Wapiga kura katika manispaa ya Bukoba, wamejitokeza kwa wingi katika Vituo vya kupigia kura, kwa ajili ya kuwachagua Viongozi wanaowataka, kuanzia rais, mbunge na Madiwani, licha ya dosari kadhaa zilizojitokeza.
Katika kata mbalimbali za manispaa ya Bukoba, wananchi wamejitokeza kwa wingi tangu Asubuhi na mapema na kujipanga katika mistari, kulingana na utaratibu ulioelekezwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini -NEC-.
Mgombea wa ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi CCM , jimbo la Bukoba mjini Balozi KHAMIS KAGASHEKI amepiga kura yake katika kituo cha National Housing na kuelezea kuridhishwa kwake mwenendo wa upigaji kura.
Mkuu
wa mkoa wa Kagera, JOHN MONGELA amepiga kura yake, katika Kituo cha Uwanja wa
Ndege katika kata ya Miembeni na kuwahakikishia wananchi kwamba ulinzi kuwa
umeimarishwa.
Amesema
uandikishaji huoumeanza kwa wakati, ingawa kuna taarifa za baadhi ya vituo
kuchelewa kufunguliwa kutokana na sababu mbalimbali.
Amesema
kuwa katika baadhi ya vituo changamoto zilizopo ni za kawaida ikiwemo mawakala
wa vyama kuchelewa pamoja na wasimamizi kuchelewa katika kupanga vifaa vya
kupigia kura.
Bwana
MONGELA ameonya kuwa mtu atakayejaribu kutaka kuvuruga amani katika kipindi
hiki, Vyombo vya Ulinzi na Usalama, vitamchukulia hatua stahiki ili kuhakikisha
Uchaguzi unakamilika salama.
Katika
wilaya za Karagwe, Muleba na Missenyi, Bukoba Vijijini, taarifa zinasema kuwa
upigaji wa kura unaendelea vizuri, licha ya baadhi ya Wasimamizi wa Vituo kuwa
na kasi ndogo.
Taarifa
hizo zinasema kuwa wananchi wamejitokeza kwa wingi kutekeleza haki yao ya
kikatiba, licha ya baadhi ya watu hususan wazee kupata shida wakati wa kutafuta
majina yao baada ya vituo kugawanywa.
Wapiga
kura Elfu 71 na 600 katika manispaa ya Bukoba, wanatarajiwa kupiga kura katika uchaguzi mkuu unaendelea
kote nchini, huku hali ya ulinzi na usalama ikiwa imeimarishwa kuhakikisha
wananchi wenye sifa wa wanatekeleza haki yao kikatiba.
Msimamizi
Msaidizi wa Uchaguzi jimbo la Bukoba
Mjini, ABDON KAHWA amesema kuwa Vituo 177
vinatumika kupiga kura katika
Kata zote 14 za
manispaa ya Bukoba.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment