MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Saturday 21 March 2015

NCCR-MAGEUZI YATIMUA VIONGOZI





Chama Cha (NCCR - MAGEUZI) kimewatimua viongozi wake katika Jimbo la Nyamagana Jijini Mwanza kwa tuhuma za uzembe na usaliti kwenye chama hicho.

Habari kutoka ndani ya chama hicho bila ufafanuzi wa usaliti huo, zinasema waliofukuzwa kwa uzembe na usaliti ni pamoja na James Chacha M/kiti Jimbo Nyamagana ambaye anatuhumiwa kuwa mlevi wa kupindukia na kushirikiana na CCM.

Katibu wa jimbo Bw, Mrisho Ntunga na mwingine ni Shaaban Moshi Katibu wa Vijana Jimbo Nyamagana, M/kiti wa Vijana Jimbo hilo Bw; Nicolas Jovinie Clinton amesema kiongozi wa vijana wamemtimua kwa uzembe uliokithiri na kusema uchaguzi wa kujaza nafasi hizo utafanyika tarehe 22 mwezi huu.
 


Na Mwanaharakati.

No comments: