Mahakama kuu kanda ya Bukoba chini ya Jaji mfawidhi wa
mahakama kuu kanda ya Bukoba Mh.Salvatory
Bangole imewahukumu watu watano wa
wilaya ya Karagwe na Kyerwa mkoani Kagera kutokana na kukutwa hatia ya mauaji.
Wakili wa serikali mkuu na mfawidhi wa ofisi ya mwanasheria
mkuu wa serikali mkoa wa Kagera Hashimu
Ngole amesema kuwa tarehe 24 may mwaka huu walianza kikao cha kesi za
mauaji ambazo kimsingi husikilizwa na mahakama kuu,na leo kikao hicho ndo
kimefikia hatima yake.
Aidha amesema kuwa kupitia kesi tisa walizokuwa wanasikiliza
leo wamefanikiwa kukamilisha saba,kesi moja mshitakiwa alikufa na kesi nne
zimetolewa maamuzi.
Kesi ya kwanza ilikuwa na washitakiwa wawili Dastan Makwaya na Jovith Mutagaywa John ambapo walikuwa wanashitakiwa kwa kosa
lililofanyika june 17 mwaka 2013 la kumuua Oscar
Martin mkazi wa kijiji Kagenyi wilaya ya Kyerwa kwa kumchoma kisu kifuani,
watuhummiwa hao wamekutwa na hatia na mahakama imewahukumu kunyongwa hadi kufa.
Kesi ya pili ilikuwa na washitakiwa watatu,Oswald Wilibard,Vicent Clement na Kato simon
ambapo walikuwa wanashitakiwa kwa kumuua Elizeus
Edimund wa kijiji Kabare wilaya Karagwe mnamo june 16 mwaka 2016,walimfunga
kamba mikononi,tumboni na miguuni kisha wakamuning’iniza mpaka kufa na baada ya
mahakama kupitia ushahidi imewahukumu wawili kunyongwa hadi kufa ambao ni Vicent Clement na Kato Saimon,pia Oswald
Wilbard ameachiwa huru baada ya kuonekana hana hatia.
Kesi ya tatu ilikuwa na mshitakiwa mmoja Ilida Innocent ambaye alikuwa
anashitakiwa kwa kumuua mme wake Innocent
Kiiza kwa kula njama na majambazi ambao walimkata mapanga mpaka akapoteza
maisha,naye amehukumiwa kunyongwa hadi
kufa.
Na kesi ya nne ilikuwa na mshitakiwa mmoja Nuriath Mzakiru ambaye alikuwa
anashitakiwa kwa kumuua mme wake Mzakiru
Mohamed wa kijiji Kibwera wilaya ya Karagwe mnamo july 26 mwaka
2013,alimuua kwa kumpiga na shoka kichwani, kumkata sehemu zake za siri na
kumumwagia maji ya moto,na mahakama wakati ikiendelea na kesi yake alionekana
kama mwendawazimu na amewekwa gerezani mpaka siku ukitokea msamaha wa Rais.
Kwa upande wake wakili wa washitakiwa Jackline Mlema amesema kuwa aliteuliwa kufanya kazi ya kuwatetea
washitakiwa hao na amefanya kazi kwa uaminifu huku akisema kuwa kufatia hukumu
iliyotolewa bado kuna safari ya kukata rufaa katika mahakama ya rufaa ambayo
itatenda haki na kutoa notice .
Mahakama kuu kanda ya Bukoba chini ya Jaji mfawidhi wa
mahakama kuu kanda ya Bukoba Mh.Salvatory
Bangole imewahukumu watu watano wa
wilaya ya Karagwe na Kyerwa mkoani Kagera kutokana na kukutwa hatia ya mauaji.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment