Shakira Abdallah mwenye umri wa
miaka 24 ametelekezwa na mume wake kwa miaka minne baada ya kupata ulemavu wa
viungo na hatimaye kushindwa kuongea.
Mtandao huu umefanya mazungumzo
na babu wa Shakira, mzee Hamis Waziri
anasema
kuwa katika kipindi chote cha uzima wa mjukuu wake alikuwa akiongea nae
mara kwa mara kwa njia ya simu ili kujua hali yake na baadae mawasilainao ya
kuongea yakashindikana, jambo lililowafanya washtuke walipoona ukimya ambao
awali haukuwepo.
Sikiliza simulizi ya babu wa Shakira
kama alivyozungumza na mtandao huu…
"Mama yake na bibi waliamua kuuza shamba na
kufunga safari ili kumjulia hali mjukuu wao ambaye wakati huo alikuwa
ameshalemaa na alikuwa hawezi tena kuongea.
Anasema kuwa mjukuu wake
alichukuliwa kutoka Mtwara kwenda Dar na rafiki wa mama yake aliyekuwa akiishi
jirani yao aliyejukana na kwa jina la Ashura kwa muda wa miezi sita hadi na
kufanikiwa kupata mchumba aliyemuoa kwa ridhaa ya mjomba yake aishie.
Waziri anasema kuwa kitendo cha
mjukuu wake kupata ulemavu bila wao kujua ilikuwa ni pigo kubwa kwa familia
nzima kwakuwa mume wake alimteyekeza bila kumpatia huduma yoyote.
“Mimba yake ilipofika miezi nane
alikuwa akitupigia simu na kusema kuwa akiwa chumbani kwake anaona vitu vya
ajabu ajabu hali ambayo ilitulazimu kumuomba mume wake amlete ili aweze
kujifungulia huku lakini alikataa.
“Mjukuu wetu anateseka sana ukimuona
huwezi amini kama alizaliwa akiwa mzima akawa anatembea na kuongea kitendo
alichofanyiwa sio kitendo cha ubinadamu tunaomba serikali itusaidie ili aweze
kupata stahiki zake kwakuwa hakupewa talaka na mume wake” alisema Waziri
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment