MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday 27 May 2012

BALOZI WA KWANZA TANZANIA KATIKA UMOJA WA MATAIFA AZIKWA RASMI MKOANI KAGERA

Mazishi ya Balozi wa kwanza wa Tanganyika Huru katika Umoja wa Mataifa- UN, Dk  KYARUZI VEDAST KYALAKISHAIJA, yamefanyika leo,  katika kijiji cha  Kasambya wilayani Misenyi mkoani Kagera.


Misa ya mazishi hayo imeongozwa na Askofu wa jimbo kuu la Bukoba Mhashamu NESTORIUS TIMANYWA.


Dk KYARUZI, alifariki jumapili Mei 20, mwaka huu akiwa na umri wa miaka 92, baada ya kulazwa katika hospitali ya rufaa ya Bukoba.

Dr KYARUZI atakumbukwa na wengi, kwa mchango wake mkubwa kwa taifa la Tanganyika, kabla ya Uhuru,  na TANZANIA, baada ya Uhuru.

Wakati wa Uhai wake, Dr KYARUZI, alilitumikia taifa kwa uaminifu mkubwa katika nyanja mbalimbali, kama Mwana diplomasia na Msomi wa fani ya Udaktari.
Alizaliwa Februari 21, 1921 kijijini KIGARAMA, Kanyigo, Kiziba. Alipata elimu yake ya Msingi katika shule za Kashasha, Mugana na Kajunguti, kabla ya kujiunga na Shule ya St Mary’s Tabora kwa masomo ya Sekondari.

Kati ya mwaka 1942 hadi 1948 alikuwa Chuo Kikuu cha Makerere, ambapo alihitimu kwa kupata shahada ya Udakatari, akiwa miongoni mwa Watanzania wa kwanza kupata nafasi hiyo.

Akiwa Makerere, Dr KYARUZI alikutana na Baba wa Taifa, marehemu Mwl JULIUS KAMBARAGE NYERERE, ambapo walianzisha tawi la Tanganyika African Association-TAA.
                           
                                             WATOTO WA MAREHEMU

                               




                            
                                  SAFARI YA MWISHO KWA DOKTA IMEFIKIA HAPA
                           

                           Ameacha mjane na watoto na wajukuu.

No comments: