MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday 27 September 2015

TAARIFA MPYA KAMILI UCHOMAJI MAKANISA SASA NI BUKOBA VIJIJINI

Ni makanisa mengine matatu ya Rc, na KKKT mawili ambapo taarifa inasema kuwa kanisa la Romani katoliki kigango cha Kiijongo kata Katoro, na makanisa ya kata Kaibanja na la kitongoji cha Musila kata Katoro Bukoba vijijini.

Kamanda wa polisi mkoani Kagera Augustine Ollomi amesema kuwa watu wasiofahamika wamevamia makanisa hayo na kukusanya vifaa kama biblia, bahasha za sadaka, majoho na ngoma na kuvichoma moto.

Amewasihi waamini, viongozi wa dini na wananchi, kutoa ushirikiano kwa mamlaka, ili wafanikishe kukamata wahusika.

September 22 mwaka huu, makanisa matatu ya kipentekoste katika manispaa ya Bukoba, yalichomwa moto na kusababisha hasara ya shilingi milioni 12.9.

Na Mwanaharakati.

Friday 25 September 2015

WATANZANIA KADHAA WAMEPOTEZA MAISHA KWENYE HIJA

Taarifa kutokwa kwa.  Shekh Khalid Mohamed Mrisho akiwa huko Mina inasema kuwa watanzania 6 kutoka Tanzania wamefariki katika hija hiyo ilhali wengine kadhaa wamejeruhiwa wanaendelea na matibabu.

Ameeleza kuwa waliopoteza maisha watazikwa hukohuko pamoja na wengine zaidi ya 700, huku akisema mamlaka zitafanya taratibu za kuwafahamisha wafiwa.
Na Mwanaharakati.

Thursday 24 September 2015

KIFO CHA WAZIRI CELINA KOMBANI SOMA HAPA

Taarifa zilizoufikia mtandao huu zinasema kuwa mh. Kombani aliyekuwa waziri wa nchi ofisi ya rais utumishi wa umma, amefariki huko India ambapo taarifa zaidi zitatolewa na mamlaka kuhusu tatizo lililomsibu.

Bi.Celina Kombani, alikuwa Mbunge aliyemaliza muda wake katika jimbo LA Ulanga mashariki mkoani Morogoro, na alikuwa akigombea tena nafasi hiyo.
Na Mwanaharakati.

SURA MPYA UCHOMAJI MAKANISA, SERIKALI KAGERA YAINGILIA KATI.



. Viongozi wa makanisa hayo kuwa washirika namba moja,
. Umoja wa makanisa ya Kipentekoste wahitaji mwongozo.
Wakati serikali mkoani Kagera, ikikagua makanisa hayo na wahakikishia wachungaji na waamini wa makanisa yaliyochomwa moto katika manispaa ya Bukoba , wachungaji waomba mwongozo wa aina gani ya makanisa wajenge ili yaheshimiwe.

Akizungumza katika ziara ya kutembelea Makanisa yaliyochomwa moto, mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani  Kagera JOHN MONGELA, amesema kuwa tayari polisi imeanza kuwatafuta waliohusika na matukio hayo.

Bwana MONGELA ambaye ni mkuu wa mkoa wa Kagera, amesema kuwa kwa nchi kama Tanzania,  vitendo hivyo vinatakiwa kukemewa na kuwaomba wachungaji kuwa wavumilivu katika kipindi hiki,  ambacho serikali inaendelea kulishughulikia.
Mwenyekiti wa makanisa ya Kipentekoste –PCCT-,  mchungaji CRODWARD EDWARD ameishukuru serikali ya mkoa kwa jinsi inavyoendelea kulishughulikia.
Mchungaji EDWARD amesema kuwa kutokana na makanisa hayo kuwa yanachomwa moto, wameaanza kupoteza imani na serikali lakini kutembelewa na mkuu wa mkoa sasa wana imani suala hilo litashughulikiwa.

Na Mwanaharakati.

VIFO VIPYA ZAIDI YA 200 KWA MAHUJAJI MECCA



Watu 220 waliokuwa wakishiriki sherehe za hija wamefariki kwenye mkanyagano uliotokea katika mji mtakatifu wa Kiislamu wa Mecca, maafisa nchini Saudi Arabia wamesema.
Idara ya ulinzi wa raia nchini humo imesema kupitia Twitter kwamba watu wengine 450 wamejeruhiwa katika kisa hicho kilichotokea mji wa Mina, takriban kilomita tano kutoka mji wa Mecca.
Shughuli za uokoaji zinaendelea, idara hiyo imeongeza.
Mkanyagano huo umetokea siku ya kwanza ya sherehe za Eid al-Adha.
 

Na Mwanaharakati.

Sunday 20 September 2015

TAARIFA YA MGOMBEA WA CCM ALIYEKUFA KWA AJALI KAGERA

Taarifa za awali zinasemakuwa amepata ajali ya pikipiki mchana wa leo akiwa katika shughuli zake za kila siku.

Ni mgombea udiwani Muleba mjini kupitia tiketi ya CCM ambaye hatahivyo kabla ya umauti alihutubia wananchi katika mkutano wa kampeini mjini Muleba.

Taarifa zaidiitakujia hapa.
Na Mwanaharakati.

Friday 18 September 2015

MAKUBWA MKUTANO WA CCM KAHORORO SAUTI HIZI HAPA



. Waliohama vyama waulizwe wayasemayo wangeyasema?
. Watakiwa kumwogopa Mungu waseme ukweli,
. WanaCHADEMA waenda CCM.
Ni mkutano wa mgombea udiwani katika kata ya Kahororo manispaa ya Bukoba, ambapo makada na baadhi ya waliogombea kuwania ubunge katika kura za maoni, wamesema kuwa wananchi wasidanganywe na maneno yanayotengenezwa na waliohama chama, ili wao waonekane wazuri na wako sahihi, na kuwataka wananchi wawaulize wayasemayo wangekuwa CCM wangeyasema? Mzee Florence Mwakyoma, akasisitiza.
Katibu CCM mkoani Kagera Bw Idd Ame, amesisitiza sula la amani, kuwa vijana wasidanganywe kwa misingi ya viongozi kujitafutia nafasi, huku akisema kuwa mabadiliko yanafanywa na CCM kwa misingi ya chachu ya maendeleo wala siyo ombwe la uongozi kwani waliokuwa wanakwamisha chama chao tayari wameondoka.

Mwenyekiti wa bodi ya maji ambaye pia ni mgombea udiwani kata Kashai Samora
Lyakurwa amesema kuwa hundi ya malipo ya wananchi wanaodai fidia walishasainiwa na wahusika walijulishwa jinisi ya kupata fidia yao, hivyo wanaowadanganya hawana pa kufuatilia suala hilo kwani yeye ndiye muhusika mkuu.






Bwana Mjuni Kataraiya aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Bukoba mjini, ambaye pia alikuwa miongozi
mwa watia nia, amesema kuwa kura zao hazikutosha na hatimaye Kagasheki kupendwa zaidi kutokana na aliyoyafanya hivyo haoni aibu kumwombea kura kwani hakuna wakumshindanisha naye. 













Na Mwanaharakati.

SIKILIZA KAULI NZITO VIONGOZI WA NCCR KUHUSU UKAWA

Ni sauti ya makamu mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Bi. Reticia Ghati Mosore akiambatana na katibu mkuu bara wa chama hicho Bw John Mosena Nyambabe, walipoongea jana na waandishi habari wakiambatana na wanachama wengine ngazi ya juu ya chama chao.
 
Na Mwanaharakati.

Thursday 17 September 2015

NEWS ALERT!!! HATIMA YA NCCR MAGEUZI NDANI YA UKAWA



. Wadai CHADEMA kimepora kila kitu cha UKAWA,
. Chasema kimeamua kupambana chenyewe,
. Wadai wameshindwa kukubaliana na mwenyekiti wao.
Makamu mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Bi. Reticia Ghati Mosore akiambatana na katibu mkuu bara wa chama hicho Bw John Mosena Nyambabe pamoja na viongozi wengine wa juu wa chama hicho, wamesema kuwa wanaamua kupambana kivyao kwa masikitiko makubwa, baada ya kuona muda umeshakuwa mfupi, na hawawezi tena kufaidika na UKAWA kwani maelngo yao yameporwa na CHADEMA.

Wametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kuwasaidia kuwachagua wagombea wao 12 pekee waliopewa na UKAWA, wakisema kuwa hawana namna lakini hawako tayari kuendelea kutegemea UKAWA ambayo sasa imegeuka kuwa CHADEMA, kwani baada ya uchaguzi wameshajiona kama watashinda hawawezi kuthaminika kutokana na mwenendo uliopo sasa, wala wanaona hawawezi kupata nafasi yoyote katika serikali itakayoundwa.
 

Na Mwanaharakati.

Wednesday 16 September 2015

LOWASSA NDANI YA CHATO KWA MAGUFULI

Wakati mgombea urais kupitia CCM John Magufuli akihutubia watanzania waishio Kigoma katika uwanja wa Kawawa mjini humo, Edward Lowassa kupitia CHADEMA ameongea na watanzania waishio Geita katika wilaya ya Chato.

Na Mwanaharakati.

Tuesday 15 September 2015

UTEUZI WAKUU WAPYA WA MIKOA, WAMNUSURU MAKALLA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua wakuu wawili wapya wa mikoa kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wakuu wa Mikoa ambao wanawania ubunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Taarifa iliyotolewa jana Jumatatu, Septemba 14, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa katika uteuzi wake, Rais Kikwete amemteua Ndugu Amos Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Ndugu Jordan Rugimbana kuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi. 

Aidha, Rais Kikwete amewahamisha wakuu wawili wa mikoa – Ndugu Mwantumu Bakari Mahiza aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Ndugu Saidi Magalula ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akitokea Mkoa wa Tanga. Ndugu Magalula anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Stella Manyanya anayewania ubunge mkoani Ruvuma pia. 

Ndugu Makalla ambaye alipata kuwa Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Morogoro na Naibu Waziri wa Maji anachuku anafasi iliyoachwa wazi na ndugu Leonidas Gama ambaye anawania ubunge mkoani Ruvuma. 

Ndugu Rugimbana ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Mahiza.

Uteuzi na uhamisho huo ulianza Jumamosi, Septemba 12, mwaka huu, 2015 na wakuu wapya wa mikoa wataapishwa kesho kutwa Jumatano, Septemba 16, 2015, Ikulu, Dar es Salaam.

Wakati huo huo, Rais Kikwete amemteua Profesa Muhammed Bakari Kambi kuwa Mganga Mkuu wa Serikali. 

Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Septemba 14, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza tokea Jumatano, Septemba 9, 2015. Kabla ya uteuzi wake, Profesa Muhammed Bakari Kambi alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tiba na Afya Shirikishi cha Muhimbili, Dar es Salaam.

Vile vile, Rais Kikwete amemteua Ndugu Mlingi Elisha Mkucha kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC). Uteuzi huo ulianza Jumatano, Septemba 9, mwaka huu, 2015.

Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Septemba 12, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Ikulu, Dar es Salaam imesema kuwa Ndugu Mlingi Elisha Mkucha ni mwanasheria kwa taaluma na mwajiriwa wa NDC kwa miaka 14 iliyopita ambako ametumikia katika nafasi mbali mbali mpaka akawa Kaimu Mtendaji Mkuu.

Ndugu Mkucha anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Gideon Nassari aliyestaafu kwa mujibu wa sheria.

Wakati huo huo, Rais Kikwete amemteua Dkt. Tulia Ackson kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuanzia Jumatano, Septemba 9, mwaka huu, 2015.Kabla ya uteuzi wake, Dkt. Tulia Ackson ni Mhadhiri wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
 14 Septemba, 2015
 

Na Mwanaharakati.