MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday 27 May 2012

BALOZI WA KWANZA TANZANIA KATIKA UMOJA WA MATAIFA AZIKWA RASMI MKOANI KAGERA

Mazishi ya Balozi wa kwanza wa Tanganyika Huru katika Umoja wa Mataifa- UN, Dk  KYARUZI VEDAST KYALAKISHAIJA, yamefanyika leo,  katika kijiji cha  Kasambya wilayani Misenyi mkoani Kagera.


Misa ya mazishi hayo imeongozwa na Askofu wa jimbo kuu la Bukoba Mhashamu NESTORIUS TIMANYWA.


Dk KYARUZI, alifariki jumapili Mei 20, mwaka huu akiwa na umri wa miaka 92, baada ya kulazwa katika hospitali ya rufaa ya Bukoba.

Dr KYARUZI atakumbukwa na wengi, kwa mchango wake mkubwa kwa taifa la Tanganyika, kabla ya Uhuru,  na TANZANIA, baada ya Uhuru.

Wakati wa Uhai wake, Dr KYARUZI, alilitumikia taifa kwa uaminifu mkubwa katika nyanja mbalimbali, kama Mwana diplomasia na Msomi wa fani ya Udaktari.
Alizaliwa Februari 21, 1921 kijijini KIGARAMA, Kanyigo, Kiziba. Alipata elimu yake ya Msingi katika shule za Kashasha, Mugana na Kajunguti, kabla ya kujiunga na Shule ya St Mary’s Tabora kwa masomo ya Sekondari.

Kati ya mwaka 1942 hadi 1948 alikuwa Chuo Kikuu cha Makerere, ambapo alihitimu kwa kupata shahada ya Udakatari, akiwa miongoni mwa Watanzania wa kwanza kupata nafasi hiyo.

Akiwa Makerere, Dr KYARUZI alikutana na Baba wa Taifa, marehemu Mwl JULIUS KAMBARAGE NYERERE, ambapo walianzisha tawi la Tanganyika African Association-TAA.
                           
                                             WATOTO WA MAREHEMU

                               




                            
                                  SAFARI YA MWISHO KWA DOKTA IMEFIKIA HAPA
                           

                           Ameacha mjane na watoto na wajukuu.

SYRIA YAENDELEA KUPOTEZA RAIA WAKE

HII NI PICHA IKIONESHA BAADHI YA MIILI YA WATOTO WALIOKUFA.

Saturday 26 May 2012

MWANAMUZIKI CONGO DRC AFARIKI DUNIA


  


Alipata umaarufu wakati alipokuwa akiimba na Hayati Luwambo Makiadi na Lutumba Simaro . Wimbo wake wa MOKOLO NA KOFUFA (Siku nitakayo fariki) ndio maarufu sana katika eneo la Afrika Mashariki na Kati na uliompandisha kwenye jukwaa la waimbaji bora wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

NAPE AZUNGUMZA NA WANA CCM MKOANI KAGERA


 

Baadhi ya wananchama waliokusanyika katika mkutano wao na katibu mwenezi Bwana Nnauye.




MSIMU WA SENENE UNAVYOCHANGIA WATOTO WA SHULE KUTOKWENDA SHULENI

 
 Baadhi ya wauzaji wa senene wanasema kuwa wameshajitahidi kuwafukuza ila wanashindwa kutokana na watoto hao kuonekana wanahitaji la pesa kulingana na familia zao.
 Chini ni magunia ya senene ambayo yamewekwa na wachuuzi wakati ambao wanunuzi wananunua fungu yaani mfuko mdogo wa plastiki kwa shilingi elfu moja.

Thursday 24 May 2012

KAMATI YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI IMEIKATAA TAARIFA YA MATUMIZI YA FEDHA ZA SERIKALI MKOANI KAGERA.

 
 Akiongea mbele ya waaandishi wa habari mwenyekiti huyo John Cheyo, amesema kamati haijaridhishwa na matumizi ya serikali yanaoishia mwezi june mwaka 2011, akifafanua kuwa miongoni mwa miradi iliyoifanya kamati kusikitika ni pamoja na usitishwaji wa mradi wa Bilioni 5.06 wa Kabanga Bay ulioasitishwa na serikali ya mkoa, akisema kuwa umeishagharimu serikali bilioni 1.7 kwa kusema kuwa mkandarasi aliyekatishiwa mkataba akiipeleka serikali mahakamani atalipwa na nani, lakini pia hasara ya bilioni 17 italipwa na nani?
 Amesema kuwa kutokana na utambulisho wa afisa Mhasibu ambaye ni katibu tawala NASORO MNAMBILA, imebainika kuwa hausiki katika baadhi ya mambo hivyo ili kujiridhisha itabidi atafutwe aliyekuwa akishika nafasi hiyo awali ambaye ni MARIA BIRIA ili kupata maelezo kamili June 1 mwaka huu.
 Jambo jingine ni matumizi ya fedha katika ujenzi wa jengo la ofisi ya mkoa kwa kiasi cha shilingi bilioni 10.8 ambazo imeonekana ni kiasi kikubwa, ikasemekana kuwa kutokana na kuwa kuna ikama kubwa ya watumishi imeonekana ni kiasi kikubwa sana hivyo inabidi litolewe maelezo.
Pamoja na hiyo Bwana Cheyo aliyeambatana na ujumbe wa kamati yake amesema hali hii inaonesha ukiukwaji mkubwa wa sheria za serikali katika matumizi ya fedha.

Naye katibu tawala mkoani Kagera Bwana Mnambila amesema kuwa wamepokea taarifa hiyo na ameahidi kuwa wataifa kazi yeye na watendaji katika serikali ya mkoa na ameahidi kutoa majibu yaliyosahihi katika mkutano utakaofanyika huko Dar es salaam ukihusisha kamati hiyo pamoja na viongozi waliokuwa mkoani kagera na mabo wapo kwa sasa.

Sunday 20 May 2012

TGNP KUFANYA MAFUNZO MIKOANI.


TANZANIA GENDER NETWORKING PROGRAMME (TGNP)
P.O. Box 8921, Dar es Salaam, TANZANIA; Gender Resource Centre, Mabibo Road,
Tel. 255 022  2443205/2443286/2443450;
Mobile 255  0754 784050, 0715 784050; 0784 784050 Fax 255  022 2443244; Email info@tgnp.org ; web www.tgnp.org
 

16/05/2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TGNP  kufanya mafunzo ya uraghibishi mikoa mitatu
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) utafanya mafunzo ya uraghibishi ngazi ya jamii kwa  mikoa mitatu ya Shinyanga, Morogoro na Mbeya, ambapo  katika mikoa hiyo watajikita katika wilaya za  Mbeya vijijini, Morogoro Vijijini na  Kishapu. Mafunzo haya yataanza tarehe 22 – Mei 2011 – 2 June 2012.

Mafunzo hayo yana malengo ya kuwajengea wananchi uwezo wa kushiriki, kuchambua kwa kina fursa na changamoto zinazowakabili katika mazingira yao na kuyatafutia ufumbuzi  kwa kujenga vuguvugu la ukombozi wa wanawake kimapinduzi.

Matarajio ya matokeo makubwa ya  Mafunzo ya Uraghibishi  na utafiti shirikishi wa kijamii,yatawashirikisha wanawake na wanaume   walioko pembezoni  katika kutambua fursa walizonazo katika kudai au kuingizwa kwa madai  yao katika mchakato wa Katiba mpya, kudai mabadiliko ya sera, kimfumo,  na haki ya uchumi kwa makundi yaliyoko pembezoni.

Mafunzo haya pia yatawajengea wanajamii uwezo wa kushiriki ipasavyo katika mchakato wa kutoa maoni kwa Tume ya Kuratibu Mchakato wa katiba mpya, haki ya uchumi, na maisha endelevu kwa wote.

Baada ya mafunzo haya, wanajamii wataibua vipaumbele vya changamoto zinazowakumba na watajadili namna ya kukabiliana nazo wakiwa na viongozi wa serikali ngazi ya wilaya,kata na vijiji.

Mwisho TGNP itaendesha warsha  kwa wanajamii namna ya kuanzisha  na kusimamia vituo vya taarifa na maarifa katika wilaya zao ikiwa ni sehemu ya kukutana na kushirikishana uzoefu na kujadili masuala  mbali mbali zinazowakabili.
 Imetolewa na

Usu Mallya
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP

WACHAWI WAWILI WANASWA LIVE MWANZA

 
Wao wanasema kuwa walipewa amri na wakuu wao (ambapo hawakuwataja jina) kuwachukuwa watu watatu wa kanisa hilo kwa mazingira ya kichawi ili wawauwe kwaajili ya kafara na mazindiko.
Kwa mujibu wa wataalamu wa imani za kichawi mwanamke alisafiri kwa kutumia ungo na mwanaume akatumia mkuki na pembe.

Hakuna kesi inayowakabili watu hao kwani kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hakuna kipengele kinacho utambua uchawi.
Mchungaji wa kanisa la Ufunua Diana Bandele (kushoto) na Abigaili Zumaridi ambaye ni nabii wa kanisa hilo ambao waliwakuta wachawi hao kanisani mwao majira ya saa 12 kwani muda huo ni ada kwa wao kujitakasa kwaajili ya kuianza siku ya ibada. 

PICHA ZOTE NI KWA HISANI YA ALBERT SENGO MZA.

RAIS JAKAYA KWENYE G8 SUMMIT;-

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


RESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tanzania itakua moja ya nchi za mwanzo barani Afrika, kunufaika na mpango wa pamoja wa Kilimo kwa nia ya kuongeza na kulinda usalama wa chakula na lishe kwa watu wake.

Rais Barack Obama wa Marekani ameeleza Leo (18.5.12) katika  hotuba yake ya ufunguzi wa kongamano kuhusu Kilimo na usalama wa chakula (Global Agriculture and Food Security) lililoandaliwa na kituo cha Masuala ya Kimataifa, Chicago Council on Global Affairs jijini Washington.

"Nimeona kuwa kuna umuhimu pia wa kuangalia changamoto zinazoikabili dunia, changamoto ya usalama wa chakula, tutatangaza ushirikiano mpya na nchi tatu zitakua za mwanzo kuanza ushirikiano huu ambao tutatangaza kwenye kushughulikia usalama wa chakula" Rais Obama amesema hayo mbele ya viongozi wa Afrika, ambao nchi zao zitakua za mwanzo kunufaika na uhusiano huo ambazo ni Ethiopia, Ghana naTanzania.

Rais Obama amesema ushirikiano huu mpya utatangazwa rasmi katika Kikao cha Nchi 8 tajiri zenye viwanda duniani maarufu kama G8 unaofanyika tarehe 19 May, 2012 katika makazi ya kupumzikia Rais wa Marekani na wageni wake maarufu kama Camp David.

Kikao hicho cha nchi tajiri duniani kimeweka katika agenda yake swala la chakula duniani kutokana na umuhimu wake katika kipindi hiki.

“Tumeliweka suala la kupiga vita njaa, Marekani ina wajibu wa kupiga vita njaa na pia suala la usalama wa chakula ni suala la kiuchumi" amesema na kuelezea kuwa Bara la Afrika linaweza kujitosheleza kwa chakula na pia katika kuuza nchi za nje.

Ushirikiano huu utakaotangazwa na Nchi 8 tajiri utahusisha serikali, watu binafsi na wafadhili ambapo mwito umetolewa kwa nchi tajiri kutimiza ahadi zao.
Kikao cha kila mwaka cha Nchi 8 tajiri zenye viwanda duniani ambazo ni Canada, ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan na Urusi, zingine ni Uingereza na Marekani.

Katika kikao cha mwaka huu, Tanzania imealikwa kuhudhuria kikao hicho kutokana na mpango wake wa Kilimo Kwanza, ambapo nchi tajiri zimeuchukua kama mfano ambapo juhudi na mikakati iliyomo katika Kilimo Kwanza, itatumika na kuendeleza nchi zingine barani Afrika.

Rais Obama amesema nchi hizi tatu za kwanza zimechaguliwa kunufaika na ushirikiano huu kwa vile zimeonyesha kufikia katika Kilimo na usalama wa chakula.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, tayari yuko jijini Washington kuhudhuria kikao hicho ambapo anategemewa kuelezea matarajio na muelekeo wa Tanzania katika ushirikiano huu.

Akizungumza katika kongamano hilo la siku moja, Rais Kikwete ameelezea umuhimu wa ushirikiano huu unaohusisha serikali, wafanya biasharabinafsi na wafadhili.

"Tunahitaji msaada zaidi katika Kilimo na pia Kilimo hakiwezi kuachwa kwenye mikono ya serikali na wafadhili peke yake, hata Sekta binafsi ina mchango mkubwa" amesema na kuelezea kuwa amefarijika sana, ana matumaini na anategemea yanayozungumzwa yatatimizwa"

Mkutano wa G8 pia utahudhuriwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, ambapo Mwenyekiti wake, Rais Yayi Boni wa Benin anatarajia kuhudhuria pamoja na Rais  John Mills wa Ghana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi.

Rais Kikwete ataondoka Marekani Jumapili usiku kurudi Dar-es-Salaam.




CHELSEA YANYAKUA UBINGWA ULAYA;-


Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 1-1 baada ya dakika 90 za kawaida na kulazimika kwenda katika dakika za nyongeza. Hata hivyo timu hizo ziliendelea kuwa sare na hivyo kulazimika kuamiliwa kwa mikwaju ya penati.

Awali, Thomas Muller alindika bao la kwanza kwa Bayern Munich katika dakika ya 83, lakini Didier Drogba alisawazisha kwa mpira wa kichwa katika dakika ya 88.

Mchezo uliendelea katika muda wa ziada na dakika nne za kipindi cha kwanza Drogba alimfanyia faulo Frank Ribery ndani ya eneo la hatari na kusababisha penati. Arjen Robben alipiga penati hiyo lakini ilidakwa na kipa Petr Cech.

Thursday 17 May 2012

KATIBU w' CHADEMA ANAYEDAIWA KUMNG'OA SIKIO MWANANCHI AMPA SIKU 14 MKUU WA MKOA WA MWANZA KUMTAKASA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

 PICHA HII IKIMWONESHA MLALAMIKAJI ALIPOINGIA OFISI KWA MKUU WA MKOA.

Abel mwesa amesema iwapo mkuu wa mkoa hatofanya hivyo kwa muda uliotajwa atamfungulia mashitaka ya udhalilishaji. Tarehe 14 kijana Lazaro Robert alifika katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Mwanza kutoa taarifa za kung'atwa na kiongozi huyo wa CHADEMA akililaumu jeshi la polisi kushindwa kumtia nguvuni mtuhumiwa. Kutokana na madai hayo mkuu wa mkoa wa Mwanza alitoa agizo kwa polisi kumkamata mtuhumiwa wa tukio hilo ambaye aliwekwa rumande kwa siku 2

Nae Lazaro Norbet amesisitiza kufanyiwa kitendo hicho na katibu huyo wa CHADEMA wilaya ya Ilemela akisema kuwa maelezo yake ya awali yalitofautianana na kumtaja mtu mwingine kutokana na mikwara aliyopigwa kwamba iwapo atamtaja katibu huyo kuhusika basi chamoto atakiona.

Katika hatua nyingine akizungumza na vyombo vya habari jana katika ofisi Kuu ya CCM Mkoa wa Mwanza Katibu wa siasa Itikadi na Uenezi Bw. Saimon Mangelepaa amesema kuwa CCM imesikitishwa na kitendo cha kiongozi wa juu (KATIBU) wa Wilaya ya Ilemela cha kujichukulia sheria mkononi na kumfanyia kitendo cha unyama kijana Nolbert kitendo ambacho hakina budi kulaaniwa na wananchi bila kujali tofauti za kisiasa zilizopo kwa vile ni kitendo cha kinyama kwa jamii na kimeonyesha kiongozi huyo hatambui wajibu wake kwa kuvunja sheria na kujichukulia uamuzi wake binafisi ambao umemsababishia kijana huyu ulemavu wa kudumu.

WAZIRI KAGASHEKI ATEUA WAJUMBE WA BODI YA USHAURI;-


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
BODI YA USHAURI YA WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA (TFS) YATEULIWA
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi Khamisi S. Kagasheki (Mb) kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali (Executive Agencies Act) Sura 245 amewateua wajumbe saba (7) kuunda Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (Tanzania Forest Service - TFS). Aidha, Waziri Kagasheki amemteua Bibi. Ester Mkwizu kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo.
Wajumbe wa Bodi hiyo ya Wakala wa Huduma za Misitu ni kama ifuatavyo:-
1. Bibi. Esther Mkwizu –  Mwenyekiti, kutoka Sekta Binafsi (Tanzania Private Sector Foundation), Dar es Salaam;
2. Bibi. Gladness Mkamba - wa Wizara ya Maliasili na Utalii;
3. Eng. Bonaventura T. Baya –  wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC);
4. Bw. Sosthenes Sambua -  wa Dar es Salaam;
5. Prof. Yonika Ngaga -  wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Morogoro;
6. Dkt. Himid Majamba -  wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam - Sheria; na
7. Bw. Rawson Yonazi – wa Dar es Salaam.
Uteuzi wa Bodi hiyo ni kwa kipindi cha miaka mitatu (3) tangu tarehe 1 Desemba 2011 hadi 30 Novemba 2014.
George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
17 Mei 2012

PATRICK MAFISANGO WA SIMBA SC AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI;-

Mchezaji wa Simba na timu ya Taifa ya Rwanda kiungo mkabaji Patrick Mafisango amefariki dunia kwa ajali ya gari leo alfajiri katika eneo la Tazara jijini Dar es salaam.


Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Simba bwana Aden Rage amesema kuwa taarifa za awali juu ya chanzo cha kifo cha mchezaji huyo zinasema kuwa mchezaji huyo amekutwa na mauti akiwa anaendesha gari na kujaribu kumkwepa mwendesha pikipiki.

Msiba huu unakuja wakati kocha wa timu ya Taifa ya Rwanda Milutin Sredovic 'Micho' akiwa amemteuwa kepteni wa zamani wa timu hiyo Hamada Ndikumana a.k.a 'Katauti' na Patrick Mafisango kujiunga na timu ya taifa hilo (AMAVUBI) kwaajili ya maandalizi ya nchi zitakazofuzu kwenda Brazil kwenye michuano ya Kombe la dunia 2014.

Kabla ya  kuichezea Simba mchezaji huyo alitokea Azam Fc ya jijini Dar es salaam.
Patrick Mafisango is dead.

Muweza twakuomba uilaze roho ya marehemu Patrick Mafisango kulingana na maamuzi yako japo tunashauri umlaze pema peponi, Jah rasta farie.