MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Saturday 31 October 2015

MATOKEO DARASA LA SABA 2015 YOTE YAKO HAPA

MATOKEO YOTE HAPA, BOFYA MKOA WAKO KUSOMA KILA SHULE

BREAKING NEWS!!! NDEGE YAANGUKA NA WATU 200

Taarifa inasema kuwa ndege hiyo ni ya Russian Airline, iliyoanguka katikati mwa Sinai ikiwa na watu 200, kwa mujibu w taarifa iliyothibitishwa na ofisi ya waziri mkuu wa Misri.

The Airbus A-321 had just taken off from the Red Sea resort of Sharm el-Sheikh, on its way to the Russian city of St Petersburg.
Egyptian media reports said wreckage of the plane had already been found and at least 20 ambulances sent to the scene.
Most of the passengers are said to be Russian tourists.

The plane was operated by the small Russian airline Kogalymavia, based in western Siberia. Latest reports say it was carrying 217 passengers and seven crew.

Initially there were conflicting reports about the fate of the plane, some suggesting it had disappeared over Cyprus.

But the office of Egyptian Prime Minister Sharif Ismail confirmed in a statement that a "Russian civilian plane... crashed in the central Sinai".

It added that Mr Ismail had formed a crisis committee to deal with the crash.

The Russian aviation authority Rosaviatsiya said in a statement that flight 7K 9268 left Sharm el-Sheikh at 06:51 Moscow time (03:51 GMT) and had been due into St Petersburg's Pulkovo airport at 12:10.

The authority added that the aircraft failed to make scheduled contact with Cyprus air traffic control 23 minutes after take-off and disappeared from the radar.

A centre to help relatives of the passengers has been set up at Pulkovo airport, Tass news agency quoted St Peterburg city officials as saying.
Na Mwanaharakati.

Friday 30 October 2015

Thursday 29 October 2015

HALI YA EDWARD LOWASA BAADA YA MAGUFULI KUSHINDA URAIS

Muda mfupi baada ya kutangazwa matokeo ya urais kuonesha kuwa Dr John Magufuli  amemshinda  Lowasa kwa zaidi ya 18%, taarifa inayoonekana kwenye mitandao kijamii ikionesha kutolewa na aliyekuwa mgombea urais kupitia UKAWA, inasema tumewasilisha malalamiko juu ya mchakato ulivyokwenda katika uchaguzi mkuuu.

Sheria inasema kuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi akishatangaza mshindi katika nafasi ya rais hairuhusiwi kufungua kesi mahakamani.

Na Mwanaharakati.

MWENYEKITIKI WA NEC AKITANGAZA MATOKEO YA URAIS 2015

Matokeo yametangazwa katika ukumbi wa mwalimu Nyerere katika kituo maalumu cha NEC huku vyama 6 vikisaini kati ya 8 vilivyokuwa kwenye kinyag'anyiro, ambapo mwakili wa CHADEMA  hakuudhulia, na mwakilishi wa CHAUMA amekataa kusaini jambo ambalo mwenyekiti Jaj mstaafu Damian Lubuva anasema sheria inaruhusu kutangaza matokeo na hana lazima chama kusaini au kutosaini.
Na Mwanaharakati.

CV YA DR. MAGUFULI RAIS WA AWAMU YA TANO TANZANIA

Dk. John Pombe Joseph Magufuli, alizaliwa Oktoba 29, 1959 wilayani Chato – wakati huo ikiwa Mkoa wa Kagera (sasa Mkoa wa Geita).
Ana Shahada ya Uzamivu ya Kemia (2006 – 2009) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mwaka 1991 – 1994, alisoma Shahada ya Uzamili (Kemia) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na baadaye Chuo Kikuu cha Salfordnchini Uingereza.
Mwaka 1985 – 1988, alisoma Shahada ya Kwanzaya Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.
Mwaka 1981 – 1982, alisoma diploma katika Chuo cha Mkwawa akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.
Mwaka 1979 – 1981, alipata elimu ya juu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Mkwawa, Iringa.
Mwaka 1977 – 1978, alisoma elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Lake, Mwanza.
Mwaka 1975 – 1977, alisoma Shule ya Msingi Katoke, Biharamulo mkoani Kagera.
Mwaka 1967 – 1974, alisoma Shule ya Msingi, Chato.
Mafunzo
Machi 1984 – Juni 1984 alihudhuria mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mpwapwa mkoani Dodoma.
Januari 1984 – Machi 1984 alikuwa JKT Makuyuni, Arusha.
Julai 1983 – Desemba 1983 alikuwa JKT Makutupora, Dodoma.
Uzoefu wa kazi
Mwaka 2010 – hadi sasa: Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Chato.
Mwaka 2008 – 2010: Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Samaki; Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato).
Mwaka 2005 – 2008: Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato)
Mwaka 2000 – 2005: Waziri wa Ujenzi, na Mbunge wa Biharamulo Mashariki.
Mwaka 1995 – 2000: Naibu Waziri wa Ujenzi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki.
Mwaka 1989 – 1995: Mkemia Chama cha Ushirika cha Nyanza Cooperative Union (Ltd.), Mwanza.
Mwaka 1982 – 1983: Mwalimu Shule ya Sekondari Sengerema (akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati).
Dk. Magufuli amepata tuzo mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
Ameshiriki na kuongoza mikutano mingi ya kitaifa na kimataifa.
Ameandika vitabu na majarida mbalimbali. Ameoa na ana watoto kadhaa.

GENERAL
Salutation Hon. Member picture
First Name: Dr. John
Middle Name: Pombe Joseph
Last Name: Magufuli
Member Type: Elected Member
Constituent: Chato
Political Party: Chama Cha Mapinduzi
Office Location: P.O. Box 9144, Dar es Salaam
Office Phone: +255 713 322 272/+255 754 292 580 Office Fax: + 255 222124505
Office E-mail: jmagufuli@parliament.go.tz
Member Status: Active
Date of Birth 29 October 1959
EDUCATION
School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
Chato Primary School CPEE 1967 1984 Primary School
Katoke Seminary Biharamulo, Kagera CSEE 1975 1977 Secondary School
Mkwawa High School ACSEE 1979 1981 Secondary School
Lake Secondary School ¿ Mwanza CSEE 1977 1978 Secondary School
Mkwawa College of Education Diploma in Education (Sc.) Chem., Maths&Edu. 1981 1982 Diploma
University of Dar es Salaam B.Sc Ed. (Hons) Chem.&Maths 1985 1988 Bachelor
Universities of Dar es Salaam, TZ &Salford -U.K. MSc. (Chem) 1991 1994 Masters Degree
University of Dar es Salaam. PhD (Chem) 2006 2009 PhD
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From To
UN-HABITAT Co-chair World Urban Forum (III) 2006 To Date
Ministry of Lands and Human Settlements Minister 2005 2/8/2008
World Road Congress (PIARC) 1st Delegate 2000 2005
Mtwara Development Corridor Member 2000 2005
Ministry of Works Minister 2000 2005
Ministry of Works Deputy Minister 1995 2000
Tanzania Chemical Society Member 1993 Todate
Nyanza Co-operative Union(NCU) Ltd.- Mwanza. Industrial Chemist 1989 1995
Sengerema Secondary School Teacher(Chemistry and Mathematics) 1982 1983
Ministry of Livestock and Fisheries Development Minister 13/02/2008 To Date
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location Position From To
Chama Cha Mapinduzi - CCM( Biharamulo East) Member of Parliament of Tanzania 1995 Todate
Chama Cha Mapinduzi - CCM Member 1977 Todate












Na Mwanaharakati.

MAAJABU; DR. JOHN POMBE MAGUFULI-ASHINDA URAIS SIKU YA KUZALIWA, SOMA HISTORIA YAKE

Alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1959 wilayani Chato Mkoani Kagera.
Kielimu, daktari Magufuli ana Stashahada ya elimu ya sayansi akibobea kwenye masomo ya Kemia, Hisabati.

Mgombea huyo wa urais ana shahada ya umahiri wa Sayansi na shahada ya uzamivu ya kemia.
Aidha daktari Magufuli amewahi kufundisha katika shule ya sekondari Sengerema miaka ya themanini kisha akajiunga na mafunzo ya JKT .

Alipohitimu, daktari Magufuli na aliaanza kufanya kazi katika kiwanda cha ‘Nyanza Cooperative Union akiwa Mkemia kabla ya kuondoka hapo na kuwania ubunge.

Magufuli alianza mbio za ubunge mwaka 1995 katika jimbo la Chato na kushinda kisha akateuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuwa naibu waziri wa Miundombinu.

Katika uchaguzi wa Mwaka wa 2000 pia aligombea ubunge na kushinda na Rais Mkapa akamteua kuwa Waziri wa miundombinu.

Alianza siasa mwaka 1995
Katika uchaguzi wa mwaka 2005 daktari Magufuli aligombea ubunge kwa mara ya tatu na kupita bila kupingwa.

Rais Kikwete alimteua kuongoza wizara ya Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi na baadaye akamhamishia hadi wizara ya Mifugo na uvuvi.

Mwaka 2010 alichaguliwa kuwa mbunge kwa mara ya nne na Rais Kikwete alimrudisha katika Wizara ya Miundombinu na ujenzi.

Daktari Magufuli anachukuliwa kuwa ni mwanasiasa mwenye msimamo thabiti, mchapa kazi na asiye yumbishwa au hata kufuata upepo wa kisaisa.

Anatambulika kuwa Mchapa kazi
Watanzaniania wanamkumbuka kwa usimamizi na ujenzi wa barabara na majengo thabiti.
Anakumbukwa kwa kuchukua hatua za kutoa amri za kubomolewa kwa majengo ya kifahari ambayo alihisi yalikiuka sheria za ujenzi.

Daktari John Magufuli, alisajili asilimia 87 % ya kura za wajumbe, hiyo ikiwa ni kura 2104.
Daktari John Magufuli, aliwashinda wapinzani wake Bi Amina Salulm Ali na dakta Asha-Rose Migiro, ingawaje itakumbukwa kuwa alikuwa katika kinyang'anyiro cha wagombea wa maoni zaidi ya 40.

Leo EC imemtangaza kama mshindi wa kiti cha urais kwa kura 8,882,935 sawa na 58.46% dhidi ya mshindani wake kupitia muungano wa UKAWA Edward Lowasa aliyepata kura 6,072,848 ambayo ni sawa na 39.97%

Na Mwanaharakati.

Sunday 25 October 2015

MATUKIO MAZITO NA PICHA YA UPIGAJI KURA BUKOBA





Wapiga kura katika manispaa ya Bukoba, wamejitokeza kwa wingi katika Vituo vya kupigia kura, kwa ajili ya kuwachagua Viongozi wanaowataka, kuanzia rais, mbunge na Madiwani,  licha ya dosari kadhaa zilizojitokeza.

Katika kata mbalimbali za manispaa ya Bukoba, wananchi wamejitokeza kwa wingi tangu Asubuhi na mapema na kujipanga katika mistari, kulingana na utaratibu ulioelekezwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini -NEC-.

Mgombea wa ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi CCM , jimbo la Bukoba mjini Balozi KHAMIS KAGASHEKI amepiga kura yake katika kituo cha National  Housing na kuelezea kuridhishwa kwake mwenendo wa upigaji kura.
 
Mkuu wa mkoa wa Kagera, JOHN MONGELA amepiga kura yake, katika Kituo cha Uwanja wa Ndege katika kata ya Miembeni na kuwahakikishia wananchi kwamba ulinzi kuwa umeimarishwa.

Amesema uandikishaji huoumeanza kwa wakati, ingawa kuna taarifa za baadhi ya vituo kuchelewa kufunguliwa kutokana na sababu mbalimbali.

Amesema kuwa katika baadhi ya vituo changamoto zilizopo ni za kawaida ikiwemo mawakala wa vyama kuchelewa pamoja na wasimamizi kuchelewa katika kupanga vifaa vya kupigia kura.

Bwana MONGELA ameonya kuwa mtu atakayejaribu kutaka kuvuruga amani katika kipindi hiki, Vyombo vya Ulinzi na Usalama, vitamchukulia hatua stahiki ili kuhakikisha Uchaguzi unakamilika salama.

Katika wilaya za Karagwe, Muleba na Missenyi, Bukoba Vijijini, taarifa zinasema kuwa upigaji wa kura unaendelea vizuri, licha ya baadhi ya Wasimamizi wa Vituo kuwa na kasi ndogo.

Taarifa hizo zinasema kuwa wananchi wamejitokeza kwa wingi kutekeleza haki yao ya kikatiba, licha ya baadhi ya watu hususan wazee kupata shida wakati wa kutafuta majina yao baada ya vituo kugawanywa.

Wapiga kura Elfu 71 na 600 katika manispaa ya Bukoba, wanatarajiwa  kupiga kura katika uchaguzi mkuu unaendelea kote nchini, huku hali ya ulinzi na usalama ikiwa imeimarishwa kuhakikisha wananchi wenye sifa wa wanatekeleza haki yao kikatiba.

Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi  jimbo la Bukoba Mjini, ABDON  KAHWA   amesema kuwa Vituo  177  vinatumika  kupiga kura  katika  Kata  zote   14  za manispaa ya Bukoba.
 

Na Mwanaharakati.

Thursday 22 October 2015

BREAKING NEWS!!!VIONGOZI WA DINI HAWAKO TAYARI KUONA WANASIASA WANAUA WAUMINI BUKOBA



. Ni katika kikao maalumu cha ulinzi na usalama,
. Wasema na wao siasa wanaziweza ila wanafanya kazi ya Mungu,
. Baadhi ya wanasiasa CHADEMA kulazimisha wananchi kukaa mita 200.

Viongozi wa vyama vya siasa wametakiwa kuacha mara moja kuchochea wananchama wao kuleta vurugu wakati wa uchaguzi mkuu.

Hatahivyo wametakiwa kutambua kuwa  wanachama hao ndiyo waumini wa kanisa na misikiti, hivyo ghasia zitahatarisha siyo wanasiasa pekee kwani wanahitajika sehemu zote husika, dini na siasa.

Msaidizi wa askofu katika kanisa la Anglikan Canon Elisha Bililiza, amesema kuwa
viongozi wa dini nao wanaweza kufanya siasa, kufanya kazi ya ulinzi na sasa wanafanya kazi za kuhubiri waumini ambao hatahivyo ndiyo wanachama wa vyama vinavyoongozwa na wanasiasa, ambao baadhi yao wanawahamasisha wakae vituoni kulinda kura, jambo ambalo ni kinyume na sheria za nchi.



Hatahivyo makatibu wa vyama, akiwamo Sadick Amzakatibu  NCCR Mageuzi, Francis
Batu wa CUF na TLP, wamesema kuwa hawakotayari kuona wapiga kura wanasalia vituoni, kwani wanatambua utaratibu wan chi hauruhusu na hawataki kuwa chanzo cha kuondoa amani iliyodumu kwa miaka yote Tanzania.





Mkutano huo maalumu, umeitishwa na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo Bwana Jackson Msome, kwa kuwashirikisha viongozi wa dini, viongozi wa siasa na kamati nzima ya ulinzi na usalama pamoja na waandishi wa habari.

Na Mwanaharakati.

Tuesday 20 October 2015

MASIKITIKO; ULEMAVU WA UTATA MUHUSIKA AFICHWA NA KUTELEKEZWA



Shakira Abdallah mwenye umri wa miaka 24 ametelekezwa na mume wake kwa miaka minne baada ya kupata ulemavu wa viungo na hatimaye kushindwa kuongea.  

Mtandao huu umefanya mazungumzo na babu wa Shakira,  mzee Hamis Waziri anasema
kuwa katika kipindi chote cha uzima wa mjukuu wake alikuwa akiongea nae mara kwa mara kwa njia ya simu ili kujua hali yake na baadae mawasilainao ya kuongea yakashindikana, jambo lililowafanya washtuke walipoona ukimya ambao awali haukuwepo.



Sikiliza simulizi ya babu wa Shakira kama alivyozungumza na mtandao huu…


"Mama yake na bibi waliamua kuuza shamba na kufunga safari ili kumjulia hali mjukuu wao ambaye wakati huo alikuwa ameshalemaa na alikuwa hawezi tena kuongea.

Anasema kuwa mjukuu wake alichukuliwa kutoka Mtwara kwenda Dar na rafiki wa mama yake aliyekuwa akiishi jirani yao aliyejukana na kwa jina la Ashura kwa muda wa miezi sita hadi na kufanikiwa kupata mchumba aliyemuoa kwa ridhaa ya mjomba yake aishie.  

Waziri anasema kuwa kitendo cha mjukuu wake kupata ulemavu bila wao kujua ilikuwa ni pigo kubwa kwa familia  nzima kwakuwa mume wake alimteyekeza bila kumpatia huduma yoyote.  

“Mimba yake ilipofika miezi nane alikuwa akitupigia simu na kusema kuwa akiwa chumbani kwake anaona vitu vya ajabu ajabu hali ambayo ilitulazimu kumuomba mume wake amlete ili aweze kujifungulia huku lakini alikataa.

“Mjukuu wetu anateseka sana ukimuona huwezi amini kama alizaliwa akiwa mzima akawa anatembea na kuongea kitendo alichofanyiwa sio kitendo cha ubinadamu tunaomba serikali itusaidie ili aweze kupata stahiki zake kwakuwa hakupewa talaka na mume wake” alisema Waziri

 
Na Mwanaharakati.