MULEBA
Mashindano ya michezo kwa
shule za sekondari{UMISETA}yamezinduliwa rasmi katika chuo cha uwalimu
katoke mkoani Kagera kwa kushirikisha wilaya zote za mkoa wa Kagera zikiwa na
jumla ya wanamichezo 469.
Akiongea mbele ya mgeni rasmi,Afisa elimu mkoa Kagera Aloyce
Kamamba amesema kuwa wanaoshiriki michezo ni jumla ya wanamichezo 469,walimu na
maafisa elimu 40,wanafunzi ni wasichana 192 na wavulana 277 huku akisema kuwa
hatua ya kwanza itakamilika may 29 mwaka huu na kupata timu moja ya mkoa
itakayokuwa na wanamichezo 91 na walimu 15.
Aidha amesema kuwa may 30 mwaka huu timu hiyo itaanza kambi
mpaka june 4 ambapo june 5 itareport chuo cha uwalimu Butimba jijini mwanza kwa
ajili ya kushiriki mashindano kitaifa ambayo yanatarajia kukamilika june 17
mwaka huu.
Pia Kamamba amesema kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo
ni pamoja na baadhi ya halmashauri ukitoa ya Bukoba,Karagwe na Kerwa
zimeshindwa kukamilisha michango yao kifedha kwa ajili ya kuendesha mashindano
hayo hali inayosababisha baadhi ya vitu kukwama.
Akizindua mashindano hayo,Katibu tawala mkoa wa Kagera Kamishina
wa polisi Diwan Athuman ametoa siku tatu kwa wakurugenzi wa halmashauri zote ambazo hazijakamilisha
michango hiyo kuhakikisha wanazitoa ndani ya muda huo na apate mrejesho wao.
Sanjali na hayo amewasihi wanamichezo kufanya vizuri katika
mashindano yao ili kuhakikisha mkoa wa kagera unafanya vizuri hatua ya kitaifa
itakayoanza june 5 mwaka huu.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment