Baada ya kifo chake saa 5;00 asubuhi saa za huko, ambazo ni 12;00 jioni kwa afrika mashariki, baada ya kufanya mawasiliano na familia ya marehemu, mbunge Kagasheki alipewa taarifa kuwa taratibu za kusafirisha mwili zinafanyika tayari kuletwa Bukoba kwa maziko.
Bw. Samuel N. Luangisa ni nani?
Ni mzaliwa wa Bukoba mmoja kati ya
waasisi wa TANU na hatimaye CCM, ambaye alipata kuwa mkuu wa mkoa wa kwanza wa
baada ya uhuru (1961–1964), ambaye hatahivyo alikuwa miongoni mwa
waliopendekeza mkoa huo kuitwa Kagera badala ya jina la awali la mkoa wa Ziwa
magaharibi.
Jina hilo lilibadilishwa na kuwa
“Kagera” mwaka 1979, mara baada ya vita kati ya Tanzania na Uganda, ambapo
mkoa, chini ya uongozi wa Mkuu wa Mkoa, aliyekuwepo wakati huo, Capt. Peter
Kafanabo, ulipendekeza uitwe “Kagera”chini ya ushauriano wa mzee Luangisa.
SAMWEL RUANGISA alipata kuwa mbunge wa jamuhuri ya muungano kupitia jimbo
la Bukoba mjini kwa tiketi ya CCM kati ya 1985-1990, na baada ya hapo
ameendelea kuwa diwani wa kata Kitendaguro anakozaliwa hadi 2014 alipovuliwa
udiwani na mahakama kutokana na mgogoro uliojitokeza na kushindwa kuudhulia
baadhi ya vikao vya baraza la madiwani, akiwa miongoni mwa madiwani sita
waliovuliwa kati ya madiwani 24 wa manispaa hiyo.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment