Meli
hiyo iliyoondoka katika bandari ya Bukoba jana usiku, mfuko wake wa kuendeshea meli ulishindwa, ikiwa
zimebakia maili kadhaa kabla ya kufika katika bandari ya Kemondo.
Kapteni
wa meli hiyo, Bempele Samson amesema kuwa mfumo wa meli hiyo ulishindwa ikiwa
majini kabla ya kufika katika bandari ya Kemondo na kulazimika kutumia mfumo wa mbadala ili
kuiwezesha kufika katika bandari hiyo.
Naodha wa meli hiyo Bwana Samson akihojiwa na mtandao huu. |
Wakizungumza
na mtandao huu, baadhi ya abiria hao wamesema kuwa kushindwa kwa mfumo huo , kuliibua
hofu kubwa miongoni mwa abiria na kufanya baadhi yao kuanza kuangaika.
Abiria
hao wameitaka serikali kupitia kwa rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Kikwete kutekeleza ahadi
yake ya kununua meli mpya aliyoitoa wakati wa kampeni za uchagunzi mwaka 2010.
Picha juu na chini ni abiria pamoja na mizigo yao kama ndizi mbivu na mbichi ambazo wanasema kuwa zitaharibika kabla ya kufika Mwanza. |
Afisa SUMATRA mkoani Kagera Bw Alex Katama, ametueleza kuwa mpaka sasa wamemsubiri fundi kutoka bandari ya Mwanza ili kufanya marekebisho ya mfumo wa meli hiyo, huku akisema kuwa unafanyika utaratibu wa kurudidha nauli za baadhi ya abiria ambao wameondoka na usafiri mwingine, huku wengine ambao hawataki tena kusafiri watarejeshewa pia pesa zao za nauli.
Na Mwanaharakati.
1 comment:
Shocked. How can this happen repeatedly? We need explanations from the responsible government leaders. Probably, from Hon Mwakyembe and his deputy Hon Tizeba. They must tell us what went went wrong and why? I still remember that darkest day when Mv Bukoba capsized. It was one of the darkest day i will never forget. We lost our loved ones, brothers, sisters, fellow staff members, neighbours, and all what one can mention . Please, please, tell us why this is reminding us tbe event in the same generation?
Post a Comment