MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday, 3 June 2012

KIMATAIFA

WAKATI NDEGE INAUA 10 NCHINI GHANA, BOMU LAUA KADHAA KATIKA KANISA NIGERIA, LAKINI WAKATI HUO KOFFI ANNA AMSISITIZA ASSAD KUKOMESHA MAUAJI SYRIA NA WAASI WA TUAREG WATAFUTA SULUHU KULE NCHINI MALI.
Mjumbe wa amani wa kimataifa Kofi Annan ameyashutumu majeshi ya rais wa Syria Bashar al-Assad kwa mauaji pamoja na kuwakamata watu kinyume na sheria . 

Annan , ambaye  ameteuliwa  kuwa  mjumbe  maalum  nchini  Syria na  umoja  wa  mataifa  pamoja  na  umoja  wa  mataifa  ya  Kiarabu, Arab League, amesema  uwezekano  wa  kutokea  vita  vya wenyewe  kwa  wenyewe  unakuwa  mkubwa   kila  siku  na  kutia wasi  wasi  mataifa  mengine  ya  mashariki  ya  kati.
Waasi wa Tuareg na viongozi wa kundi la Kiislamu kaskazini mwa Mali wanajaribu kutafuta muafaka, baada ya Watuareg kuukataa mpango wa kuanzisha taifa lililojitenga na Mali lenye kufuata sheria za kiislamu yaani Sharia.

Viongozi wa Vuguvugu la Tuareg la Ukombozi wa Azawad (MNLA) na wa kundi la Ansar Dine walikutana katika mji wa kaskazini mashariki wa Gao ikiwa ni June 1 2012 baada ya MNLA kusema kuwa imeachana na mpango wa makubaliano yaliyodumu kwa wiki moja kwa sababu kundi la Ansar Dine kusisitiza utumiaji wa Sharia.

No comments: