MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Wednesday 25 March 2015

WAANDISHI WATAKIWA KUBADILIKA KIMTANDAO KULINGANA NA MAITAJI KUBADILIKA

Bwana HassahMwambene akiongea na waandishi habari


Kubadilika kwa teknolojia na hali halisi ya maisha, kumebadilisha tasnia ya habari hivyo kuwalazimu waadishi wa habari wabadilike kulingana na hali hiyo.

Akizungumza na waandishi wa mjini Dodoma, mkurugenzi wa habari maelezo Bwana Hassah Mwambene, amesema kuwa wanahabari waende sambamba na wanaowahabarisha kwa kuwapa habari zilizo sahihi na zenye kuleta mabadiliko.

Bwana Mwambene amefafanua kuwa matumizi ya mtandao kihabari yanakuwa makubwa zaidi kwasasa, huku akiongeza kuwa kuna kila sababu ya kuweka utaratibu maalumu kuwezesha watumiaji kuweka habari zenye tija kwani watakuwa wakifuatiliwa na kusimamiwa na mamlaka. 

Amesema ukishakuwa mwanahabari, unatakiwa kuchambua mambo mambo buhimu kuwekwa kwenye chombo husika,  kwa kuvaa viatu vya Yule anayeandikwa au kutangazwa kama umemtendea vyema au vibaya, huku akitolea mfano picha za utupu na sura za watu zinazowekwa na baadhi ya wamiliki wa mitandao kwa udhalilishaji.



Amesisitiza kuwa Tanzania imekuwa na baadhi ya wadau wanaojidhalilisha na kuingiza mijada kati ya Tanzania na mataifa mengine, kwasababu ya watanzania kubeza mambo yaliyopo nchini badala ya kutafuta jinsi ya kurekebisha.

Waandishi habari 20 kutoka kanda mbalimbali wanaounda mtandao wa SAUTI, wanaendelea na mafunzo ya kuandika na kutangaza habari kupitia mtandao, yaliyodhaminiwa na mfuko wa waandishi wa habari Tanzania TMF, ambapo pia wanajadili jinsi ya uendelezaji wa taasisi ya SAUTI kwa lengo la kuwafikia wanyonge na kuleta sauti zao adharani.
 

Na Mwanaharakati.

SOMA MAGAZETI YA LEO 25 MACH 2015










Na Mwanaharakati.

Tuesday 24 March 2015

ALICHOKIONA RAIS KIKWETE BAADA YA KUTEMBELEA WAHANGA 1500 WA MAFURIKO BUGURUNI HIKI HAPA

Rais Jakaya Kikwete amefanya ziara ya kushtukiza katika eneo la Buguruni Mnyamani ili kujionea madhara makubwa ya mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam na kusababisha zaidi ya watu 1500 kukosa hifadhi baada ya nyumba zao kuingiwa na maji.

Baada ya Rais Kikwete kuwasili  katika eneo hilo amebaini tatizo kuwa linatokana na ukosekanaji wa mtaro wenye uwezowa kupitisha maji yanayozibwa na uchafu pamoja na ujenzi usiosalama................

SOMA ALIYEDAI KULAZIMISHWA KWENDA KWA LOWASA, ABDALAH BULEMBO AKANWA NA WAJUMBE WA JUMUHIYA YA WAZAZI, NGONYANI AKATAA KUOMBA RADHI

Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Dodoma, Dk. Damas Mukassa, akiwaonesha waandishi wa habari picha ambayo mjumbe mwenzao alisema wamelazimishwa kwewnda kwa Lowassa jinsi alivyo kula pozi na Lowassa.

Huyu ndiye Jackline Ngonyani anayeoneshwa kwenye picha hapo juu, aliyejitambulisha kwa Lowassa kama ‘Maji mafupi’ na kutoa salam za shukrani kwa wana Ruvuma kwa jinsi Lowassa alivyoshiriki katika mazishi ya Capt.John Komba lakini jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa alilazimishwa kushiriki katika msafara huo. Lakini wenzake wanasema yeye alikuwa mmoja wa waratibu.
Naye Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani, alisema yeye alielezwa kuhusiana na safari hiyo na rafiki yake Vioroka Kajoko.
“Nimekuwa katika jumuiya hii kwa miaka 15. Siko tayari kuchaguliwa kiongozi, marafiki wala maadui. Mimi siko tayari  kuomba radhi kwasababu sina kosa nililotenda,”alisema Ngonyani.
Alisema hajawahi kumshawishi mtu wala kumlazimisha mtu kumpenda mtu anayempenda yeye.


VIONGOZI waliotajwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCMTaifa, Abdallah Bulembo, kuratibu safari ya baadhji ya wajumbe wa jumuia hiyo na baraza la Wazazi Taifa kwenda kumsalimia Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa leo wamekanusha vikali kuhusika na uratibu wa baraza hilo.

Jana Bulembo aliwashukia wajumbe waliokwenda nyumbani kwa Waziri Mkuu wa Zamani, Edward lowassa,na kumchakingaia fedha na kumshawishi..............

NDEGE ILIYOANGUKA, KISANDUKU CHA KUMBUKUMBU CHAPATIKANA

Ni ndege ya abiria inayomilikiwa na shirika la ndege la Germanwing Airbus A320 Imeanguka katika milima ya Alps nchini Ufaransa. 

Ndege hiyo ilikuwa imewabeba abiria 142, wahudumu 6 na marubani 2ikitoka Barcelona Uhispania kuelekea Duesseldorf.

Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa chini ya nembo Germanwings imeripotiwa kuanguka karibu na mji wa Digne.

Ndege hiyo ya A320 ilianguka saa tano asubuhi katika Kusini mwa Milima ya Alps.
Viongozi wa Ujerumani na Ufaransa wanaendelea kushauriana kuhusiana na mkasa huo unaowakabilia macho.

Ndege hiyo ya Ujerumani imeanguka katika eneo lisilo na mijengo ambalo halifikiki kwa urahisi nchini Ufaransa Kusini mwa Milima ya Alps.

Taarifa inasema kisanduku cha kumbukumbu kimepatikana na kinaendelea kuchunguzwa ili kujua kamahali mbaya ya hewa ndiyo imesababisha ajali hiyo au vinginevyo.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametaja ajali hiyo kama mkasa na amesema kuwa uwezekano wa kuwapata watu wakiwa hai ni mgumu.

Hali ya hewa katika eneo hilo ilitajwa kuwa nzuri na kituo maalumu cha kukabiliana na mikasa kimetengwa kukabiliana na mkasa huo.

Waziri wa Maswala ya ndani ya nchi uko njiani kuelekea mahali pa ajali hiyo.
Vyombo vya habari nchini Ufaransa vinasema kuwa ndege hiyo ilituma ujumbe wa kuwa hatarini kabla ya mawasiliano yake kutoweka .

Na Mwanaharakati.

LIVE UPDATES: GERMANWINGS FLIGHT CRASHES IN FRENCH ALPS; 150 FEARED DEAD, BLACK BOX FOUND

  • GERMANWINGS AIRBUS A320 CRASHES IN SOUTHERN FRENCH ALPS
  • 144 PASSENGERS AND SIX CREW ON BOARD ALL FEARED DEAD
  • PASSENGER JET HAD BEEN TRAVELING FROM BARCELONA TO DUSSELDORF
  • GERMANWINGS CEO: PLANE DESCENDED 31,000FT IN 8 MINUTES BEFORE CRASH
  • DEBRIS HAS BEEN LOCATED ON THE ALPS AT AN ALTITUDE OF ABOUT 6,500 FT 
  • 16 GERMAN HIGH SCHOOL STUDENTS BELIEVED TO BE ON BOARD
  • DEADLIEST CRASH ON FRENCH SOIL SINCE 2000
  • WEATHER WAS REPORTEDLY CALM AT TIME OF CRASH
  • CAPTAIN HAD MORE THAN 10 YEARS OF FLIGHT EXPERIENCE AND MORE THAN 6,000 FLIGHT HOURS
  • FRENCH OFFICIALS SAY ONE OF THE PLANE'S BLACK BOXES HAS BEEN LOCATED
 "This is the hour in which we all feel deep sorrow," German Chancellor Angela Merkel told reporters, adding that she was planning to travel to the crash site.

A recovery team has reached the crash site but there are fears that a looming storm could hamper its work.
Bruce Robin, a prosecutor from Marseille, told the Reuters news agency that he had seen the wreckage of the aircraft from a helicopter.

"The body of the plane is in a state of destruction, there is not one intact piece of wing or fuselage," he said.

Na Mwanaharakati.

Breaking news! Ndege yadondoka ikiwa na watu zaidi ya 142

Taarifa zinasema kuwa ndege hiyo kutoka Barcelona kwenda Dusseldorf Ilikuwa na marubani wawili na wahudumu wanne.

Ni aina ya airbus A320 kwa mujibu wa Germanwings
Na Mwanaharakati.

KIFO CHA VENGU WA ORIGINAL COMMEDY NI UZUSHI

Taarifa za kifo cha Vengu ambaye majina halisi ni Joseph Shamba simesambaa ktk vyombo mbalimbali vya habari, ambaye hatahivyo ameugua kwa kipindi kirefu na kupelekwa nchini India kwa matibabu.

Kwa mujibu wa Kiongozi wa kundi hill Seck, Vengu amekuwa akizushiwa kifo mara kwa mara hivyo na leo wamezusha tu, anasema.

Na Mwanaharakati.

Saturday 21 March 2015

KAGASHEKI; WATENDAJI WA SERIKALI WASIHARIBU KAZI ZA WANANCHI KWA KUSINGIZIA WANASIASA KUWA NDIYO WANASABABISHA MATATIZO, AZUNGUMZIA MASUALA MATATU MAZITO MANISPAA YA BUKOBA.

UJENZI WA SOKO, MAUAJI NA UCHOMAJI MAKANISA PAMOJA NA USAJIRI WA PIKIPIKI


Balozi Kagasheki ambaye pia ni mbunge jimbo la Bukoba mjini CCM, amesema kuwa lazima masuala ya wananchi yasimamiwe kwa pamoja kwasababu wanasiasa wanafuta dola na kuajiri watalaamu watekeleze mambo ya wananchi.
Amesema kuwa kujenga soko la kisasa ni muhimu lakini wanatafuta sehemu pembezoni mwa mji ili kuupanua na watu wafanye biashara kwa uhuru, uhalifu ulioibuka manispaa ya Bukoba amesema kuwa wanashirikiana na kamanda wa polisi kuukomesha wanameshaweka mkakati mbadala lakini baadhi ya wavunjifu wa amani wasitumie siasa kuhatarisha amani iliyopo...................

NCCR-MAGEUZI YATIMUA VIONGOZI





Chama Cha (NCCR - MAGEUZI) kimewatimua viongozi wake katika Jimbo la Nyamagana Jijini Mwanza kwa tuhuma za uzembe na usaliti kwenye chama hicho.

Habari kutoka ndani ya chama hicho bila ufafanuzi wa usaliti huo, zinasema waliofukuzwa kwa uzembe na usaliti ni pamoja na James Chacha M/kiti Jimbo Nyamagana ambaye anatuhumiwa kuwa mlevi wa kupindukia na kushirikiana na CCM.

Katibu wa jimbo Bw, Mrisho Ntunga na mwingine ni Shaaban Moshi Katibu wa Vijana Jimbo Nyamagana, M/kiti wa Vijana Jimbo hilo Bw; Nicolas Jovinie Clinton amesema kiongozi wa vijana wamemtimua kwa uzembe uliokithiri na kusema uchaguzi wa kujaza nafasi hizo utafanyika tarehe 22 mwezi huu.
 


Na Mwanaharakati.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI 21 MACH 2015


MASKINI ZITTO KABWE, BARUA YAKE INATIA HURUMA


Na Mwanaharakati.

Thursday 19 March 2015

WANANCHI KATA KAGONDO MANISPAA YA BUKOBA WAKATAA KUMSIKILIZA DIWANI WAO BAADA YA KUSHINDWA KUITISHA MIKUTANO TANGU AINGIE MADARAKANI.



Diwani kata Kagondo manispaa ya Bukoba, ambaye hatahivyo alikuwa meya wa manispaa ya Bukoba Anatory Aman, amezomewa na wananchi baada ya kuitisha mkutano wa hadhara kuzungumzia matatizo ya maji yanayowakabili wananchi wa kata hiyo.

Katika mkutano huo, Mh Aman alitaka kujua undani wa matatizo ya maji yanayowakabili wananchi hao, ambao hatahivyo wameshalalamika zaidi ya mwaka sasa, tangu kujengewa kwa vyanzo mbalimbali vya maji na kusababisha ukosefu mkubwa wa maji kwa wananchi hao....................

MAGAZETI YA LEO MACH 19 2015 YOTE YAKO HAPA





Tuesday 17 March 2015

BUNGE LILILOFUNGULIWA LEO USIPITWE NA TAARIFA ZA MAGAZETI YA LEO.

MASKINI JOSE KAMILION (Chameleone),SOMA TAARIFA YA KIFO HAPA

Taarifa zilizotolewa na mtandao wa burudani nchiniUganda "New Vision Uganda" Jose Chameleone amesema kusikitishwa na kifo chamdogo wake Emmanuel Mayanja Hummertone aliyejulikana zaidi kama AK47, mwanamuziki na mwimbaji wa dancehall nchini Ugandan, kuwa amefariki akiwa njiani kupelekwa hospitali ya Nsambya.

Kifo cha msanii huyo AK47,kimetokea usiku wa kuamkia leo nchini Uganda, baada ya kuanguka bafuni na taarifa za awali zinasema amefarikimuda mfupi kabla ya kufikishwa hospitali ya Nsambya, kutokana na damukuvujia ndani.
Emmanuel Mayanja
 Dr Jose amesema kuwa kimekuja wakati mgumu sana kwake huku akiongeza kuwa familia imepoteza msanii aliyekuwa anakuja juu sana katika muziki.

Na Mwanaharakati.

Monday 16 March 2015

AJALI INAYOTAJWA KUUA ABIRIA 13 SINGIDA, KAMANDA WA POLISI SINGIDA ASEMA


Kamanda Thobias Sedoyeka, amesema habari zinazoendelea kuruhswa leo katika mitandao na baadhi ya redio na Tv kama habari mpasuko, wananchi wazipuuze kwani ni ajali iliyotokea januari mwaka jana.

Awali zimesambazwa habari kuwa ................

HOSTEL ZA MABIBO KUUNGUA MOTO TAZAMA PICHA NA TAARIFA YA AWALI HAPA.

Taarifa zinasema kuwa moto huo umeibuka katika mabweni ya Hostel za wasichana Mabibo ambapo kikosi cha zimamoto kimeanza shughuli ya kuzima moto huo, ambapo hatahivyo wamesemekana kuchelewa kufika katika eneo la tukio.










Na Mwanaharakati.

SOMA HABARI KAMILI, ALIVYOPAMBANA NA MAMBA KWA NUSU SAA

MWENYEKITI wa Kamati ya Shule ya Msingi Udasi mwambao mwa Ziwa Tanganyika, kata ya Kabwe wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Ismail Ndomboya (42) amenusurika kuuawa na mamba kwa kupambana kijasiri na mnyama huyo kwa zaidi ya nusu saa.
Hata hivyo, licha ya kuokoa maisha yake mnyama huyo katika mapambano hayo alimng’ata na kumnyofoa mkono wake wa kulia na kutokomea nao ziwani...............