Kikao cha kujadili bajeti cha Baraza la madiwani wa
halmashauri ya manispaa ya Bukoba leo kimelazimika kuahirishwa kutokana na
sababu ya akidi kutotimia ambapo wajumbe walioudhuria kikao hicho walikuwa 11
kati ya 24.
Mkurugenzi wa manispaa ya BUKOBA Bwana HAMIS KAPUTA amesema kuwa kwa mujibu wa sheria na kanuni
za uendeshaji wa vikao vya alimashauri kikao hicho kisingeweza kuendelea kama wajumbe hawajafika nusu ya wajumbe wote wa kikao
hicho.
Kikao cha kujadili bajeti cha baraza la madiwani kimeharishwa na mstahiki
MAE wa manispaa ya Bukoba DR ANATHORY AMANI kwa siku saba na endapo akidi
isipokamirika bajeti itajadiliwa na wajumbe watakaoudhuria.
Wakati huo huo muheshimiwa mkuu wa wilaya ya Buoka bi ZIPORA
PANGANI amewaomba watumishi wa serikali katika manispaa ya Bukoba kutojiusisha
na migogoro ya siasa na kuonyesha itikadi zao sehemu za kazi na kuongeza kuwa
atakaefanya hivyo atawajibishwa kwa mujibu wa sheria.
No comments:
Post a Comment