Akizindua shughuli hiyo Naibu waziri wa Kilimo,mifugo na
uvuvi mh.William Ole Nasha amesema kuwa nchi ya Tanzania ina changamoto kubwa
kwa upande wa matumizi ya maziwa ambapo kwa mwaka mtanzania mmoja anatumia
wastani wa lita 47 ambayo ni chini ya robo ya kiwango kinachopendekezwa na
shirika la afya duniani badala ya lita 200,hali aliyosema inasababisha hata
kuendelea kwa kiwango kikubwa cha udamavu kwa Watanzania.
Pia amewasihi wananchi kuhudhuria kwa wingi katika kipindi
hiki cha wiki ya maziwa ili waweze kupatiwa elimu ya kutosha juu ya matumizi ya
maziwa ikiwa ni pamoja na kutambua magonjwa unayoweza kupata usipokunywa
maziwa.
Wiki ya maziwa kitaifa imezinduliwa leo mkoani kagera katika viwanja
vya Kyakairabwa vilivyopo ndani ya manispaa ya Bukoba ambayo itafikia kilele june 1 mwaka huu,ikiwa na lengo la kutoa elimu
kwa wananchi juu ya matumizi ya maziwa.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment