Chama tawala cha zamani nchini Zambia cha Movement for Multiparty Democracy –MMD kimefutiwa usajili wake
baada ya kushindwa kulipa ada.
Msajili mkuu wa vyama vya siasa
nchini ZAMBIA Bwana Clement Andeleki, amesema kuwa vyama vya siasa vinatakiwa
kulipia ada ya mwaka, lakini MMD haijalipia tangu mwaka 1993 na mpaka sasa
inadaiwa zaidi ya kwacha milioni 390, sawa na dola zaidi ya milioni 74.
Akizungumza mbele ya waandhishi habari mjini Lusaka,
bwana Andeleki mesema anafuta usajili wa chama
hicho kwa kufuata sheria ya vyama siasa ya nchi hiyo.
Amemwambia Spika wa bunge la nchi hiyo Bwana Patrick Matibini kuwa uamuzi huo umebatilisha viti 53 vya wabunge wa chama hicho kuanzia leo, kwa kumtaka kutekeleza sheria hiyo kutowaruhusu kukanyaga bungeni tangu kutolewa kwa uamuzi huo.
Chama kitarudishiwa viti vyake vya bunge baada ya kupewa taarifa rasmi kupitia kwa Spika wa bunge.
Msajili huyo amesema kuwa uamuzi huo umefikiwa na ofisi yake baada ya kupokea malalamiko mbalimbali kuhusu kuonekana kuna ubaguzi kwa vyama vingine kulipa huku MMD ikiendelea kudaiwa kwa zaidi ya miaka 20.
MMD ilipoteza kiti cha urais katika uchaguzi wa mwaka jana baada ya mgombe wa upinzani kupitia Patriotic Front Bwana MICHAEL SATTA kuchukuwa madaraka kutoka kwa rais wa zamani wan chi hiyo RUPIA BANDA.
Tangu rais SATTA kuchukuwa madaraka ya nchi hiyo amegundua tuhuma mbalimbali za rushwa kwa viongozi MMD.
No comments:
Post a Comment