Wito umetolewa kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya
Tanzania -TADB kuwafikia wakulima, wafugaji na wavuvi wadogo nchi nzima ili
kuweza kuwakwamua katika changamoto zinazorudisha nyuma juhudi zao za
kujiongezea kipato kwa kukosa mitaji ya uhakika katika kuongeza tija ya kilimo
nchini.
Wito
huo umetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Tate
Ole Nasha (MB) wakati akifungua rasmi Maadhimisho ya Kampeni ya Wiki ya Maziwa
inayofanyika Kitaifa mjini Bukoba, mkoani Kagera.
Mhe.
Ole Nasha amesema kuwa dhima ya kuanzishwa kwa TADB ni kutoa suluhisho la
ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha na mikopo kwa wakulima wadogo nchini ili
kuchagiza maendeleo ya kilimo nchini hivyo Benki ina wajibu wa kuwafikia
wakulima wote wadogo wenye uhitaji wa mikopo.
“Nawaomba
mujielekeze kutoka mikopo yenu ya gharama nafuu kwa wakulima wadogo ambao
hawawezi kupata mikopo kwenye benki za biashara ili kutekeleza lengo la
Serikali la kuwainua wakulima kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara
ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini,” Mhe. Ole
Nasha alisema.
Aliongeza
kuwa anafahamu kuwa Serikali ikishirikiana na TADB ilifanya mazungumzo na Benki
ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na kupelekea Bodi ya Benki ya Maendeleo Afrika
kutoa kibali cha kuipatia TADB fedha za kukopesha kwenye sekta ya kilimo, na
kuitaka Benki hiyo kutumia fedha hizo kwa kuwapatia wakulima wadogo ambao ni
wahitaji zaidi wa miko hiyo.
“Naomba
muwakopeshe wakulima hizo fedha ya zaidi Bilioni 200 ili kuwaongezea tija
katika shughuli zao,” aliongeza.
Kwa
mujibu wa mpango kazi wa TADB hadi kufikia miaka mitano ijayo itakuwa imefungua
ofisi sita za kikanda zenye lengo la kuwahudumia wakulima wote nchini. Ambapo
katika hatua za awali Benki hiyo inaendelea kuwajengea uwezo wakulima wa nchi
nzima ili kuwaandaa kupata mikopo kutoka Benki hiyo.
Mpango
kazi huo unaweka bayana malengo mengine yanayojumuisha utafutaji wa fedha toka
vyanzo mbalimbali zenye gharama nafuu kwa minajili ya kuwakopesha Wakulima
katika hatua zote za mnyororo wa ongezeko la thamani kwenye mazao ya Kilimo na
kupanua wigo wa utaoji mikopo toka Minyororo Kumi na Minne (14) ya mwanzo na
kuhusisha pia mazao mengine ya Kilimo na pia kuwaunganisha wakulima na masoko
ya ndani na nje ya nchi.
TADB
ni taasisi ya serikali ambayo ilianzishwa kwa ajili ya kutatua ufinyu mkubwa wa
upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini ambao
ulikuwa unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha
kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa; riba kubwa kwenye mikopo
ya kilimo; mikopo ya muda mfupi; masharti magumu ya kukopa bila kuzingatia hali
halisi ya sekta ya kilimo na mazao ambayo inaathiriwa kwa kiasi kikubwa
na mabadiliko ya hali ya hewa.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment