MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Saturday 30 June 2012

KASIBANTE LIVE NDANI YA SABA SABA 2012

Jamani sikuewpo kwa muda mfupi katika masuala ya kikaziambazo zilinifanyakutokufanya kazi blog but kwa sasa nimerejea. Baada ya kuwasili kazi ya kufanya live kwenye viwanja vya maonesho ikaanza na hii ni mitambo ya live KFM.



MAONESHO YA KILIMO NA BIASHARA SABASABA MWAKA HUU YAPENDEZA MAPEMAAAAAAAA.

Yanafanyika katika viwanja vya CCM ambapo washiriki mbalimbali zikiwemo Redio za mjini humo zimeshiriki kurusha matangazo Live (KASIBANTE REDIO na VISION FM)




BALIMI YAKAMILISHA ZOEZI LA KUSAKA MSHINDI WA NGOMA ZA ASILI KAGERA

MMgeni rasmi katika mashindano hayo uwanjani kaitaba mjini Bukoba alikuwa mkuu wa wilaya ya Bukoba Bi ZIPORA PANGANI.






Ras Niga kichwa ya simba ni miongoni mwa waimbaji wa ngoma, ambapo makundi saba yameshiriki mashindano hayo.

ASKARI ANAPOMKAMATA RAIA BILA MKOSA WANANCHI WAKABAKI WANALALAMIKA BILA KUSAIDIA

 Kijana mmoja katika manispaa ya Bukoba amekamatwa na askari wa usalama barabarani baada ya kuonekana kama amelewa jambo ambalo limewasikitisha jamaa zake walioshuhudia hali hiyo, lakini kinachowauzunisha wananchi zaidi ni kumkwida kijana huyo kitendo wanachodai ni unyanyasaji.
 Hapa kuna maswali kuhusu kutii sheria bila shuruti kwamba kweli inawezekana?

Sunday 3 June 2012

KIMATAIFA

WAKATI NDEGE INAUA 10 NCHINI GHANA, BOMU LAUA KADHAA KATIKA KANISA NIGERIA, LAKINI WAKATI HUO KOFFI ANNA AMSISITIZA ASSAD KUKOMESHA MAUAJI SYRIA NA WAASI WA TUAREG WATAFUTA SULUHU KULE NCHINI MALI.
Mjumbe wa amani wa kimataifa Kofi Annan ameyashutumu majeshi ya rais wa Syria Bashar al-Assad kwa mauaji pamoja na kuwakamata watu kinyume na sheria . 

Annan , ambaye  ameteuliwa  kuwa  mjumbe  maalum  nchini  Syria na  umoja  wa  mataifa  pamoja  na  umoja  wa  mataifa  ya  Kiarabu, Arab League, amesema  uwezekano  wa  kutokea  vita  vya wenyewe  kwa  wenyewe  unakuwa  mkubwa   kila  siku  na  kutia wasi  wasi  mataifa  mengine  ya  mashariki  ya  kati.
Waasi wa Tuareg na viongozi wa kundi la Kiislamu kaskazini mwa Mali wanajaribu kutafuta muafaka, baada ya Watuareg kuukataa mpango wa kuanzisha taifa lililojitenga na Mali lenye kufuata sheria za kiislamu yaani Sharia.

Viongozi wa Vuguvugu la Tuareg la Ukombozi wa Azawad (MNLA) na wa kundi la Ansar Dine walikutana katika mji wa kaskazini mashariki wa Gao ikiwa ni June 1 2012 baada ya MNLA kusema kuwa imeachana na mpango wa makubaliano yaliyodumu kwa wiki moja kwa sababu kundi la Ansar Dine kusisitiza utumiaji wa Sharia.

Saturday 2 June 2012

LVEMP WASISITIZA UTUNZAJI WA MITO INAYOMWAGA MAJI ZIWA VICTORIA

Maazimio mbalimbali yamepitishwa ambapo jambo kubwa ni utekelezaji mbandala wa sheria ya utunzaji mazingira.
 Waandishi wa habari wamependekeza awekwe mratibu kila halmashauri ili aweze kuwa kiunganishi cha halmashauri na LVEMP ili kuendeleza utunzaji wa mazingira.
 Baadhi ya washiriki wametembelea bandari ya Bukoba ili kujionea shughuli za meli kwani nayo ni mojawapo ya vyanzo vya uchafuzi wa maji ziwa victoria.