MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday, 18 October 2015

MTOTO WA WAZIRI AKUTWA AMEFARIKI CHUONI

Ni Zanele Moyo mtoto wa waziri wa afya nchini Zimbabwe profesa Jonathan Moyo ambapo taarifa za awali zinasema kuwa amekutwa amefariki katika chumba chake kwenye chuo kikuu nchini Afrika kusini, Jana tarehe 17 jumamosi.

Kikosi maalumu cha polisi nchini humo kimesema kuwa sababu ya kifo inachunguzwa na kueleza kuwa wanaendelea na uchunguzi pamoja na kuifahamisha familia ya Moyo sambamba na kuipa ushauri nasaha.

Zanele Moyo, alikuwa mwanafunzi katika kitivo cha sayansi ya siasa na utawala bora, katika chuo hicho, kama alivyofafanua Gerda Kruger ambaye ni mkuu wa chuo hicho UCT.
Na Mwanaharakati.

No comments: