Taarifa imeeleza kuwa Amissi Tambwe, Kpah Sherman, Haruna Niyonzima na Mbuyu
Twite kuzuiwa kwa saa moja kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Seretse Khama, mjini Gaborone, Botswana.
Mbrazili Coutinho hakuondoka na wenzake kutokana
na kuwa majeruhi wa goti aliloumia katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya
Mbeya City mwishoni mwa wiki.
Yanga iliwasili Gaborone saa 4: 35 asubuhi (5:35
kwa saa za Tanzania) na kukutana na kadhia hiyo baada ya wachezaji wake
kulazimika kukaa hapo kwa zaidi ya saa wakisubiri suala la wenzao
kukamilisha taratibu za uhamiaji.
Wakati wachezaji wakipita katika ukaguzi wa pasi
za kusafiria.........
, zile za nyota hao wa kigeni zilionekana na dosari ndogo ambazo uongozi wa Yanga umetamka kwamba walifichwa wakati wakiulizia mambo ya muhimu kuhusu safari yao.
, zile za nyota hao wa kigeni zilionekana na dosari ndogo ambazo uongozi wa Yanga umetamka kwamba walifichwa wakati wakiulizia mambo ya muhimu kuhusu safari yao.
Maofisa hao wa usalama walianza kumzuia Mrundi
Tambwe akifuatiwa na Mliberia, Sherman kabla ya kuhamia kwa Wanyarwanda,
Twite na Niyonzima.
Maofisa hao walidai kuwa raia hao wa kigeni
walitakiwa kuwa na viza za kuingilia nchini humo hati ambazo zilikuwa na
msamaha kwa wachezaji na viongozi Watanzania pamoja na kocha Mholanzi,
Hans Pluijm.
Kutokana na hali hiyo, mkuu wa msafara wa Yanga
kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ayoub Nyenzi akiwa na Katibu
Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tibohora walimwaga fedha kuwaondoa wachezaji hao
katika kizuizi. Akizungumzia hali hiyo, Tiboroha alisema walishangazwa
na hatua hiyo ya wachezaji wao kuzuiwa kutokana na awali wakati wanapata
taarifa ya nyaraka wanazotakiwa kukamilisha hawakuambiwa kuhusu hayo.
“Hizi ni siasa za mpira, Yanga tumeshangazwa na
hili tuliuliza mapema kule katika ofisi zao za ubalozi wa Botswana
jijini Dar es Salaam hatukuambiwa kama kuna hili la viza tunatakiwa
kulifanya.
Hata wao wakati tunawapokea kule kwetu walikuwa na
wachezaji wageni kutoka Zimbambwe, hawakufanyiwa haya, tumelazimika
kutoa fedha nyingi ili kuwaondoa wachezaji wetu pale uwanjani,” alisema
Tiboroha.
Katika hatua nyingine, Yanga ikiongozwa na makamu
mwenyekiti wake, Clement Sanga iligomea basi na hoteli waliyoandalizi wa
wenyeji wao, BDF XI kwa kuhofia hujuma.
Sanga ameliambia gazeti hili kuwa jambo la kwanza
ambalo uongozi wao uliligomea baada ya kujiridhisha ni hoteli isiyokidhi
viwango vya timu yao ambapo wanajeshi hao walipanga timu ifikie katika
eneo lisilokuwa na utulivu wa kutosha.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment