PICHA HII IKIMWONESHA MLALAMIKAJI ALIPOINGIA OFISI KWA MKUU WA MKOA.
Abel mwesa amesema iwapo mkuu wa mkoa hatofanya
hivyo kwa muda uliotajwa atamfungulia mashitaka ya udhalilishaji. Tarehe 14
kijana Lazaro Robert alifika katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Mwanza kutoa
taarifa za kung'atwa na kiongozi huyo wa CHADEMA akililaumu jeshi la polisi
kushindwa kumtia nguvuni mtuhumiwa. Kutokana na madai hayo mkuu wa mkoa wa
Mwanza alitoa agizo kwa polisi kumkamata mtuhumiwa wa tukio hilo ambaye aliwekwa rumande kwa siku 2
Nae Lazaro Norbet amesisitiza kufanyiwa kitendo
hicho na katibu huyo wa CHADEMA wilaya ya Ilemela akisema kuwa maelezo yake ya
awali yalitofautianana na kumtaja mtu mwingine kutokana na mikwara
aliyopigwa kwamba iwapo atamtaja katibu huyo kuhusika basi chamoto
atakiona.
Katika hatua nyingine akizungumza na vyombo vya habari jana katika
ofisi Kuu ya CCM Mkoa wa Mwanza Katibu wa siasa Itikadi na Uenezi Bw. Saimon
Mangelepaa amesema kuwa CCM imesikitishwa na kitendo cha kiongozi wa juu
(KATIBU) wa Wilaya ya Ilemela cha kujichukulia sheria mkononi na kumfanyia
kitendo cha unyama kijana Nolbert kitendo ambacho hakina budi kulaaniwa na
wananchi bila kujali tofauti za kisiasa zilizopo kwa vile ni kitendo cha
kinyama kwa jamii na kimeonyesha kiongozi huyo hatambui wajibu wake kwa kuvunja
sheria na kujichukulia uamuzi wake binafisi ambao umemsababishia kijana huyu
ulemavu wa kudumu.
No comments:
Post a Comment