MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Wednesday 27 May 2015

HAYA NDIYO MAUAJI MAPYA YA KUTISHA BUKOBA, WENGINE WACHINJWA LEO

. Waliochinjwa leo watolewa pua,
. Kwa mara ya kwanza auawa mwanamke,
. Tukio moja lafanyika vijijini.
Watu wawili wameuawa kwa kuchinjwa, na hatimaye kutolewa pua, huku wakikatwa na kitu chenye ncha kazi kisogoni, mauaji ambayo yanafanana, ambapo mtandao huu umetembelea maeneo ya kata Karabagaine  katika kijiji cha Kitwe, na kukuta Joseph Gabriel, aliyekuwa akifanya vibarua mbalimbali kukutwa amekatwa na kitu chenye ncha kali, huku akiondolewa sehemu ya pua na shavu la kushoto, huku kukiwa na kipande cha sabuni inayoonesha kuwa aidha alitoka au akienda kukitumia.
Mtandao huu umezungumza na mwenyekiti wa kijiji Kitwe, muda mfupi kabla ya kuwasili poilisi, ambao hatahivyo walichelewa kufika kutokana na kuwa katika tukio lingine lililotokea siku moja na hilo la Kitwe.
 
Mashuuda waliozungumza na KANDAYAZIWA, wamesema kuwa aina hii ya mauaji na kuondoa pua za marehemu ilikuwa haijawahi kutokea, ukiachilia mbali mauaji yale alipouawa kijana katika barabara ya Kagondo Rwamishenye wiki chache zilizopita.

Mauaji mengine yaliyofanyika leo, inasemekana mwanamke ambaye jina lake halikufahamika maramoja, ameuawa kwa kuchinjwa na pua yake kuokotwa katika maeneo ya karibu na tukio, katika mtaa wa Kibeta kata Kibeta.
Mtandao huu umefika katika eneo la tukio na kukuta mwili wa marehemu umeshaondolewa na polisi, kama picha inavyoonesha chini, lakini taarifa aliyotupa mmoja wa askari waliofika kwenye tukio hilo, amesema kuwa pua ya mama huyo umeokotwa maeneo jirani huku katika eneo hilo kutokutikana kiasi cha damu ya kumwagika ispokuwa matone tu ya damu.

Mwezi uliopita, polisi Kagera ilitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu mauaji ya manispaa ya Bukoba, ikieleza kuwashikilia watu kadhaa na kinara wa mauaji hayo, ambao majina yamehifadhiwa kwasababu za kiusalama, huku ikisema kuwa watu wawili waliuawa na polisi kwa kupigwa risasi, wakati wakiwapelka kwenye maeneo wanakopangia uhalifu huko Bugabo halmashauri ya Bukoba.
Na Mwanaharakati.

No comments: