipoanzishwa mwaka 1935.
 Pamoja na madarasa mawili yaliyosalia, bado ni taabu kwao kuyatumia kwani shule ina wanafunzi 480 ambapo wa awali ni 50 na 430.
Huyu chini ni mtendaji wa Kata ya Katoke FAUSTNE RWEYEMAMU, kwa upande wake amesema tatizo hilo linafanyiwa ufumbuzi baada ya kuhamasisha wananchi kuchangia nguvu kazi sambamba na michango ya fedha zitakazo pitishwa baada ya kamati ya kata itakayokaa leo jumamosi kujadili hali hiyo.
Ufaulu wa wanafunzi mwaka 2011 darasa la saba, kati ya wanafunzi 69 wameshinda 49 kujiunga kidato cha kwanza, ambapo kwa mujibu wa mratibu elimu kata hiyo Bwana JULIUS KATALE jumla au zaidi ya wanafunzi 200 wa kata nzima walichaguliwa kwenda kidato cha kwanza ila kutokana na mgogoro wa kata kutokuwa na shule ya kata walikuwa wamesalia wanafunzi 96, ambao hata hivyo wamekubaliwa kuendele kusoma katika shule ya kata Izigo.

Kata hiyo inakabiliwa na mgogoro wa kutokuwa na shule ya kutokana na kutegemea iliyojengwa na mbunge wa zamani RUTH MSAFIRI ambayo ni shule yake binafsi lakini hata hivyo bado haijamilika ujenzi wake.

Friday 9 March 2012

 Juu ni sura ya mbele ya shule hiyo iliyopo kata Katoke wilayani Muleba, na chini ni sehemu moja wapo ya jengo la shule hiyo yenye madarasa kadhaa na inatarajiwa kupokea wanafunzi wa Bweni wasichana.
 Akizungumzia mgogoro unaosemekana kuwepo kati ya wananchi na mbunge huyo Ruth Msafiri, amesema yeye anavyojua hakuna mgogoro kwasababu eneo hilo alipewa na serikali ya kijiji kupitia VDC miaka kumi iliyopita hivyo marumbano hayo yanapikwa kisiasa.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na Kamera hii wamesema eneo lenye ukubwa wa ekari 40 alipewa baada ya kuliomba kuwa anajenga shule ya kijamii lakini baada ya kushindwa ubunge ameamua kujitwalia kuwa anajenga shule binafsi, na wengine wanasema ni shule yake kwasababu hakuna mchango wowote wa mwananchi.

Mapema mwezi februari, mkuu wa mkoa wa Kagera alifanya ziara katika kata hiyo na alipopewa taarifa aliwataka viongozi wa VDC na WDC kukaa pamoja kupata ufumbuzi lakini akazuia wasijenge shule nyingine kabla ya kukamilisha walizokwishaanzisha.

Mpaka sasa hali ni tete kutokana kuwa kuwepo vikao mbalimbali vya baadhi ya viongozi WDC ikilaumu lakini yeye Ruth akisema VDC ilimpa kihalali.

Tuesday 6 March 2012

 Hapa juu hii ndiyo meza na Chemri vilivyoko kwenye chumba kinacholipiwa shilingi za kitanzania elfu nane(8,000) kwa usiku mmoja, na hii ni Gest ambayo jina lake limehifadhiwa.
 Hivi ni viatu aina ya Yeboyebo anavyopewa mteja kwa matumizi kama kanda mbili.Chini ni Bafu la kuogea lakini rangi zinazoonekana ni uchafu ambao unateleza na kuna harufu mbaya unapooga, bahati mbaya sabuni haikuwepo wala tauro hivyo ni juhudi za mteja mwenyewe
 Nilipofanya mahojiano na mama huyu amabAye pia hakupenda niweke jina lake kwenye vyombo, japo nilichukuwa picha hii kupitia mashine maalum, anasema gest hiyo ina jumla ya vyumba 18 na Bosi mwenyewe wala hana mpango wa kurekebisha chochote kwani wateja wanalipa, na nilipohoji aina ya wateja alisema hasa ni wasafiri ambao wanashuka kwenye mabasi kwani hawana pa kwenda vyumba vikiisha kwenye gest zingine.
JE! WADAU TUFANYE NINI KATIKA HILI AU TUYAFUMBIE MACHO TUENDELEE KUUMIA?

Saturday 3 March 2012

 Miongoni mwa watangazaji jembe wa michezo katika Kasibante Redio Bukoba Abdulrazak kulia aliyeshika kipande cha keki ametimiza miaka kadhaa ya kuzaliwa leo.
 Hapa anamlisha mkurugenzi wa Redio Kasibante fm Bwana ABDUL KAGASHEKI.
 Kama kawaida Abdulrazaki akimlisha keki mmliki wa Blog hii Nicolaus Mac Ngaiza-mwanaharakati.
 Huyu ni Meneja utawala Kasibante Fm Redio Abela Kamala akilishwa keki.
Emmanuel Mbaule meneja vipindi Kasibante Redio akilishwa keki na mtoto aliyezaliwa leo, katika ofisi za kasibante Redio.