JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
TAARIFA
KWA UMMA
BODI
YA USHAURI YA WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA (TFS) YATEULIWA
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi Khamisi
S. Kagasheki (Mb) kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa
Serikali (Executive Agencies Act) Sura 245 amewateua wajumbe saba (7) kuunda
Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania
(Tanzania Forest
Service - TFS). Aidha, Waziri Kagasheki amemteua Bibi. Ester Mkwizu kuwa
Mwenyekiti wa Bodi hiyo.
Wajumbe wa Bodi hiyo ya Wakala wa Huduma za
Misitu ni kama ifuatavyo:-
1. Bibi. Esther Mkwizu – Mwenyekiti, kutoka Sekta Binafsi (Tanzania
Private Sector Foundation), Dar es
Salaam ;
2. Bibi. Gladness Mkamba - wa Wizara ya Maliasili na Utalii;
3. Eng.
Bonaventura T. Baya – wa Baraza la Taifa
la Usimamizi wa Mazingira (NEMC);
4. Bw. Sosthenes Sambua - wa Dar
es Salaam ;
5. Prof. Yonika Ngaga - wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Morogoro;
6. Dkt. Himid Majamba - wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam - Sheria; na
7. Bw. Rawson Yonazi – wa Dar es Salaam .
Uteuzi wa Bodi hiyo ni kwa kipindi cha miaka
mitatu (3) tangu tarehe 1 Desemba 2011 hadi 30 Novemba 2014.
George
Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
17 Mei
2012
No comments:
Post a Comment