MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Wednesday 27 February 2013

TANZANIA YAPATA MFUMO WA UTAMBUZI WA BIDHAA


TATIZO la Tanzania la kuuza bidhaa nje na kushindana katika Soko la Kimataifa limetatuka baada ya sasa kuwa imeingia katika mfumo wa kimataifa wa utambuzi wa bidhaa kwa kutumia Nembo za Mistari (Bar Code).
Hayo yalifahamika wakati  Waziri Mkuu Mizengo Pinda  anazindua mpango mkakati wa miaka mitano wa taasisi inayosimamia nembo hiyo nchini Global Standard One (GS1) – Tanzania National Ltd., kwenye ukumbi wa Blue Pearl Hotel, Ubungo jijini Dar es Salaam leo (Jumatano Feb. 27, 2013) mchana.
Namba ya utambulisho ya nembo hiyo kwa Tanzania ni 620 na tayari imeunganishwa katika mtandao wa GS1 duniani. Mpaka sasa wazalishaji 370 wa bidhaa mbalimbali wamekwishapata na wanatumia nembo hiyo wakiwa na jumla ya bidhaa 6,000 sokoni.
“Hili ni jambo jema. Bado nina imani kwamba tunaweza kufanya vizuri zaidi  na kupiga hatua kubwa zaidi kama tukidhamiria. Changamoto ninayoiona sasa ni jinsi ya kutangaza mafanikio hayo ambayo tayari tumeyafikia,” Pinda alisema.
Waziri Mkuu aliitaka GS1 Tanzania, kutumia matangazo ya Televisheni, kushiriki katika Maonyesho ya Kilimo na Nane Nane na Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara kutangaza nembo hiyo ili wazalishaji wengi zaidi wajiungenayo.
GS1 ni Shirika la Kimataifa lisilo la kiserikali na lisilo la faida lililoanzishwa mwaka 2005 na lenye makao makuu yake Brussels, Ubelgiji. Shirika hilo limeisaidia Tanzania kuanzisha shughuli hiyo nchini, miaka miwili iliyopita.
Kabla ya GS1 Tanzania, wazalishaji wa bidhaa wa Tanzania walikuwa wanapata nembo Kenya na Afrika Kusini na kuonyesha kama vile bidhaa hizo zinatoka katika nchi hizo.
Waziri Mkuu alisema kuanzishwa kwa GS1 Tanzania ni sehemu ya matokeo ya nia ya serikali ya awamu ya nne kuhakikisha kuwa chombo hicho kinaanzishwa nchini kama moja ya taasisi za viwango nchini.
Alisema nembo hiyo ni fursa nzuri kwa wazalishaji, hasa wajasiriamali wadogo, kupenya kwenye soko la kimataifa na kupata biashara nzuri na fedha nyingi.
Pinda aliliagiza Shirika la Viwango nchini TBS na Wakala wa Usajili wa Makampuni na Leseni za Biashara, kutoa umuhimu wa kwanza kwa wazalishaji wadogo wanapotaka kupatiwa nembo ya viwango na kusajili biashara.
“TBS muwe na kitengo cha wafanyabiashara wadogo na wajasiriamali. Msiwachanganye hawa na wafanya biashara wakubwa, mtawabana sana na watashindwa kunyanyuka,” alisema.
Katika sherehe hiyo, Waziri Mkuu alizindua mpango huo kwa kukata utepe na kuanzisha king’ora. Pia litoa mfano wa nembo hiyo ya mistari kwa wazalishaji mbalimbali.
Waziri Mkuu pia yeye mwenyewe alikabidhiwa nembo hiyo kwa kuzalisha asali.
(mwisho)
Imetolewa na:
          Ofisi ya Waziri Mkuu,
          S.L.P. 3021,
          DAR ES SALAAM

RAIS KIKWETE AMETEMBELEA JKT KWA MARA YA KWANZA TANGU KUWA KWAKE RAIS WA NCHI HII

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akielekea kwenye uwanja wa sherehe baada ya kupata maelezo na kutoa maagizo kwa  uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alipotembelea makao makuu yake  leo February 27, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia walihudhuria.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jijini Dar es salaam alipotembelea leo February 27, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia walihudhuria.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jijini Dar es salaam alipotembelea leo February 27, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia wapo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na kada mbalimbali za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alipotembelea leo February 27, 2013
MWANA HARAKATI/ PICHA NA IKULU

PAPA BENEDICT 16 AFANYA MHADHALA WA MWISHO KATIKA UONGOZI WAKE

Wkati wa kuwaanga maelfu ya waumi hao, amewabusu watoto wawili waliokuwa karibu na njia aliyozungukia kwenye gari maalumu.

Mapema mwezi huu, papa Benedict wa 16, alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo kutokana na umri kuwa mkubwa pamoja na matatizo ya kiafya ambapo kesho FEB 28 2013, ndiyo siku ya mwisho katika utawala wake.

Tuesday 26 February 2013

RAIS AFANYA UTEZI


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


Coat of Arms
PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Jaji na Balozi Mstaafu Mheshimiwa Hamis Amiri Msumi kuwa Mwenyekiti wa BARAZA LA MAADILI.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumanne, 26 Februari, 2013 jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue, inasema kuwa uteuzi huo ulianza Februari 18, mwaka huu, 2013.

         “Mwisho”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
DAR ES SALAAM.
26 Februari, 2013

BARAZA LA BAJETI LA MADIWANI WA MANISPAA YA BUKOBA LASHINDWA KUFANYIKA BAADA YA IDADI YA MADIWANI WANAOTAKIWA KUTOTIMIA



Kikao cha kujadili bajeti cha Baraza la madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba leo kimelazimika kuahirishwa kutokana na sababu ya akidi kutotimia ambapo wajumbe walioudhuria kikao hicho walikuwa 11 kati ya 24.

Mkurugenzi wa manispaa ya BUKOBA Bwana HAMIS KAPUTA  amesema kuwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za uendeshaji wa vikao vya alimashauri kikao hicho kisingeweza kuendelea kama wajumbe hawajafika nusu ya wajumbe wote wa kikao hicho.

Kikao cha kujadili bajeti cha  baraza la madiwani kimeharishwa na mstahiki MAE wa manispaa ya Bukoba DR ANATHORY AMANI kwa siku saba na endapo akidi isipokamirika bajeti itajadiliwa na wajumbe watakaoudhuria.

Wakati huo huo muheshimiwa mkuu wa wilaya ya Buoka bi ZIPORA PANGANI amewaomba watumishi wa serikali katika manispaa ya Bukoba kutojiusisha na migogoro ya siasa na kuonyesha itikadi zao sehemu za kazi na kuongeza kuwa atakaefanya hivyo atawajibishwa kwa mujibu wa sheria.

RAIS KIKWETE



THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


Coat of Arms
PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RAIS KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA  BABA
YAKE RAIS MUSEVENI
            Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete jana februari 23, 2013 aliungana na mamia ya wananchi wa Uganda katika mazishi ya Mzee Amos Kaguta (97), Baba wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda, yaliyofanyika katika kijiji cha Rwakitura, Magharibi ya Uganda.
Rais Kikwete aliwasili katika mazishi hayo akitokea Addis Ababa, mji Mkuu wa Ethiopia alipohudhuria Mkutano wa viongozi wa kutafuta amani ya kudumu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Akitoa salamu zake za rambirambi katika msiba huo, Rais Kikwete alisema kuwa Watanzania wapo pamoja na ndugu zao wa Uganda wakati huu wa majonzi na kusema kuwa yeye binafsi anampa pole Rais Museveni na familia yake na kumtaka awe na moyo wa subira katika kipindi hichi na kumuombea marehemu.
Rais Museveni alimshukuru Rais Kikwete kwa kufika katika msiba huo ambapo alisema kuwa Marehemu Mzee Amos atakumbukwa kwa kuithamini elimu ambapo aliwapeleka watoto wake shule na kwa kufanya mabadiliko ambapo alikubali kufuata njia bora za ufugaji wenye tija jambo ambalo ni gumu kwa wazee wengi wenye umri wake (97).
Rais Museveni alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana kuwatunza vyema wazazi wao ili waishi muda mrefu na kulaani tabia ya baadhi ya vijana kuishi kwa kutegemea mali za wazazi wao badala ya kuzalisha mali yao wenyewe akiongeza kuwa wazee wana hazina kubwa ya maarifa kutokana na kukumbana na changamoto nyingi katika maisha yao.
Marehemu Mzee Amos Kaguta alizaliwa mwaka 1916 katika kijiji cha Kabahambi, Kikoni Ntungamo nchini Uganda.
Rais Kikwete na ujumbe wake akiwemo Waziri wa Ulinzi Mh. Shamsi Vuai Nahodha waliondoka kurejea jijini Dar es Salaam baada ya mazishi hayo.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

25 Februari, 2013

TASWIRA HII LIMENIGUSA


MWANA HARAKATI

Mdahalo wa mwisho wa wagombea Kenya

Mdahalo huo umefanyika jana usiku wa kuamkia leo, ambapo wagombea wanane kutoka vyama mbalimbali wamejibu hoja mbalimbali, lakini kubwa zaidi mfumo uliotumika ni ulio tumika awali wa kuuliza swali katika kila kitengo ambapo nifrahi zaidi katika swali lililoelekezwa kwenye upande wa sekta ya ardhi na wagombea wakajibu kila mtu na swali lake.
Laira Odinga, yeye amesema ardhi iliyopo inatosha kwa shughuli za raia wake ila siyo ya ziada, na sheria ya nchi hiyo ikowazi kwa kila mwananchi kutumia ardhi kwa shudhuli za kiuchumi.

Upande wake Uhuru Kenyata, amesema kuwa katiba ya sasa haijawa wazi katika suala la ardhi hivyo inabidi kuweka mipango thabiti, lakini Mgombea ambaye anafahamika kama Dida, yeye amesema akiwa rais jambo la kwanza ataelimisha wananchi kuhusu umilikaji wa ardhi kwani wananchi wanakosa elimu hiyo.

Monday 18 February 2013

MKURUGENZI WA KADETFU AMEKABIDHI VITABU 21 KWA NYUMBA YA KUMBUKUMBU MKOANI KAGERA

Akikabidhi vitabu hivyo 21 kwenye Museum ya mkoa wa Kagera, mkurugenzi huyo Bwana YUSTO MCHURUZA, amesema kuwa ni vema wadau na mashirika yenye uwezo wa kuwafikia waliowengi na kutoa mafunzo kwao, ili kusaidia kueneza uelewa kwa wananchi, pamoja na kuhakikisha maliasili zinatunzwa kwa misingi inayotakiwa.

 Vitabu hivyo 21 vimetolewa na Marehemu KLAUS GOTCHLING wa nchini Ujerumani kwa ajili ya wananchi wa afrika hasa wana Kagera, kutokana na yeye kuishi nchini Tanzania na kufanya research mbalimbali za mambo ya kiafrika hasa kuhusu mkoa wa Kagera. PICHA CHINI NI MKURUGENZI WA KADETFU na MENEJA WA KAMPUNI YA UTALII YA KIROYERA Wiliam Rutta.
 Picha chini ni Wiliam Rutta akitoa ufafanuzi wa mojawapo wa kitabu miongoni mwa vile 21 vilivyotolewa kwa ajili ya makumbusho hayo.
 Ni picha ya marehemu KLAUS GOTCHLING, wakati wa uhai wake.

 Picha juu ni baadhi ya nyumba za mfano zinazopatikana mkoani Kagera, na chini ni moja ya kifaa cha muziki chenye kutumia "SANTURI" ambacho wakati huo kilikuwa katika mtindo uliofahamika kama wa kisasa.
MWANA HARAKATI

Thursday 14 February 2013

SIKU YA WAPENDANAO

KASIBANTE FM REDIO BUKOBA WALA CHAKULA CHA MCHANA NA WATOTO YATIMA




MWANA HARAKATI

Thursday 7 February 2013

RAIS AZINDUA VITAMBULISHO VYA TAIFA

Pamoja na uzinduzi huo, rais amewataka wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali na taasisi za kiraia kumuunga mkono mkurugenzi wa NIDA Bwana MAIMU, ili kuwezesha kufanikisha zoezi hilo kikamilifu.
 Picha juu ni mfano wa kitambulisho kilichozinduliwa hii leo, na kugawiwa kwa baadhi ya  viongozi amabo tayari wameshatengenezewa vitambulisho, na chini ni picha pamoja. Nikutake radhi kwa mwonekano hafifu wa picha zetu.
MWANA HARAKATI