MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Friday, 27 February 2015

NDEGE YATEKETEA MWANZA


Taarifa inasema kuwa ni ndege ya jeshi la wananchi JWTZ, ambayo imeanguka katika viwanja vya jeshi wilayani Ilemela mkoani Mwanza, ambapo hakuna aliyepoteza maisha.

Inasemekana ndege hiyo ambayo hatujapata namba yake, imeteketea kabisa, huku rubani aliyekuwa ndani yake amenusurika katika ajali hiyo na hakuna aliyepoteza maisha kwasababu alikuwa pekee kwenye ndege hiyo...................


Ni ndege hiyo ya  ya Jeshi ambayo hubeba mabomu, ilikua kwenye mazoezi ya kawaida ambayo hufanyika mara kwa mara. Lakini kwa leo haikuwa na mabomu na ilikuwa na Rubani pekee, ambaye inasemekana amepata majeraha kidogo baada ya kuruka na mwavuli na kukimbizwa hospital ila ndege yote imeteketea kwa moto.
Na Mwanaharakati.

No comments: