. Ni katika kikao maalumu cha ulinzi na usalama,
. Wasema na wao siasa wanaziweza ila
wanafanya kazi ya Mungu,
. Baadhi ya wanasiasa CHADEMA kulazimisha
wananchi kukaa mita 200.
Viongozi wa vyama vya siasa wametakiwa
kuacha mara moja kuchochea wananchama wao kuleta vurugu wakati wa uchaguzi
mkuu.
Hatahivyo wametakiwa kutambua kuwa wanachama hao ndiyo waumini wa kanisa na
misikiti, hivyo ghasia zitahatarisha siyo wanasiasa pekee kwani wanahitajika
sehemu zote husika, dini na siasa.
Msaidizi wa askofu katika kanisa la Anglikan
Canon Elisha Bililiza, amesema kuwa
viongozi wa dini nao wanaweza kufanya
siasa, kufanya kazi ya ulinzi na sasa wanafanya kazi za kuhubiri waumini ambao
hatahivyo ndiyo wanachama wa vyama vinavyoongozwa na wanasiasa, ambao baadhi
yao wanawahamasisha wakae vituoni kulinda kura, jambo ambalo ni kinyume na
sheria za nchi.
Hatahivyo makatibu wa vyama, akiwamo
Sadick Amzakatibu NCCR Mageuzi, Francis
Batu wa CUF na TLP, wamesema kuwa hawakotayari kuona wapiga kura wanasalia
vituoni, kwani wanatambua utaratibu wan chi hauruhusu na hawataki kuwa chanzo
cha kuondoa amani iliyodumu kwa miaka yote Tanzania.
Mkutano huo maalumu, umeitishwa na
mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ambaye pia ni mkuu wa
wilaya hiyo Bwana Jackson Msome, kwa kuwashirikisha viongozi wa dini, viongozi
wa siasa na kamati nzima ya ulinzi na usalama pamoja na waandishi wa habari.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment