Baadhi ya wananchi katika kata ya Rubale iliyopo halmashauri
ya wilaya Bukoba wameungana na serikali katika kuwezesha kata yao kupata shule
ya serikali kwa kidato cha tano na sita jambo ambalo wanaamin litawasaidia kuinua
kiwango cha elimu katika maeneo yao.
Wakiongea macmedianews.blogspot.com,wamesema kuwa wamejitoa
kuchangia mchanga,matofali,mawe na kokoto kwa kila kaya inayojiweza huku
wakiiomba serikali kuwaunga mkono kwa kuwanunulia vifaa vya madukani ili kuhakikisha wanakamilisha kwa muda
uliopangwa.
Kwa upande wake afisa mtendaji wa kata Rubale Bw.Abdala
Rwabigimbo amesema kuwa muitikio wa wananchi ni mzuri lakini wameshirikisha kata
za jirani kwa ajili ya kuongeza nguvu maana wanataka ujenzi uanze rasmi mwezi
wa sita.
Aidha ameongeza kuwa wana mpango wa kujenga mabweni,jiko na
bafu maana madarasa ya kutumia tayari yapo,huku akisema kuwa kwa upande wa
fedha ipo million mbili ya kuanzia na serikali ipo mbioni kuwaunga mkono.
Diwani wa kata Rubale Stanslaus Rutta amesema kuwa mradi huo
wameshauombea fedha lakin hazijapatikana ila wanasubili kikao cha bajeti cha
bunge kiishe ili waweze kupata hizo fedha zitakazounganishwa na nguvu za
wananchi ili kufanikisha ujenzi huo
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment