MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Saturday 28 February 2015

GAUNI LA MWIGIZAJI LUPITA NYONG'O LAPATIKANA

Polisi mjini Los Angeles, Marekani, wameweza kulipata lile gauni lilopambwa na lulu, ambalo liliibiwa kutoka chumba cha hoteli cha mchezaji sinema kutoka Kenya, Lupita Nyong'o, ambalo alivaa katika tamasha la Oscars.
Polisi walitomezwa na mtandao wa kijamii, TMZ.
Mtandao huo ulipata simu kutoka kwa mwanamme mmoja ambaye alidai kuwa aliichukua kanzu hiyo na kisha aliirudisha hoteli, baada ya kutambua kuwa lulu 6,000 zilizopambwa juu ya nguo hiyo zilikuwa za uongo.
Hapo awali iliarifiwa kuwa nguo hiyo ilikuwa na thamani ya dola 150,000.

Na Mwanaharakati.

SOMA TAARIFA KUHUSU KIFO CHA MH. JOHN KOMBA



Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, hata hivyo hakuwa tayari kuelezea kwa undani kwa madai kuwa taarifa hizo zimemfikia sasa hivi.

Mmoja wa watoto wa Komba ambaye alijitambulisha kwa jina la Herman amethibitisha kutokea kwa msiba huo na akasema, msiba wa baba yake upo nyumbani kwake Mbezi Tangi Bovu, Dar.

Habari zinasema asubuhi ya leo Komba alikwenda kwenye shughuli zake za kikazi kama kawaida lakini .............

KIFO CHA CAPTAIN JOHN KOMBA

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, hata hivyo hakuwa tayari kuelezea kwa undani kwa madai kuwa taarifa hizo zimemfikia sasa hivi.

Mmoja wa watoto wa Komba ambaye alijitambulisha kwa jina la Herman amethibitisha kutokea kwa msiba huo na akasema, msiba wa baba yake upo nyumbani kwake Mbezi Tangi Bovu, Dar.

Habari zinasema asubuhi ya leo Komba alikwenda kwenye shughuli zake za kikazi kama kawaida lakini
Taarifa zaidi tutakuletea kuhusu kifo hicho cha mbunge wa Mbinga ambacho kimestua watanzania wengi.
Na Mwanaharakati.

Friday 27 February 2015

NDEGE YATEKETEA MWANZA


Taarifa inasema kuwa ni ndege ya jeshi la wananchi JWTZ, ambayo imeanguka katika viwanja vya jeshi wilayani Ilemela mkoani Mwanza, ambapo hakuna aliyepoteza maisha.

Inasemekana ndege hiyo ambayo hatujapata namba yake, imeteketea kabisa, huku rubani aliyekuwa ndani yake amenusurika katika ajali hiyo na hakuna aliyepoteza maisha kwasababu alikuwa pekee kwenye ndege hiyo...................

TAARIFA INASEMA KUWA WASHITAKIWA WA CUF WAMEZIDI POLISI UJANJA

HATI ya kuwafutia mashtaka wafuasi 30 wa Chama cha Wananchi (CUF) waliotakiwa kuunganishwa katika kesi moja na Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahimu Lipumba, imezua sintofahamu baada ya wafuasi hao kutoweka.

Wafuasi hao waliotakiwa kuachiwa na kukamatwa tena walitoweka jana katika.............

BARUA YA KUBOMOA KANISA LA MCHUNGAJI GWAJIMA

Thursday 26 February 2015

JINSI DADA WA AFANDE SELE ALIVYOFIA GEST, SOMA UNDANI WAKE

Dada wa msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, 
Seleman Msindi Afande Sele Zaria Kambi (30) ambaye alikuwa ni mhudumu 
wa baa, amekutwa ameuawa kikatili katika Gesti ya Stavi (Gesti ya 
Marafiki) iliyopo Kichangani, mjini Morogoro.
 
Tukio hilo la kinyama lilitokea usiku wa Jumapili iliyopita baada ya 
marehemu kuwa amekubaliana kulala pamoja na mteja aliyekuwa akimhudumia 
kinywaji, ambaye pia alikuwa amechukua chumba katika nyumba hiyo hiyo 
iliyokuwa na baa.
 
Kwa mujibu wa rafiki wa marehemu, ambaye pia alikuwa ni mhudumu wa 
gesti hiyo, Rehema Saleh, alisema mtu mmoja asiyefahamika, alifika 
kazini kwao na kupanga chumba namba 8A na baadaye alienda upande wa baa 
kunywa pombe akihudumiwa na Zaria.
 
Mimi na Zaria (pichani) tunaishi jirani, sasa baada ya kumhudumia na
 yeye kununuliwa pombe, wakakubaliana walale pamoja, tunaishi jirani 
hivyo kila siku baa ikifungwa tunaongozana na jana tuliongozana njiani 
aliniambia amepata kichwa hivyo anakwenda nyumbani kuaga na baadaye 
arejee kwa bwanake huyo ambaye ni mara ya kwanza anaonana naye, 
alisema Rehema na kuongeza.
 
Cha ajabu saa 8 usiku napigiwa simu na mlinzi akidai Zaria 
amenyongwa na mteja wake, sikuwa na jinsi, kulipokucha nilifika hapa 
gesti na kukuta mwili wa marehemu ukiwa kitandani, alisema na kuangua 
kilio



Mlinzi wa gesti hiyo, John Emmanuel akizungumzia tukio hilo, alisema 
majira ya saa 6 usiku Zaria aliingia katika chumba namba 8A na saa moja 
baadaye, akasikia kelele zikitoka chumbani humo, ambazo alihisi ni za 
kimapenzi
 
Sijakaa vizuri saa 8 usiku jamaa alitoka na begi lake akitaka 
nimfungulie aondoke huku mkononi akiwa na tiketi ya basi kuelekea Mbeya,
 nikamwambia kwanza twende chumbani kwake nikachunguze ndipo nimruhusu 
atoke, awali aligoma na mimi nikagoma kumfungulia geti, tukaganda kama 
dakika mbili akakubali kwenda chumbani tulipofika tukamkuta Zaria 
amekufa huku akiwa mtupu, nikamjulisha bosi Pascal Mafikiri ambaye 
aliita polisi wakamchukua mtuhumiwa na mwili wa Zaria, alisema.
 
Mama mzazi wa marehemu, Mwajuma Hassani Kambi ambaye ni Mjumbe wa 
Serikali ya Mtaa wa Mwande Kata ya Kichangani kwa tiketi ya Chadema 
alipokea taarifa za kifo cha mwanaye Jumapili usiku
 
Alisema mwanaye ameacha mtoto anayeitwa Rashid lsmail Kaliembe ambaye
 anasumbuliwa na uvimbe tumboni na kwamba kila mwezi alikuwa akipelekwa 
Muhimbili kwa matibabu.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo alithibitisha 
kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa, Erick Bruno, ambaye ni mkazi
 wa Manzese Tip Top Dar es Salaam, anashikiliwa. Marehemu huyo alizikwa 
Jumanne iliyopita mjini Morogoro.

Na Mwanaharakati.

WACHEZAJI TAMBWE NA NIYONZIMA WAZUIWA BOTSWANA

Taarifa imeeleza kuwa Amissi Tambwe, Kpah Sherman, Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite kuzuiwa kwa saa moja kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Seretse Khama, mjini Gaborone, Botswana.
Mbrazili Coutinho hakuondoka na wenzake kutokana na kuwa majeruhi wa goti aliloumia katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City mwishoni mwa wiki.
Yanga iliwasili Gaborone saa 4: 35 asubuhi (5:35 kwa saa za Tanzania) na kukutana na kadhia hiyo baada ya wachezaji wake kulazimika kukaa hapo kwa zaidi ya saa wakisubiri suala la wenzao kukamilisha taratibu za uhamiaji.
Wakati wachezaji wakipita katika ukaguzi wa pasi za kusafiria.........

MWANAMUZIKI CHID BENZ AHUKUMIWA LEO

Hatimaye kesi ya mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Rashidi Abdallah Makwaro Maarufu kama (Chid Benzi) imehukumiwa leo na kumfunga kifungo cha miaka miwli jela au kulipa faini ya shingili laki tisa bada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ikiwemo kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin yenye thamani ya sh. 38,638, bangi ya sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae..........
Na Mwanaharakati.

Tuesday 24 February 2015

PINA AZINDUA UANDIKISHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA

Baadhi ya watalaamu wa kuandikisha wapiga  wakiwa na zana za kazi kabla ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ya kuzinua Uborereshaji wa Daftari kla Kudumu la Wapigakura  katika mji mdogo wa Makambako Februari 24, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua  Uborereshaji wa Daftari kla Kudumu la Wapigakura  katika mji mdogo wa Makambako Februari 24, 2015.Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva na Katikati ni Katibu wa Tume hiyo, Ndugu Malaba.



 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda   na Naibu Katibu Mkuu  ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa CHEDEMA  John Mnyika wakitazama kadi mpya ya mpigakura baada ya Waziri Mkuu, Kuzindua uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura  katika mji mdogo wa Makambako  Februari 24, 2015..(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Na Mwanaharakati.