Taarifa ya ndani
ya Oktoba 2, mwaka huu ya Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu Dar es Salaam
iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, imesema askari hao walisimamisha gari
dogo na baada ya dereva kujitetea, waliendelea kutafuta makosa hali
iliyosababisha abiria aliyekuwa mgonjwa kufariki.
Kutokana na
tukio hilo, makamanda wa polisi wa wilaya zote za Mkoa wa Kipolisi wa Dar es
Salaam wametakiwa kuwakumbusha askari wao kuepuka kutolazimisha kutafuta makosa
ambayo hayana madhara.
“Makosa ambayo
hayana madhara katika kusababisha ajali mfano ni vifaa vya kuzimia moto, rangi,
kadi kutoandika anuani, motor vehicle, leseni chini ya siku 30 na kadhalika,”
lilisomeka agizo hilo kwa makamanda hao wa polisi.
Na Mtanznia
No comments:
Post a Comment