MKOA WA KAGERA KUANDAA MKUTANO WA KISWAHILI NA USHAHIRI KITAIFA;
Mkoa wa Kagera umeteuliwa kuwa mwandaaji wa mkutano
mkuu wa Usanifu wa Kiswahili na ushahiri Tanzania utakao-anza mwishoni mwa
mwezi huu.
Taarifa iliyotolewa na ofisi ya mkuu wa mkoa kagera,
imesema kuwa mkutano huo unatarajiwa kuudhuriwa na wajumbe zaidi ya 80 kutoka
mikoa mbalimbali hapa nchini.
Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali FABIAN INYASI MASSAWE,
ametumia fursa hiyo kuwaalika wananchi,
wadau, taasisi na makampuni mbalimbali kuhudhuria harambee itakayofanyika kesho
asubuhi katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa.
Hata hivyo, kanali MASSAWE amesema wakti wa mkutano
huo litafanyika kongamano litakalojadili changamoto litakalojadili changamoto
zinazoikali lugha ya Kiswahili hapa nchini.
Mkuu wa mkoa amesema kuwa Kongamano hilo litaongozwa na mabingwa wa lugha ya
Kiswahili kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment